Naendelea kushangazwa na waislam wanavyozidi kutangatanga na mitazamo tofauti Wenyewe kwa wenyewe na kubishana hata kile kitabu chao ili kuficha ukweli,hilo ni jambo baya sana,kuamini tu kwa sababu umeambiwa uamini maana imani bora ni kuamini kweli Kwa hiyo, ni jambo la muhimu sana tena sana kutafuta ushahidi au kuyapima tena na tena yale tunayoyaamini ili tusije kupata hasara mwisho wa safari.Kwaajili ya hilo ninapenda kuchukua fursa hii kukualika katika muendelezo wa somo letu juu ya isa /Yesu ni Mungu wasomaji na wafuatiliaji wa makala mbalimbali za Sheikh mstaafu lakini haswa katika makala hii muhimu inayo zungumzia mada hii nzito ihusuyo ukweli juu ya Bwana isa/Yesu kuwa yeye ni nani haswa kiasili? Kimsingi mada hii ni miongoni mwa mada zenye utata mkubwa katika ulimwengu wa Imani na Dini mbalimbali, maoni na mitazamo tofauti imetolewa na watu wa Dini juu ya namna wanavyoelewa kuhusu mada hii.
Quran inasema: And remember the woman who kept her chastity. We breathed into her Our Spirit, and made her and her son a sign to all men. Yaani: Mkumbukeni mwanamke aliyetunza ubikira wake. Tulimpulizia ndani yake Roho Yetu, na kumfanya yeye na mwanawe kuwa ishara kwa wanadamu wote. (Al-Anbiya 21:91). Pia, imeandikwa: And Allah has given as example Mariam, Imran’s daughter, who preserved her chastity and into whose womb We breathed Our spirit; who put her trust in the words of her Lord and His scriptures and was truly devout. Yaani: Na Allah amemtoa kama mfano, Mariamu, binti wa Imran, ambaye alitunza ubikira wake na ambaye ndani yake tulipulizia Roho Yetu; ambaye aliyaamini maneno ya Bwana na maandiko yake na alikuwa kweli mcha Mungu. (Al-Tahrim 66:12.)
Vilevile tuliyoyaona katika Sura ya AlNisa 4:171 Quran inasema: Al-Masih, Isa son of Mariam, was no more than Allah’s Apostle and His Word which He cast to Mariam; a spirit from Him. Yaani: Masih, Isa mwana wa Mariam, alikuwa ni Mtume wa Allah na Neno Lake alilolirusha (au alilolituma) kwa Mariam; roho kutoka Kwake, na si zaidi ya hapo. (Al-Nisa 4:171). Tunachojifunza hapa ni kuwa, kumbe kilichoingia tumboni mwa Mariam ni Roho ya Allah. Katika Al-Anbiya 21:91 na Al-Tahrim 66:12, tumeona Quran ikisema wazi kabisa kuwa Allah anamwita Isa roho Yetu. Na katika Al-Nisa 4:147, nako pia Quran inasema wazi kuwa Isa ni roho kutoka Kwake (yaani kutoka kwa Allah). Hapa ndipo tunapojiuliza kuwa: Je, roho ya mtu si ndiyo mtu
mwenyewe? Je, mwanao uliyemzaa ni roho yako? Tumezoea kusikia watu wakisema, ‘Huyu ni damu yangu.’ Lakini huu ni msemo tu. Katika hali halisi, damu ya baba au mama na ya watoto wao si moja hata kidogo. Ndiyo maana mzazi akiishiwa damu, daktari hawezi tu kuchukua damu ya mtoto na kumwekea mzazi, kisa tu eti ni mwanawe. Mzazi huyo anaweza kufa! Kwa nini? Kwa sababu damu zao zinaweza kabisa kuwa tofauti. Ni hadi damu hiyo itakapopimwa na kuhakikiwa kuwa zinafanana ndipo atakapopewa yule muhitaji. Kama basi damu tu haziwezi kufanana, je roho? Je, unaweza kusema kuhusu mwanao kuwa, ‘Huyu ni roho yangu?’ Haiwezekani! Sisi kama wanadamu si roho ya Mungu hata kidogo. Tunatambua kuwa
wanadamu wameumbwa kwa mfano wa Mungu.
