Muhubiri 5:3 kwa maana ndoto huja kwasababu ya shughuli nyingi....kwasababu baadhi yetu tunandoto na hatutaki kufanya kazi na wakati mwingine hatuna budi kupitia hali ngumu.
Naamini unapokuwa na ndoto ni kama unapokuwa na ujauzito,kuna wanawake wachache ambao huweza kujifungua bila uchungu lakini si wengi sana.Nafikiri kwamba ukitaka kuzalisha kitu lazima ufahamu kwamba ni zaidi ya kuwa na wazo nzuri,Unakuwa na ndoto,unakuwa na matumaini,unakuwa na mpango lakini lazima uwe tayari kufanya kazi na kupitia yale ambayo unapaswa kupitia ili ndoto yako iweze timia.
Nataka kuongea nawewe ikiwa una moyo wa mtimizaji.
Katika Yohana 17:4 Yesu anasema "Mimi nimekutukuza duniani nami nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye." Na sijui niwaelezeje jambo hili ni moja ya yale yasio yakawaida yamkini miaka 10 iliyopita nilisoma maandiko hayo nikaketi katika kiti changu mahali ambapo nilikuwa naomba na kulia na kulia na nilijua wakati huo ni muhimu kutimiza kazi ambayo Mungu alikuwa amenipa niifanye.
Unajua hakika siyo ngumu sana kuanza,hapo mwanzoni kila mtu huwa amesisimka,ni kitu kipya kwahivyo kuna kuwa na kiwango fulani cha msisimko na hisia kinachoambatana nacho lakini hayo yote yataisha,itafika wakati watu hawatapiga makofi wala kushangilia ,unajipata pekee yako unaweza jiuliza kama utaweza timiza ndoto yako na hapo ndio inabidi ufanye uamuzi kama utaendelea na Mungu hadi mwisho.
Hiyo inaweza kuwa rahisi kama vile kuamua kutoka kwa madeni au kuamua kurudi kwa afya bora,watu wengi wanaafya mbaya lakini unajua nini hustahili kusalia katika afya mbaya,unaweza kufanya mambo fulani ili kurejesha afya yako...inaweza chukua muda mrefu lakini unaweza.
"basi ningependa mchungaji aniombee"sawa hivyo ni vizuri, wataomba unavyotaka waombe lakini ndoto hutimia kwa maombi,kazi nyingi na juhudi za kutia uchungu..watu wengi wanatamani sana lakini tunachohitaji kwa hakika ni kutenda,hatuhitaji kuketi na kusema "laiti laiti...."tunahitaji kuwa na anzima....
Hakika ni ajabu hakuna mtu asiyekuwa na furaha kama mtu anayeketi na kutumai kitu kinzuri kitamtendekea lakini hafanyi juhudi zozote kuhakikisha kuwa kinatendeka..Unajua juzi nilisikia kitu kinzuri sana"ukitenda zaidi unapata uwezo wa kutenda ata zaidi na ukitenda machache uwezo wako wa kutenda unapungua zaidi.
Kuwa na ndoto katika maisha yako,iwe unataka kutoka kwa madeni,kuwa na ndoa nzuri.
Utafanya nini kesho? "sijui,pengine nisubiri kitu kitachotendeka" sawa lakini naweza kukwambia kwamba hakitakuwa kitu cha kujivunia,Ni sharti uwe na mpango,ni lazima uanze kutunga ujauzito...
Mwanamke hawezi tunga ujauzito ikiwa hawezi kutunga mimba.Na neno hilo "kutunga"linamaanisha kuamini,Kwahiyo kiasilia mke hutunga mbegu ya mumewe na kushika ujauzito.Kiroho unatunga mbegu za ndoto na matumaini na imani ambayo Mungu ameweka ndani yako kisha unashika mimba lakini huo sio mwisho.
Wangapi watavumilia kubeba ujauzito hadi mwisho,ni wangapi watavumilia maumivu hatimae kujifungua,utagundua hawasemi ila wanasena kujifungua tuu....hawasemi kama hiki ni chumba cha kujifungua,Ni chumba cha maumivu na kujifungua.
Unamaono gani kuhusiana na Maisha yako ya baadae?
