Monday, 28 May 2018

JE UMEZALIWA MARA YA PILI?

  

"Nilizaliwa mara ya pili nikiwa na umri wa miaka tisa na bado ninakumbuka sana nilivyojihisi kana kwamba nilisuguliwa ndani. Nilijihisi msafi , mwepesi, upya na mchangamfu ndani yangu."-jimmy

Inamaanisha nini kuzaliwa mara ya pili?  Katika kitabu cha  Yohana Mtakatifu 3:3   Yesu alisema, “Amini, amini, nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.”Nikodemo ambaye  Yesu alikuwa akimzungumzia hapa alisema “Awezaje mtu kuzaliwa akiwa mzee?  Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?” (Yohana Mtakatifu 3:4) Labda wewe pia unafi kiri vivyo hivyo.

Je mtu awezaje kuzaliwa ambaye tayari ameshazaliwa?  Yesu anazungumzia kuzaliwa kiroho. Hapo mbeleni nilisema wewe ni roho, una nafsi na unaishi katika mwili.   Mwili wako tayari umezaliwa lakini Biblia inafundisha kwamba roho na nafsi zetu zimekufa na zimejaa giza kwa sababu ya dhambi.
  • Unaweza kujitazama katika kioo, ukatingiza kichwa chako, mikono na miguu. Unavuta pumzi. Unaweza kusema uko hai. Lakini je, yule “wewe wa kweli” yuko hai?
  • Je uko hai na una nuru ya kutosha ndani  yako? Una amani? Je  nafsi yako ina amani na utulivu? Je unajipenda? Una furaha na tumaini?  Je unaogopa kifo? Haya ni maswali unayopaswa kujiuliza mwenyewe.

Unaweza kutabasamu usoni mwako lakini iwe ndani hauna furaha. Wakati  Yesu alikuwa akimzungumzia kuhusu kuzaliwa mara ya Pili, alikuwa akifundisha kwamba mtu wa ndani lazima  awe hai kwa Mungu.

Yohana Mtakatifu 3:6 “Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.” Wamama wanapojifungua na kupata watoto, ni mwili unaozaliwa na mwili. Roho wa Mungu anapoingia kwa roho ya mtu ndipo unapozaliwa rohoni. Hii inaitwa “kuzaliwa upya.”
Roho Mtakatifu huingia kwa roho ya mtu kwa njia moja tu. Unaweza kuzaliwa mara ya pili kwa njia moja tu. Sawa na  jinsi mtu huzaliwa kimwili mara moja ndivyo ilivyo hata katika kuzaliwa kwa roho. Huwezi kujipatia maisha ya kiroho kibinafsi sawa na jinsi huwezi kujizaa mwenyewe. Kuna utaratibu wa kufuatiliwa ili mtoto azaliwe na vivyo hivyo kuna utaratibu wa kiroho ambao lazima ufuatwe ili kuzaliwa upya. 

Je utaratibu huo ni nini?  Ukiamua leo kwamba unataka kuzaliwa mara ya pili, je utafanya nini? Kwanza, lazima utambue na kukubali kwamba umekufa kiroho kutokana na dhambi maishani mwako.   Warumi 3:23 inasema “Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.”  Hakuna mtu ambaye hana dhambi.  Usiogope kusema wewe ni mwenye dhambi.  

Waraka wa kwanza wa  Yohana 1:8 “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo ndani mwetu.” Kifungu cha tisa kinasema “Tukiziungama dhambi zetu,  Yeye ni Mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafi sha na udhalimu wote.” Mpendwa, hii ni habari njema. Ndiposa injili inaitwa habari njema. Kwa hiyo tunaona kwamba  hatua ya kwanza  katika kuzaliwa mara ya pili ni  kukubali  wewe ni mwenye dhambi. Hii inamaanisha kuwa unakubali ukweli unaokuhusu. Ni vigumu kukubali ukweli. Ni jambo la kuhuzunisha kukubali makosa yetu.

Shetani anataka uishi katika uongo. Mungu anataka ukubali ukweli. Hatua ya pili  ni  kukiri  dhambi zako.  Kukiri kunamaanisha kuzungumza. Hatua hiyo inaleta kusafishwa unapokiri kwa kinywa chako makosa uliyoyafanya na unayotaka kuondolewa. Mambo hayo yamo ndani yako, na ni kumbukumbu ya mambo hayo, na kule kuyahisi kuwa ni makosa ambako kumekujaza giza.   Yakiri kwa Babako aliye Mbinguni. Hii ndio njia ya Mungu ya kukukomboa kutoka kwayo. Unayaondoa kwa kuyakiri naye Mungu anakupa msamaha. Ni kama kuoshwa ndani.

Nilizaliwa mara ya pili nikiwa na umri wa miaka tisa na bado ninakumbuka sana nilivyojihisi kana kwamba nilisuguliwa ndani. Nilijihisi msafi , mwepesi, upya na mchangamfu ndani yangu.
Mpendwa, unaweza kuingia bafu na kuosha mwili wako. Unaweza kujisugua nje mpaka ukawa safi , lakini ni  Yesu pekee ambaye anaweza kukusafi sha  ndani.

No comments:

Post a Comment