Hakuna mwanadamu yeyote – kuanzia wanadamu wa kawaida, mitume na manabii wote - ambaye Mungu alisema, “Huyu ni roho yangu.” Sasa kwa nini, katika Quran, ambacho ni kitabu kisicho na shaka, Allah aseme kuwa Isa ni roho Yetu? Nadhani jibu ni wazi - Isa/Yesu ni zaidi ya mwanadamu. Yeye si mwanadamu wa kawaida. Sasa, kama Isa ni roho, ambaye Quran katika Al-Anbiya 21:91, AlTahrim 66:12 na Al-Nisa 4:171 inatuambia wazi kuwa ni roho ya Allah, maswali rahisi ya kujiuliza ni kuwa:
• Je, roho yangu na mimi tuko tofauti?
• Je, roho yangu si ndiyo mimi mwenyewe?
• Je, roho ya Mungu si ni Mungu mwenyewe?
Kumbuka kuwa, tunaposema mtu amekufa, maana yake ni kuwa roho yake imetoka kwenye mwili; si mwili umetoka kwenye roho. Na sote tunatambua kuwa hata yule tunayesema amekufa, yupo hai mahali fulani – iwe ni peponi au kuzimu. Lakini yupo! Na hata maiti tunaiita, ‘Huu ni mwili wa fulani.’ Hii inaonyesha kuwa kumbe kupumua, kutembea, kuongea n.k. kwa mtu kunatokana na roho iliyo ndani yake. Yaani mtu ni ile roho iliyo ndani na si mwili. Uhai wa mtu umo katika roho yake, si katika mwili wake. Ndiyo maana kwa habari ya mambo ya Mungu tunatakiwa kuelekeza nguvu zetu zote katika roho; si katika mwili. Kwa wasomaji wa Biblia wanatambua kuwa imeandikwa Roho ndiyo itiayo
uzima, mwili haufai kitu (Yohana 6:63). Pia, imeandikwa, … mwili pasipo roho umekufa ... (Yakobo 2:26). Na hili ni jambo lililo wazi tu. Kwa hiyo basi, roho ya mtu ndiyo mtu mwenyewe. Hii inatupeleka kwenye kujiuliza maswali zaidi kuwa: Je, Roho iliyoingia kwa Mariam ni ya Mungu au si ya Mungu? (rejea aya tulizosoma hapo juu). Kama Roho hiyo ilifanyika Isa, je, hakuna mantiki (logic) kusema kuwa Mungu alifanyika Isa? Ni jambo lisilobishaniwa na Quran kwamba, Isa kama mtoto alizaliwa bila baba wa kibinadamu kwa namna tofauti na ambavyo sisi tumezaliwa. Ndiyo maana anaitwa Isa ibn Mariam. Lakini, ni jambo lililo wazi pia kuwa, Isa hakutokana na Mariam peke yake. Maana kabla ya malaika kuja, Isa hakuwapo tumboni mwa Mariam.
Sasa upande wake wa pili wa Isa umetoka wapi? Tumeona jinsi ambavyo Quran imeweka wazi kabisa kuwa yeye ni roho kutoka kwa Allah. Kwa hiyo, ni wazi kuwa Isa ni mwana aliyetokana na Mungu. Je, kimantiki (logically), kuna ajabu gani basi yeye kujiita au sisi kumwita ni Mwana wa Mungu? Hata wewe msomaji hebu nisaidie hapo. Wewe unasemaje? Kulingana na aya tulizosoma, je, Isa ni Mwana wa Mungu au si Mwana wa Mungu? Kwa
nini? Lakini mimi nasema kwamba, kulingana na aya tulizosoma, tumeona kuwa, Isa kama mtoto, alitokana na Mungu. Hivyo ni Mwana wa Mungu. Kwa hiyo, Mungu ni Baba yake na Mariam ni mama yake. Vilevile, Isa ni roho ya Mungu. Ni katika msingi huu tu ndipo Ukristo unapata majina haya matatu, yaani: Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu, yaani Utatu Mtakatifu. Lakini, kama umefuatilia vizuri toka mwanzo utakuwa umegundua bila shaka yoyote kuwa, ni yuleyule na katu si watatu. Maana, roho yangu ndiyo mimi mwenyewe. Kwa hiyo, kama Yesu ni Roho ya Mungu, basi Yesu ni Mungu yuleyule. Yeye ni Mungu Baba kwa sababu yeye ni roho ya Mungu – na roho ya mtu ndio mtu mwenyewe.
