Na KWA AJILI YA KUSEMA KWAO MV BUKOBA Ilizama; na kwa hakika MV BUKOBA haikuzama Bali ulizama tu mtumbwi uliofanana na MV BUKOBA na wale wanaosema ilizama wamo katika shaka na jambo hilo la kusema MV BUKOBA alizama mwaka 1996; hawana uhakika isipokuwa wanafuata Dhaka tu. Na wala Meli hii haikuzama Bali mtumbwi unaofanana na MV BUKOBA ndio uliozama. Na kwa yakini MV BUKOBA haikuzama”-Maalim Chaka
Qurani 4:157-158 Suratul An-Nisaa (Wanawake) Na kwa (ajili ya )kusema kwao sisi tumemuua masihi Isa mwana wa Maryamu, mtume wa Mungu. Hali hawakumuua wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa (mtu mwingine wakamdhani nabii Isa.) Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika (hakika)hiyo (ya kumuua nabii Isa) wamo katika shaka nalo (jambo hilo kusema kauwawa]. Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo)hili (la kuwa kweli wamemuua nabii isa) isipokuwa wanafuata dhana tu.Na kwa yakini hawakumuua. Bali mwenyenzi Mungu alimnyanyua kwake. Na mwenyenzi Mungu ni mwenye nguvu (na)mwenye hikima.
Je hadithi hizo mbili hazifanani??Ni wazi kuwa Quran inasema kwamba Isa/Yesu hakufa. Hapo nyuma{Kwa page hii} tumeona kuwa, Quran inasema Isa ni Neno la Allah, ni Roho ya Allah. Kisha, tukafikia kujiuliza endapo roho ya mtu ni tofauti na mtu mwenyewe. Kimantiki (logically), ni sahihi kabisa kusema:
• Kama ndugu yangu anaitwa Kapama,
• Na Kapama ni Mwalimu, • Kwa hiyo, ndugu yangu ni
Mwalimu. Hata kwenye somo la Hisabati tunafundishwa kwamba:
• kama a = b; • na b = c, • basi a = c.
Itakuwa ni jambo la ajabu na haileti maana endapo nitang’ang’ania kusema:
• Ndugu yangu anaitwa Kapama;
• Kapama ni Mwalimu, • Kwa hiyo ndugu yangu si
Mwalimu.
• Ndugu yangu anaitwa Kapama;
• Kapama ni Mwalimu, • Kwa hiyo ndugu yangu si
Mwalimu.
Haiwezekani! Kwa hiyo: Kama Mungu ni Roho; na Yesu ni Roho, basi Yesu ni Mungu. Sasa, kama Isa ni Neno la Allah; Isa ni Roho ya Allah kama tulivyoona; Je, anaweza kusema uongo? Je, anaweza kusema vitu asivyovijua?
Quran inatuambia kuwa, Isa alisema: So peace be on me on the day I was born; and on the day I die; and peace be on me on the day when I shall be raised to life.
Yaani:
Kwa hiyo, amani iwe juu yangu katika siku niliyozaliwa; na katika siku nitakayokufa; na amani iwe juu yangu katika siku ambayo nitafufuliwa. (Mariam 19:33). Ni kweli aya hii bado haisemi moja kwa moja kuwa Isa alikufa au alifufuka. Lakini, swali ni kuwa, Kwa nini aongelee habari ya kufa kwake? Kwa nini habari ya kufufuliwa kwake?
Kwa hiyo, amani iwe juu yangu katika siku niliyozaliwa; na katika siku nitakayokufa; na amani iwe juu yangu katika siku ambayo nitafufuliwa. (Mariam 19:33). Ni kweli aya hii bado haisemi moja kwa moja kuwa Isa alikufa au alifufuka. Lakini, swali ni kuwa, Kwa nini aongelee habari ya kufa kwake? Kwa nini habari ya kufufuliwa kwake?
Ni lazima tufahamu kuwa, kwa kadiri ya Quran, hapa alikuwa anaongea wakati angali kichanga kabisa, ndio kwanza amezaliwa. Hivyo, alikuwa anaongelea siku zake za mbeleni. Sasa, ni siku zipi hizo? Je, hakumaanisha kuwa ni wakati ambao angekuwa mtu mzima? Hayo ni maswali ambayo bila shaka mtu angependa kujiuliza. Na Biblia (Torati na Injili), ambayo Quran katika Al-Imran 3:2-3 inasema kuwa ni kitabu cha kuwaongoza wanadamu wote; Biblia hiyo inasema kuwa Yesu alikufa na alifufuka.
Njoo Kwa Yesu
No comments:
Post a Comment