"Nimepata rafiki wa kike/kiume (Girlfriend/Boyfriend) nimtazamiaye. Naomba ushauri..."
Nitakushauri:
Wengi niliokwisha waona huwa wanakosea sehemu ndogo sana ambayo inapelekea kuharibu kwengine kote. Huwa wanadanganywa na shetani kupitia WAZO na HISIA za MWILI hata kuharibu msingi wa mahusiano ule uliowekwa na Mungu wa kufaana kwa ajili ya KUSUDI la Mungu kwenye maisha yao.
Biblia inasema "Misingi ikiharibika mwenye haki atafanya nini?"
Mtu mmoja akisha pata rafiki wa KIKE au wa KIUME (Girlfriend/Boyfriend) huanza kufikiria hasa WAKATI ULIOPO NA HILO NDO KOSA KUBWA.
Kufikiria wakati uliopo ndio chanzo cha mabaya yote yanayoendelea kwenye urafiki mwingi. Mtu mmoja atafikiria hasa kumpendeza mwenzi wake zaidi na maigizo huanza hapo, kupoteza muda huanzia hapo, matumizi mabaya ya pesa huanzia hapo, uzinzi huanzia hapo nk. Shetani amedanganya watu wengi. Kwa hiyo, mtu mmoja akipata tu rafiki, cha kwanza anafikiria KULIPIZA/KUFIDIA MUDA ALIOKAA PEKE YAKE. Kumbe ndio anaharibu zaidi.
Kitu ambacho ninakushauri ukiwa na rafiki wa Kike au wakiume ambae unamtazamia cha kufanya ni hiki:
Think more about the future than the present. Kwa Kiswahili tunasema, fikiria zaidi kuhusu wakati ujao kuliko wakati wa sasa. Hii itakusaidia kuacha UJINGA na kufanya vitu vya msingi.
Katika nyakati hizo mawazo mabaya yataendelea kuja. Lakini mtii Roho Mtakatifu ndani yako ili akuongozae katika KWELI na NURU kuliko kutii mwili wako au mawazo ya Ibilisi ya kutia muhuri kabla hujaachwa na uongo mwingine.
Nikwambie tu UKWELI, ukiwa na rafiki anayetaka mfanye upuuzi wakati wa sasa, jua kabisa huna future naye bali mtatumiana tu. Mkishachokana, mtaachana.
If you think about the future you will never take off ur dress but preparing the future of the coming Kids, you will have a good use of time and money, you will focus more on GOD than pleasures of the world and flesh. If you think about the future you will use more time in studies and investment than charting 24/7. Neighbour, be wise and refuse to follow the lies of devil. Jesus is coming soon!
No comments:
Post a Comment