"Nimepata rafiki wa kike/kiume (Girlfriend/Boyfriend) nimtazamiaye. Naomba ushauri..."
Nitakushauri:
Wengi niliokwisha waona huwa wanakosea sehemu ndogo sana ambayo inapelekea kuharibu kwengine kote. Huwa wanadanganywa na shetani kupitia WAZO na HISIA za MWILI hata kuharibu msingi wa mahusiano ule uliowekwa na Mungu wa kufaana kwa ajili ya KUSUDI la Mungu kwenye maisha yao.