Wednesday, 29 August 2018

Nguvu za Kuendelea Mbele

Nakumbuka  siku  moja  nilipokea  habari  mbaya  sana  muda  mfupi kabla kuaanza kongamano la siku  tatu. Ilikuwa vigumu kuendelea, lakini  nilijua  sina  budi  kuendelea.  Nilihisi  Roho  Mtakatifu  akisema, “Nyanyua  mguu  wako  na  upige  hatua  kwenda  mbele.  Endelea kwenda Mbele!”

Kuendelea  kwenda  mbele  hakukuondoa  uchungu wote  na hali ya kuvunjika  moyo niliyohisi,  lakini  kulinizuia  nisiweze kuzama katika kilindi cha kukata tamaa,  na baada ya majuma machache, hali iliweza kutatuliwa.  Moja ya dalili  za ukomavu  wa kiroho ni kuwa  na nidhamu ya kutimiza ahadi zako, hata ikiwa  unapitia wakati  mgumu.  Nilikuwa  naumia,  lakini  nilihitaji  kuendelea kuwahudumia wengine  waliokuwa wanaumia,  na nilifanya  hivyo, Mungu aliniponya na kusuluhisha tatizo langu.

Thursday, 9 August 2018

Je, Yesu Alikuja kwa ajiri ya Wayahudi Pekee ??

Ndugu   zetu   Waislamu   wanapenda  sana  kudai   kuwa   Yesu   alikuja kwa   ajili   ya  Wayahudi   peke   yao   na   sio   kwa   ajili   ya   ulimwengu  wote.   Na   andiko   wanalolitumia   tena  na  tena  ni   la  Mathayo   15:24  pale  Yesu  alipozungumza   na   mwanamke   Mkananayo:  Akajibu,   akasema,   Sikutumwa   ila   kwa   kondoo   waliopotea   wa  nyumba  ya  Israeli.  

Na   tazama, mwanamke   Mkananayo   wa   mipaka   ile   akatokea,  akampazia   sauti   akisema,   Unirehemu,   Bwana, Mwana  wa  Daudi;  binti   yangu   amepagawa   sana   na   pepo.   Wala   yeye   hakumjibu  neno.   Nao   wanafunzi   wake   wakamwendea,   wakamwomba,  wakisema,   Mwache   aende   zake;   kwa   maana   anapiga   kelele  nyuma   yetu.   Akajibu,   akasema,   Sikutumwa   ila   kwa   kondoo  waliopotea

Sunday, 5 August 2018

Je, Yesu Alikufa...??

Na KWA AJILI YA KUSEMA KWAO MV BUKOBA Ilizama; na kwa hakika MV BUKOBA haikuzama Bali ulizama tu mtumbwi uliofanana na MV BUKOBA na wale wanaosema ilizama wamo katika shaka na jambo hilo la kusema MV BUKOBA alizama mwaka 1996; hawana uhakika isipokuwa wanafuata Dhaka tu. Na wala Meli hii haikuzama Bali mtumbwi unaofanana na MV BUKOBA ndio uliozama. Na kwa yakini MV BUKOBA haikuzama”-Maalim Chaka

Qurani 4:157-158 Suratul An-Nisaa (Wanawake) Na kwa (ajili ya )kusema kwao sisi tumemuua masihi Isa mwana wa Maryamu, mtume wa Mungu. Hali hawakumuua wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa (mtu mwingine wakamdhani nabii Isa.) Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika (hakika)hiyo (ya kumuua nabii Isa) wamo katika shaka nalo (jambo hilo kusema kauwawa]. Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo)hili (la kuwa kweli wamemuua nabii isa) isipokuwa wanafuata dhana tu.Na kwa yakini hawakumuua. Bali mwenyenzi Mungu alimnyanyua kwake. Na mwenyenzi Mungu ni mwenye nguvu (na)mwenye hikima.

Wednesday, 1 August 2018

Amini Kilicho Bora

Nimeokoa  nguvu nyingi  ambayo ingetumiwa na hasira kwa  kusema, “ Ingawa  wanachosema  au kunifanyia huniumiza, nachagua  kuamini  moyo wao  uko sawa.” Naendelea kujiongelesha hadi hisia za  hasira yangu zianze kufifia.  Ninasema mambo kama, Siamini  wanaelewa  jinsi  vitendo  vyao  vinavyoniathiri. Siamini wangejaribu kuniumiza kimakusudi. Hawaelewi jinsi  ninavyojisikia wanaposema hivyo. Pengine  hawahisi vyema kimwili  leo au pengine  wana  tatizo la kibinafsi linalowafanya kutojali jinsi walivyo.”

Ninajua  kutokana  na  ujuzi nilio nao  kwamba  kuweka kumbukumbu za  kimawazo  za  makosa  hutuathiri maisha  yetu na hakumbadilishi mtu mwingine.  Mara  nyingi hupoteza  siku tukiwa tumemkasirikia mtu fulani ambaye hata  hatambui kuwa  alifanya kitu kinachotuudhi.Wanafurahia  siku yao  na  sisi  twaipoteza  yetu. Ikiwa  tutaweka  kumbukumbu hizo,  basi  ni kwanini hatuweki kumbukumbu za  mambo  mazuri  watu  wanayosema  na  kufanya kuliko makosa wanayofanya?

Ikiwa  tunataka  kuwapenda watu, lazima  tumwache  Mungu abadilishe jinsi tunavyofikiri kuhusu watu  na  mambo  wanayofanya. Twaweza  kuamini  mabaya na kushuku  kila kitu watu wengine wafanyacho  na kusema, lakini  upendo  halisi  kila mara unaamini kilicho bora. Kile  tunachofikiria  na kuamini  ni  chaguo. Chanzo cha dhiki yetu nyingi katika maisha ni kuwa hatudhibiti au kunidhamisha mawazo  yetu.  Kwa  kutochagua  kunidhamisha  mawazo  yetu, huwa moja kwa moja twachagua kuamini mabaya ya mtu au kushuku. Nabii Jeremiah aliwauliza watu haya, “Mawazo yako mabaya yatakaa ndani  yako hata lini?  (angalia YER  4:14). Mawazo  waliyochagua kufikiria yalikuwa mabaya kwa Mungu.

Wakati tunapochagua kuamini  kilicho bora,  twaweza  kuacha kila kitu  kiondoke  hasa  kile  ambacho  chaweza kudhuru  uhusiano wetu mzuri.

```Amini Kilicho Bora.```
Mtumishi