Kila mmoja anafikiria juu ya kuubadili ulimwengu, lakini hakuna anayefikiria kujibadili yeye mwenyewe. Jimmy J
Wakati kitu fulani kinapofufuliwa, mambo ya zamani yanaletwa tena kuwa hai, mawazo mapya yanaletwa yanaletwa kuwa kitu. Wakati jamii inaposhuhudia maslahi mapya ya kidini, huo huitwa ufufuo. Kamusi ya MerrianWebster Collegiate inaelezea ufufuo kama “mkutano wa hisia za juu sana wa kiinjilisti au msururu wa mikutano.” Katika maisha yangu ya utu uzima kama Mkristo, nimewasikia watu wakiongea kuuhusu na kuombea ufufuo. Lakini sina hakika kwamba ufufuo ndio tunaohitaji.
Nafikiri twahitaji kitu kikubwa zaidi. Nafikiri twahitaji Mageuzi. Kamusi ya Webster inaelezea neno hili mageuzi kuwa “mabadiliko ya ghafla, makubwa, au makamilifu.” Kwa kawaida hatuna shida kushughulikia mambo ya zamani kuliko mabadiliko makubwa. Lakini je, ufufuo uliopita umelibadili kanisa na ulimwengu? Umekuwa na manufaa wakati huo; lakini ni nini tunachohitaji sasa katika kanisa ili tuweze kuwa na utendaji ufaao katika ulimwengu? Itatuchukua nini ili tuwe nuru ambayo Kristo alitaka tuwe? Katika kitabu chake The Barbarian Way, Erwin McManus anaandika, “Wacha Ukristo wa usafi utuondokee na turejelee imani ya kale yenye nguvu inayochagua mageuzi badala ya kushawishika, hatari badala ya usalama, na huruma badala ya kuwa vuguvugu na dini zilizo majimaji.”
Huruma ya Kristo ilimfanya asulubishwe msalabani. Je, yetu itatufanya tujitolee baadhi ya njia zetu za zamani ili kizazi kijacho kishuhudie nguvu ya mabadiliko ya Mageuzi ya Upendo? Yesu alikuwa mpenda mageuzi, na alikuwa hatetei utamaduni. Alikuja ili kuleta mabadiliko, na yakawakasirisha watu wa kidini wa siku hiyo. Mungu habadiliki, lakini Huwabadilisha wengine. Nimepata kwamba Anapenda ubunifu na mambo mapya na huweka mambo kuwa mapya na yakiwaka moto.
Baadhi ya makanisa hayatafikiria kubadilisha kitu kama vile mtindo wa muziki wao. Wataimba nyimbo za kitabu cha nyimbo na kucheza kinanda pekee ikiwa wataendelea kuwepo. Wanapuuza ukweli kwamba waumini wao huendelea kupungua kiwango chao na hawawaathiri jamii yao hata kidogo. Wanahitaji kuchunguza Jumapili asubuhi na wajiulize ni kwanini kila mtu katika jengo hilo ni wa makamu au mtu mzima. Vijana wako wapi? Iwapi furaha? Uwapi uhai? Miaka kadhaa iliyopita, Nilianza kushuhudia kupungua kwa mikutano katika kanisa letu na nikagundua kwamba wengi wa waliokuwa wakihudhuria walikuwa watu wa makamu, ndugu wakaribu(wafanyakazi)wa washirika/au watu wazima.
Niliongea na rafiki yangu wa kiume, aliyekuwa na umri wa miaka ishirini na minne wakati huo alianza kunihimiza tufanye mabadiliko makubwa katika mtindo wa muziki, taa, mapambo na aina ya nguo wanazovaa wahubiri. Alisema kwamba kizazi chake kinahitaji kufikiwa na injili ya Yesu Kristo, lakini kinasinywa na mtindo wa zamani wa dini wenye sifa ya kuzingatia sheria na unaochosha. Kwa karibu mwaka mzima, mimi na mchungaji mmoja tulipinga sana jambo hilo.
Ulisema kile ambacho watu wengi husema wanapokuwa hawataki mabadiliko: “Mungu habadiliki.” "Sisi pia tulionelea kile tulichofanya kufikia hapo kimeendelea vyema. Kwanini ukibadilishe? Majivuno mengi yalihusika, na ilikuwa vigumu kumfanya kijana Jimmy J mwenye umri wa miaka ishirini ambaye alikuwa ameanza tu kufanya kazi nasi kutuambia kile tunachopaswa kufanya.... Lakini mwaka ulipoendelea tulianza kuwasikiliza vijana wengine, na tukatambua kwamba hatukuhitaji mbinu za kuabudu. Ujumbe wetu haungebadilika, lakini njia unayotokea ujumbe huo ilihitaji kubadilika" -Kasisi Barnet
Ulimwengu unabadilika, watu wanabadilika, kizazi kipya kinafikiria tofauti kuliko wale wa zamani, na twahitaji kufikiria jinsi ya kuwafikia. Tunataka kuona vijana kwenye mikutano, lakini hatuwi tayari kuwapa chochote kinachowafurahisha. Hatuwi tayari kukutana nao mahali waliko. Lakini kidogo kidogo mioyo yetu ikifunguka ili kujaribu mambo mapya, na tunaweza kuona matokeo makuu. Hatutawaapoteza tena watu na badala yake watu wapya watakuja, na wengi wao watakuwa vijana wenye furaha. Ikiwa tuna hekima ya kizazi cha watu wazima na furaha ya ubunifu ya vijana, basi tuko na wote walio bora ulimwenguni.