Yeye ni Mwana wa Mungu kwa sababu upande wa kike ni Mariam na upande unaobaki ni Mungu. Yeye ni Roho Mtakatifu kwa sababu tumeona Quran ikisema kuwa Allah anasema Isa ni ‘Roho kutoka Kwetu.’ Yaani, ni Mungu yuleyule aliingia ndani ya Mariam. Labda unasema Mungu hazai. Hapo ina maana tu kuwa unaibishia Quran ambacho ni kitabu kisicho na shaka, inayosema kuwa Isa alitokana na pande mbili – Mariam na Allah! Ni wazi kwamba utata kuhusu Yesu, hususan kuhusu yeye kuwa Mwana wa Mungu unatokana na mtazamo wa wengi juu ya suala la uzazi. Watu wengi unapowaeleza kuhusu jambo la uzazi wa Yesu, wao hulihusisha moja kwa moja na namna binadamu anavyozaa. Watu hawa
wanachukulia kwamba, ili uzaaji utokee, basi ni lazima mwanamke na mwanamume wafanye tendo la ndoa. Huu si mtazamo mpana kiasi cha kutosha. Je, viumbe wote huzaliana kwa njia moja tu? Zipo namna nyingi zinazowezesha viumbe wachanga kupatikana. Hebu tazama mifano michache ifuatayo:
(a) Miti: Mbegu za kiume na kike hukutanishwa na upepo au na wadudu kama vile nyuki.
(b) Konokono: Mbegu za kiume na kike zipo zote ndani ya konokono huyo huyo.
(c) Bakteria na virusi: Bakteria au kirusi mwenyewe hujigawa mara mbili katikati.
(d) Samaki: Mbegu za kike na kiume hukutana zenyewe baada ya kumwagwa kwenye maji.
(e) Chawa: Uchafu tu wa mwili ukikaa katika mazingira fulani, chawa hutokea.
(f) Wanadamu: na wanyama Mbegu za kike na kiume hukutana baada ya mke na mume kukutana kimwili.
Tulichoona hapo juu ni kuwa Mungu ni mwenye uweza mkuu sana. Kuzaa si tu kitendo cha mwanamke na mwanamume kukutana kimwili. Lakini, Mungu kwa hekima yake ipitayo ufahamu wetu ameweka njia nyingi za kuwezesha wana/watoto kuzaliwa au kupatikana. Mti mchanga una baba na mama yake; samaki, chawa, konokono, virusi n.k. Kwa ujumla kila mmoja ametokana na mbegu ya kike na ya kiume. Lakini mbegu zote hazikutanishwi kwa mfumo mmoja.
Sasa kwa nini tunaposikia kuhusu kuzaliwa kwa Yesu na Mungu tuwazie au kuzungumzia tu habari ya tendo la ndoa? Bila shaka lengo linakuwa si
kushinda kwa nguvu ya hoja bali ni kutaka tu kutoa kashfa na kuwanasa wale ambao ama hawako tayari au hawana uwezo wa kuhoji kimantiki mambo wanayoambiwa. Yaani wale wanaobeba tu mambo kishabiki. Mimi nasema Yesu ni Mwana wa Mungu – na hili si kwa kadiri ya imani, bali ni kwa kadiri ya maandiko tuliyosoma. Tofauti tu ni kuwa yeye alizaliwa kwa njia tofauti na njia ya kibinadamu tunayoifahamu. Wewe msomaji unasemaje? Kwa nini?
