“Ni nani atakayenitunzia watoto wangu?” analia mama anayekufa, akijua kwamba watoto wake hivi karibuni watajiunga na mamilioni ya wengine kote duniani kumtafuta mama mpya. Nimewaona marafiki wanaougua saratani wakilia maombi hayo hayo. Siwezi kufikiria juu ya afueni kuu ya moyo, au mauguzi makuu yanayosikika nyakati za giza kuu
Nataka kumpigia yowe nimwambie. “TUTAKUTUNZIA” Hii kwa kweli ni sehemu ambayo twahitaji kujikakamua, kuvumilia, kuomba na KUAMINI, na kutoka kwa imani.
Si lazima uishi katika nchi zinazostawi ili kuwapata mayatima wanaohitaji familia, au watu wenye upweke wanaotafuta urafiki, kila mmoja wetu anaishi kwenye miji ambako watoto wanateseka kwenye mifumo ya serikali inayojaribu iwezavyo kutimiza mahitaji ambayo sisi kama kanisa twaweza kusaidia kuyatimiza.
Ninalipenda kanisa …yeye ni mjuzi wa mambo mengi na kweli ameinuka kupitia kote duniani akiwa na mawazo mapya ya imani na furaha. Lakini kanisa katika mahali pake bora ni wakati anapompenda Mungu akiwa kama alivyo… na kisha Kanisa linasimama na mikono imenyooshwa kuhudumia jamii inayoteseka na ulimwengu uliovunjika, kuwaunganisha watu kwa Yesu na yote yanayomaanisha haya. Sio kuhukumu au kulaumu maskini, bali KUWAPENDA…na kuwapenda kuna gharama, na ni kitendo…sio jina.
Pamoja, twaweza kusimama mahali penye pengo kwa wale wasiokuwa na sauti…kumpenda Bwana Mungu wetu kwa moyo wetu wote, roho, akili na nguvu…NA kuwapenda jirani zetu kama tujipendavyo sisi wenyewe. Kwa kweli inashangaza!
Kwahiyo twaweza kuishughulikia kivipi hali hii kubwa ya kukosa matumaini? Twawezaje kuwafungulia mlango wale waliokwama katika gereza hili hatari? HAKUNA hata mmoja anayeweza kushughulikia jambo hili kibinafsi. Hata watu werevu zaidi duniani wanaopenda kutoa misaada WANAWAHITAJI wengine na ujuzi wa makundi mbali mbali ya wataalam wanaofanyakazi pamoja kwa manufaa bora kwa watu. Lakini twahitaji kuanza mwanzo, twaweza kumdhamini mtoto mmoja, kuwa sauti kwa wale waliovunjika katika jamii zetu, saidia kwa njia moja ikiwa una uwezo katika mfumo wa malezi wa kupanga (mfano, Matunzo ya dharura, matunzo ya muda mfupi au muda mrefu, mifumo ya kuwa na malezi ya mwisho wa wiki) changa pesa za msaada au mahitaji yaliyo kwenye moyo wako, ianzishe miradi hii katika kanisa lako na ufanye huduma hii ianze kuendelea, ishi maisha ya kawaida ya kujali kutoa kwa watu wengine na wala sio kutumia…orodha ni ndefu mno. Lakini la muhimu, tuhakikishe kwamba mioyo yetu na maisha yetu yanatiwa mafuta na kuwa imara kwa fursa yoyote iliyoko kila siku, ama iwe ni ya kimataifa au ya nchi yako… ni kama vile hadithi ya Msamaria mwema, aliyetumia siku yake nzima kwenda kuleta msaada na majibu mahali ambapo wengine walishuhudia na kupita. Msamaria ALIGUSWA na upendo wa huruma…na hakuguswa tu hisia za moyo, bali alijibu kwa vitendo. Na ningependa kusema kwamba ikiwa unapitia msimu ambao unadhani unahitaji kuhudumiwa, kuliko wewe kwenda kutoa huduma, basi jipe moyo.
Jiweke kwenye mazingira ya kuabudu na kutukuza, ijaze nyumba yako na muziki unaosisimua moyo wako, jaza gari lako na kanda na CD za neno la Mungu, ungana na familia, kanisa na jamii unayojua kwamba utaburudishwa na kutiwa moyo…na mruhusu Roho wa Bwana aendelee kukujaza kutoka ndani hadi nje. Iwapo unahitaji uponyaji, au ushindi wa kifedha, au miujiza ya uhusiano…Mungu wetu anaweza. Jiruhusu uangukie kwenye mikono salama ya Mungu wetu na nguvu yetu, kwani hatakuacha wala kukukana, kumuamini Yeye ni furaha kuu na matumaini yako. Lakini ninakuachia jambo hili ukumbuke…
KUMPENDA Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, akili yako yote, roho yako yote na nguvu zako zote NA umpende jirani yako kama ujipendavyo wewe mwenyewe. Umejazwa hazina na thamani kikamilifu. Usisahau!
#JitoeMwangaKwaMaishaYaWengine.
Jimmy J.
No comments:
Post a Comment