Kasisi Barnet alinisimulia kisa hiki"siku moja Dan alitaka kutumia rangi fulani katika jarida letu la kila mwezi ambazo tulikuwa hatujawahi kuzitumia. Mimi sikuzipenda kwa hiyo nikasema hapana. Alikuwa mkakamavu kuhusu kutumia rangi mpya, na nikasisitiza nikasema, “Mimi sizipendi, na hatutazitumia!” akasema, “Sikutambua kwamba uliitwa ili kujihubiria. Je, ikiwa watu wengine wanazipenda rangi hizo?” Kufikia hapo nilipata funzo la kunifungua macho. Nilitambua kwamba nina sheria za mavazi za ofisi ambazo nilipenda na tulitumia rangi katika jarida, kwa matangazo, na katika jengo ambazo nilizipenda. Tulikuwa na muziki ambao niliupenda. Niliaibika wakati nilipotambua jinsi mawazo yangu mengi ni kuhusu yote ninayoyapenda na ilikuwa ni faraja kwangu, sio watu wengine wanavyohitaji. Mimi na viongozi tulianza kutambua tunaabudu mbinu na kwamba mbinu hizo hazikumaanisha chochote kwa Mungu.
Ulikuwa na ujumbe Wake aliotaka kuutoa, na njia uliotokea ingebadilishwa. Kwa hiyo tulianza kubadilika na tumeendelea kuwa wazi kubadilika tangu wakati huo. Tumebadilisha mitindo yetu ya mavazi kwa kuzingatia mitindo ya kisasa zaidi. Tulibadilisha bendi zetu za kuabudu na zile ambazo zitawavutia vijana wengi zaidi. Niliamua kukipenda kizazi cha sasa ili waimbe nyimbo wanazofurahia. Tulipunguza muda wa ibada zetu kwa sababu jamii yetu yote leo inataka mambo yafanywe haraka. Nilikuwa nimezoea ibada za kanisa za muda wa saa tatu, lakini sio kila mmoja alipenda hivyo, kwa hiyo tukaamua kukutana na watu kati kati. Tulibadili taa zetu kuwa za kuvutia zaidi. Hata tulipata mashine ya kutoa moshi wa ukungu wanayoniambia inavutia sana watu. Mimi bado nafikiria inawazuia watu kuona vizuri, lakini naweza kupata ukungu ikiwa unawafanya watu kuwa na uhusiano wa kutisha na mimi na kusikiliza ujumbe wa injili. Kumbuka Paulo alisema alikuwa hali zote kwa watu wote; ili kwa njia zote apate kuwaokoa watu kwa kuwahubiria injili ya Yesu Kristo (angalia 1 KOR 9:2022). Hakuabudu mbinu na hata sisi pia."-Kasisi Barnet
Biblia inasema kwamba katika siku za mwisho tutashuhudia kanisa lenye uchoyo na ubinafsi. Watu watapoteza maadili na watashikilia aina ya dini lakini watanyimwa nguvu ya injili (angalia 2 TIM 3:1-5). Twahitaji kuona nguvu ya Mungu katika makanisa yetu. Twahitaji kuona mabadiliko ya maisha, uponyaji, kudumishwa na kukombolewa.
Twahitaji kuona upendo wa Mungu ukitiririka kwa njia huru. Twahitaji kuona Mageuzi, na nimejitolea kuwa sehemu yake! Ninaweza kusema kuwa mabadiliko mengi tunayoweza kufanya kwenye mikutano yetu si yale ambayo tunayaweza kuyapenda. Lakini ninajifunza zaidi kila siku kwamba upendo unahitaji tuwache njia zetu na tutafute njia za Mungu kwa msimu wa sasa.
Mabadiliko yetu mengi yamekuwa kujitolea kwangu mimi binafsi, lakini najua katika moyo wangu kwamba yamekuwa jambo la sawa kufanya. Kulikuwa na wakati ambapo nilifikiri kwamba Mungu hangeweza kumbariki mtu ikiwa yuko jukwaani akijaribu kuwaongoza watu ilhali amevalia nguo aina ya jeans. Kisha nikafikiria kuhusu kile ambacho Musa pengine alikuwa amevalia wakati alipokwenda juu mlimani kupokea Amri Kumi na hatimaye nikatambua jinsi nilivyokuwa mjinga.
Yohana Mbatizaji alikuwa akivalia mavazi ya aina ya kipekee, alikuwa tabia za kipekee za ulaji, na makazi yake yalikuwa jangwani, lakini aliongoza mageuzi. Alitayarisha njia ya Masihi. Hakuwa shabiki wa dini yenye mpangilio na aliwaita viongozi wakuu wa kidini wa nyakati zake kuwa kundi la nyoka wenye sumu kali. Alichukizwa mno na watu wa kidini waliojichukulia kuwa wenye haki wa siku hizo ambao walikwenda hekaluni kuomba lakini hawangeweza kuinua kidole kumsaidia mtu yeyote anayehitaji msaada. Mungu anaangalia moyo, na twahitaji kujifunza kufanya hivyo pia. Hakujali jinsi Musa au Yohana waliovyoonekana. Alifurahi kupata mtu asiyeogopa kuongoza maasi dhidi ya dini iliyokufa na kuwaongoza watu kuwa na uhusiano na Mungu.
Imeandikwa na Jimmy J.
Mwana Mageuzi ya Upendo.
Email: mawaidhapopote@gmail.com
No comments:
Post a Comment