Isa/Yesu ni huruma za Allah
Quran inasema kuwa: We shall make him a sign to mankind and a mercy from Us. Yaani: Tutamfanya kuwa ishara kwa wanadamu na huruma kutoka Kwetu. (Mariam 19:21)
Ninapenda tuangalie zaidi neno huruma (mercy). Tunafahamu bila ubishi kuwa, Mungu hashirikiani na dhambi. Na wote watendao dhambi, mwisho wao ni katika jehanamu ya moto wa milele. Hilo halina ubishi! Lakini hebu jiulize swali hili wewe mwenyewe: Je, katika kujitahidi kwangu kote, nimeweza kushinda dhambi? Yaani, sina hasira, chuki, uongo, wivu, tamaa n.k? Ni wazi hakuna mwanadamu yeyote atakayejibu, ‘Ndiyo!’ Sasa kama bado nina dhambi, mwisho wangu ni wapi? Nafikiri jibu liko wazi! Hakuna mwanadamu yeyote hapa duniani anayeweza kushinda dhambi. Hakuna! Wewe mwenyewe ni shahidi. Kutokana na ukweli huo, Mungu alifahamu kuwa, hatima ya wanadamu wote ni motoni! Kwani kila mtu si ana dhambi? Na kila mwenye dhambi lazima aende jehanamu? Sasa wa kupona ni nani? Hapa ndipo unakopatikana msingi wa huruma (mercy) ya Mungu kupitia kwa Isa/Yesu! Ndiyo maana basi Isa ni huruma ya Mungu kwetu. Lakini Isa/Yesu ni huruma ya Allah kivipi? Hapa tena ndipo linapokuja suala la waulizeni Watu wa Kitabu. Kabla Yesu hajaja duniani, wale waliopewa Torati walitakiwa kutoa damu za wanyama ili ziwe sadaka kwa ajili ya kusamehewa dhambi zao. Maana, hakuna msamaha kwa Mungu bila damu kutolewa – tena damu safi! Katika Biblia, Torati inasema, … nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho juu ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa ajili ya nafsi. (Mambo ya Walawi 17:11).
Tena imeandikwa, Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. - yaani, hakuna ondoleo la dhambi au kusamehewa dhambi – (Waebrania 9:22). Kwa kuwa Mungu ni Mungu wa nyakati na majira; amepanga historia nzima ya ulimwengu katika vipindi. Nyakati hizo walikuwa wanatoa damu za wanyama kama ishara ya kile ambacho kilikuwa kinakuja. Yaani, kipindi ambacho ingetolewa sadaka moja takatifu na kamilifu kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote. Ndiyo maana Yesu Kristo anaitwa Mwanakondoo wa Mungu. Aliuawa msalabani ili damu yake imwagike kama kafara ya dhambi za wanadamu wote. Na ndiyo maana hakuna tena haja ya kuendelea kuchinja wanyama kila unapotenda dhambi. Yesu Kristo alikufa na kumwaga damu yake kwa niaba ya wanadamu wote ili yeyote amwaminiye na kukubali sadaka/kafara hiyo awe amelipiwa deni au hukumu yake ya jehanamu. Kama huhitaji kupokea alichokifanya Yesu Kristo msalabani kwa ajili yako, unachomwambia Mungu ni kuwa, ‘Mimi nitajua nitakakotoa damu ya kutoa ili unisamehe dhambi zangu!’ –
maana hakuna kabisa ondoleo pasipo kumwaga damu safi! Swali ni kuwa, utaipata wapi? Kama ni ya kwako, haifai maana wanadamu wote tuna dhambi! Kwa maana nyingine ni kuwa, unapokataa damu ya Yesu iwe ni badala ya dhambi zako, unaikumbatia jehanamu moja kwa moja. Sasa, kama Yesu ametuponya na adhabu kubwa namna hiyo ya jehanamu ya moto wa milele, Je, Yesu si rehema/huruma (mercy) ya Mungu kwetu? Naomba nikuulize tena: Je, wewe huwa unamwaga damu gani safi ili usamehewe dhambi zako? Kama humwagi, utasamehewa kwa sababu gani?
Chukua Hatua.
Njoo kwa Yesu