Monday, 2 October 2017

DALILI LA SHAMBULIO LA KIROHO

Image result for demons

Unapoteza njaa na kimya kiroho. Unaanza kujenga mazoea na NENO, hauna muda wa maombi, unakuwa mzito kwenda kanisani, unapuuzia ibada za ktkt.. Zaburi 37:4
*Nawe utajifurahisha kwa Bwana, naye atakupa haja za moyo wako*
Uchovu wa mwili, unashindwa kuomba kwa ajili ya usingizi, maumivu ya viungo bila sababu ya maana. Yaani hujafanya kazi nzito ila uko hoi, unataka kusali ghafla usingizi mzito huo.
*Kumb.25:8*(Soma)

Wana wa Israel walipigwa na Amaleki walipochoka na kuzimia..
Ukiona dalili hii unashambuliwa.
Udhaifu ktk maombi.
Ulikuwa unaomba dk 10,unashuka dk 5 mwisho unaacha kabisa.
Ulikuwa unafunga, unashindwa. Yaani madhabahu yako ya maombi inavunjwa.
*Mathayo 26:40-41*(soma)
Unaanza kukosa tumaini la mafanikio, miujiza. Yaani unakata tamaa.
Ukipoteza tumaini, umepoteza msaada.
*Zaburi 125:1*(soma)
Chochote unachopitia mpendwa usikate tamaa, matatizo, dhiki sio vita ya milele, lipo tumaini, ipo asubuhi yako inakuja.
Haijalishi umejikwaa mara ngapi, haijalishi umeanguka mara ngapi!
Biblia inasema *mwenye haki huanguka mara saba akasimama*
Unajitenga na wapendwa wenzio, unakuwa mtu wa kujitenga na watu wa Mungu.
Adui anakupa mapito na anakufunga mdomo ili akumalize, usipate msaada.

*Jinsi ya kujinasua*
Jenga /tengeneza mahusiano yako na Mungu. Zab92:12
Usiache mahala pako pa maombi. Zidisha maombi, ongeza idadi ya siku za kufunga, pambana umuaibishe shetani.
Usiliache kanisa.. Kanisa ndo mji wako wa makimbilio. Yoshua 20:1-2
Usijitenganishe na mchungaji wako.. Baba yako wa kiroho. Waebraniah 13:17
NB: *Tumia muda mwingi kukaa na Neno na kuomba ili uweze kusimama*
Mathayo 26:41
Muwe na siku njema!!!e

No comments:

Post a Comment