Monday, 17 December 2018

Mungu Anakupenda

Usifike mwishoni mwa maisha yako ukiwa umejawa na majuto ya hasara ya maisha yako kwa sababu uliyatumia  kwa. vitu visivyo  na  maaana  kamwe.......

Wakati  ni  karama  ya  ajabu  kutoka  kwa Mungu, na ni muhimu  tuwe waangalifu  sana tunatumia  wakati  wetu kufanya nini.  Wajua, mradi tu tumeshautumia  mda, hatuwezi kuupata tena.  Kuwa na wakati  na Mungu huleta  thawabu  ya ajabu,  lakini  vitu vingine vingi huleta sisimko lisilo na thamani kwa bei ghali.


Ninapendekeza  ufanye uamuzi  wa kutumia  mwaka ulio mbele yako ukitilia  mkazo jambo la upendo wa Mungu, ukisoma maandiko yanayozungumzia  upendo, ili ujifunze jinsi ya kupokea upendo wake. Upendo wake huleta  uzima,  amani, na furaha na msisimko wa kuishi. Na anataka  tutulie  na  kufurahia  kuwa  mtoto  wake.  Soma  maandiko kuhusu asili yake na upate kumfahamu vyema zaidi. 1  Yohana 4:16  inasema,  “ Nasi tumelifahamu  pendo alilo  nalo Mungu kwetu sisi na kuliamini.”
Labda huna nguvu hata kidogo, na unaona jinsi itakavyokuwa rahisi kuwa  na  manung’uniko  mchana  kutwa.  Habari  njema  ni  kwamba, unaweza  kubadilisha  nia  yako  kwa  kuzungumza  maneno  ya kutia moyo  na  imani.  Tamka  kwa sauti, “Mungu ananipenda  sana.  Mimi ni mboni ya jicho lake, na ana mpango mwema kwa ajili  yangu.” Ukizungumza  juu ya Mungu na Neno lake  badala  ya shida zako na hisia zako, unaweza kuleta tofauti kwa siku yako yote.
Lazima  ujizungumzie  na umakinike  kwamba  umezungukwa  na upendo wa Mungu. Biblia  inasema kwamba Mungu amechora  picha yako  katika  vitanga  vya  mikono  yake  (tazama  Isaya  49:16).  Ninaweza kumwona kule juu akisema,  “ Tazama,  unaona hapa?  Ah, jamani, si wanapendeza?  Ninawapenda sana. Ona watoto wangu, papa hapa  kwenye  vitanga  vya  mikono  yangu.”Amekuweka  hapo  kama kumbukumbu daima  kwamba anakupenda  na anatamani  ushirika na wewe.

Kumbuka kuwa mtu wa shukrani daima kwake Mungu na kukuza uhusiano wa ushirika endelevu naye. Nyakati zingine huenda utaamua kuacha shughuli zako zote na kuchukua mda mfupi na kumshukuru Mungu kwamba unamjua  na kumwambia  jinsi alivyo wa ajabu.  Tulia na umpende  Mungu. 1  Yohana  4:16-17 inasema,  “Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. Katika hili pendo limekamilishwa  kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu
#MunguAnakupenda
#Jimmy J

No comments:

Post a Comment