Usifike mwishoni mwa maisha yako ukiwa umejawa na majuto ya hasara ya maisha yako kwa sababu uliyatumia kwa. vitu visivyo na maaana kamwe.......
Wakati ni karama ya ajabu kutoka kwa Mungu, na ni muhimu tuwe waangalifu sana tunatumia wakati wetu kufanya nini. Wajua, mradi tu tumeshautumia mda, hatuwezi kuupata tena. Kuwa na wakati na Mungu huleta thawabu ya ajabu, lakini vitu vingine vingi huleta sisimko lisilo na thamani kwa bei ghali.
Ninapendekeza ufanye uamuzi wa kutumia mwaka ulio mbele yako ukitilia mkazo jambo la upendo wa Mungu, ukisoma maandiko yanayozungumzia upendo, ili ujifunze jinsi ya kupokea upendo wake. Upendo wake huleta uzima, amani, na furaha na msisimko wa kuishi. Na anataka tutulie na kufurahia kuwa mtoto wake. Soma maandiko kuhusu asili yake na upate kumfahamu vyema zaidi. 1 Yohana 4:16 inasema, “ Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi na kuliamini.”
Labda huna nguvu hata kidogo, na unaona jinsi itakavyokuwa rahisi kuwa na manung’uniko mchana kutwa. Habari njema ni kwamba, unaweza kubadilisha nia yako kwa kuzungumza maneno ya kutia moyo na imani. Tamka kwa sauti, “Mungu ananipenda sana. Mimi ni mboni ya jicho lake, na ana mpango mwema kwa ajili yangu.” Ukizungumza juu ya Mungu na Neno lake badala ya shida zako na hisia zako, unaweza kuleta tofauti kwa siku yako yote.
Lazima ujizungumzie na umakinike kwamba umezungukwa na upendo wa Mungu. Biblia inasema kwamba Mungu amechora picha yako katika vitanga vya mikono yake (tazama Isaya 49:16). Ninaweza kumwona kule juu akisema, “ Tazama, unaona hapa? Ah, jamani, si wanapendeza? Ninawapenda sana. Ona watoto wangu, papa hapa kwenye vitanga vya mikono yangu.”Amekuweka hapo kama kumbukumbu daima kwamba anakupenda na anatamani ushirika na wewe.

Kumbuka kuwa mtu wa shukrani daima kwake Mungu na kukuza uhusiano wa ushirika endelevu naye. Nyakati zingine huenda utaamua kuacha shughuli zako zote na kuchukua mda mfupi na kumshukuru Mungu kwamba unamjua na kumwambia jinsi alivyo wa ajabu. Tulia na umpende Mungu. 1 Yohana 4:16-17 inasema, “Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu
#MunguAnakupenda
#Jimmy J
#MunguAnakupenda
#Jimmy J
No comments:
Post a Comment