Tuesday, 22 May 2018

MAANA YA KUFUNGA


Neno KUFUNGA linatokana na neno la Kiyunani NESTEVO, ambalo nalo linatokana na maneno mawili ya Kiyunani NE na ESTHIO. 

Neno NE maana yake BILA au HAPANA, Kiingereza NO au WITHOUT. 

Neno ESTHIO maana yake KULA CHAKULA AU KINYWAJI. Kwa Kiingereza ni TO EAT SOLID OR LIQUID FOOD. 


Neno “NESTEVO” sasa linaunga maneno hayo mawili ya Kiyunani NE na ESTHIO, na lina maana BILA KULA CHAKULA AU KINYWAJI CHOCHOTE. Hivyo maana ya kufunga, ni BILA KULA CHAKULA AU KINYWAJI CHOCHOTE.

Kufunga sio kuacha kusoma gazeti ulilozoea, kuacha kuchana nywele n.k. Kufunga ni kuacha kabisa kula au kunywa kinywaji chochote. Maana hii ya kufunga, inathibitishwa na maandiko yafuatayo EZRA 10:6; YONA 3:7; 2 SAMWELI 3:35; ESTA 4:16; KUMBUKUMBU LA TORATI 9:9; MATENDO 9:9.

Kufungulia sasa inaweza kuwa ni kinyume ya haya maelezo.

No comments:

Post a Comment