Katika kitabu cha Mwanzo 13 tunaona hali ambapo Mungu alimbariki ambrahamu na mpwa wake Lutu kwa kiwango kikubwa,walikuwa na mifugo wengi na wafanyakazi wengi kiasi kwamba wafanyakazi hao walikuwa wanagombana wenyewe kwa wenyewe,kila mmoja alitaka mifugo yake ipate lishe,unajua watu wanaweza pigania kitu chochote.Kwahivyo Abrahamu alikuwa mtu wa Mungu mwenye busara,akamwendea Lutu na kumwambia "Tafadhali kusiwe na ugomvi kati yetu..."Hii ilimvutia Mungu,wapatanishi humvutia Mungu,daima tunataka kuwa na amani na watu wote lakini tuko tayari kuwa wapatanishi?
Abrahamu akamwendea Lutu ambae hangekuwa na chochote kama Abraham asingembariki,na Unajua ingekuwa raisi sana kusema "sasa unafikiri wewe ni nani?,hungekuwa na chochote kwasababu isingekuwa kwaajili yangu,ikiwa kuna tatizo hapa Mimi ndio nitapata lishe kwa mifugo lakini badala yake Abrahamu akamwambia "Tafadhali kusiwe na ugomvi kati yetu.."
Ikiwa huko katika Ndoa na uzozane na mkeo,je utakuwa tayari kuanza kuleta mapatanisho? Pengine utasema "Loooh makosa sio yangu.."katika Biblia hakuna mstari unaosema unapaswa kuomba msamaha kama ni makosa ni yako au ikiwa makosa si yako...Je utakuwa tayari kufanya mapatanisho hata kama ukiwa huna hatia?Mungu atakueshimu kama utafanya hivyo,Mungu atakuheshimu kama utafanya kile kitachofanya kudumisha Amani.
"Naomba kusiwe na Ugomvi kati yangu nawe,Chagua sehemu ya bonde la Yordani unayotaka nami nitachagua sehemu inayobakia"Tazama unyenyekevu ulioje.Basi bila shaka Ruthu alichagua sehemu iliyo bora zaidi na kilichosaria kwa Abraham hakikuwa kizuri sana.Abraham angekuwa na siku mbaya sana,angehisi kana kwamba "Looh sasa naanza Upya,unajua nini Nafikiri kuanza Upya wakati mwingine ni kuzuri,Ninataka watu fulani wajue kwamba bado hawajachelewa.Wewe si mzee sana wala si mtoto sana,hujapatwa na matatizo mengi kupita kiasi,hujakumbwa na chochote cha kukuelemea,hujachelewa kuanza Upya.
Unaweza kuwa na ndoto kama utafanya kitu cha ajabu,unaweza kuwa na ndoto kutoka kwa madeni,Unaweza kuwa na ndoto za kuwa na Amani nyumbani kwako,Unaweza kuwa na ndoto yakuona watato wako wakibadilika.Lakini ikiwa hutaamini chochote hutapata chochote kamwe.Ni heri ni amini kupokea mengi na nipate nusu yake kuliko kutoamini chochote na kukosa chochote.
Kwahivyo katika kitabu cha Mwanzo 13:14
Bwana akamwambia Abrahamu ,alipokwisha kutengana na Lutu...inua sasa macho yako,ukatazame kutoka hapo ulipo upande wa kaskazini ,na wa kusini na mashariki na magharibi:maana nchi hii yote uionayo,nitakupa wewe na uzao wako hata milele.
Kwahiyo Mungu alisema,"haya basi Inuka juu ya mlima huu,toka katika shimo hili la fadhaa,wacha kukata tamaa,inuka uende mahali ambapo unaweza kuona vizuri。kaskazini,kusini,mashariki na magharibi,chochote utachoona nitakupatia..
Unaona nini Leo?mwenzangu naona unahitaji hii.....
Kisha mstari wa 17 unasema
Ondoka,ukatembee katika nchi hii katika mapana yake,na marefu yake,maana nitakupa wewe nchi hiyo.Mwanzo 13:17
Kwahivyo alimwambia mambo mawili Nenda utazame kisha tekeleza..
Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa nasikiliza kanda,nilikuwa nimeguswa na Mungu kwa njia kuu week chache zilizotangulia na kujazwa Roho mtakatifu kwa njia kubwa sana,na Mungu anapogusa maisha yako kwa njia hiyo,hataki tu uwe na hisia fulani,anakutayarisha Ufanye kitu.Umetiwa mafuta ufanye jambo fulani,ikiwa hatungeitajika kufanya kitu basi hatungeitaji kutiwa mafuta na hatujatiwa mafuta ili kukata tamaa,hatujatiwa mafuta kuwa wazembe,tumetiwa mafuta ili kuona kitu kwa macho ya kiroho na tukitekeleze maishani mwetu..Siku hiyo niliposikia kanda hiyo ya mafundisho kutoka marko 4 yaliitwa Vuka uende n'gambo nyingine na nilikuwa kanisani kwa miaka mingi na sikuwa nimewah kumsikia mtu akihubiri kwa lisaa linzima,tulikuwa na mahubiri ya dakika 15 paka 20 na nisingeamini mtu ahubiri mstari mmoja kwa lisaa limoja nikafurahia,kwanini nilipenda sana?Ilikuwa imetiwa mafuta,unajua kutiwa mafuta huko kunaridhika vipi?unaweza kuketi na kusikiliza mchana kutwa,kwasababu si mwanadamu atakaye kuzungumzia bali ni Mungu anayemtumia Mtu huyo kukunenea.na aifiki tu akilini mwako bali moyoni mwako ambapo wewe mwenyewe unaweza kushuhudia ni Neno la Mungu...Siku hiyo baada ya kusikia mafundisho hayo kitu kilinijia kama upepo mkali unaovuma,si kitu nilichohisi kwa mwili lakini ni kitu kilichozaliwa ndani yangu..
Mungu anataka Uwe na ndoto juu ya maisha yako,mnahitaji kujihamasisha,umekuwa na matatizo fulani,umekuwa na Uchungu fulani,umekuwa na masikitisho na umeyaruhusu yakufunge na kanakwamba unataka kukata tamaa...na nafikiri Mungu amenituma ili nikutie moyo kwa kusema vile Paulo alivyomwambia Timotheo...
"Ichochee karama ya Mungu"2Timotheo 1:6
Usiache moto wako uzimike,kumbuka unabii,kumbuka imani ya nyanya yako na ya mama yako,kumbuka yale Mungu amenena kwaajili yako,kumbuka ahadi ya Mungu,Usiangalie tu watu wengine na Upendezwe wanachofanya,Fanya kitu.Mungu ni yuleyule kwa kila mtu.
Kuwa na Ndoto kisha itekeleze.
Na napenda kitabu cha mwanzo 15 unajua kuna kitu ambacho tunaweza tizama hapa mstari wa kwanza unasema...
"Baada ya mambo hayo neno la Bwana likamjia Abrahamu katika njozi,ikanena,Usiogope ,Abrahamu Mimi ni ngao yako,na thawabu yako kubwa sana."
Basi hapo Mungu alikuwa akimpa Abrahamu neno kuu juu ya maisha yake.Naye Abrahamu alimjibu kwa kumuuliza
Mwanzo 15:2
...eeeh Bwana Mungu,utanipa nini,nami naenda zangu hali sina mtoto,na atakayeimiliki nyumba yangu nu huyu Eliezeri,Mdameski?...
Unaweza nifanyia nini Mungu ?sina mtoto wa kurithi kile nilichonacho,Huyu mfanyakazi wangu ndio atakayerithi nyumba yangu?
Mstari wa 3
Abrahamu akasema,Tazama,hukunipa Uzao,na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu nduye mrithi wangu.
Hakusema mara moja tu,alisema mara mbili,hakuwa na uhakika kwamba Mungu ndiyo ananena naye.
Mungu ananena nawe Leo,Wewe,Wewe...Sawa Unajua kuna watu kuna mtazamo ambao wanashikiria,unaweza kusoma na kufurahia mafundisho haya..sasa unajua Nini,Mungu anaweza kutekeleza kitu cha ajabu kupitia kwako,huenda kisiwe kitu sawa na chetu lakini kinaweza kuwa cha ajabu...Lazima uwe na uwezo wa kutunga mimba,nataka watu wengi washike ujauzito,wanaume watashika ujauzito,Unahitaji mtu wa kukutoa katika maisha yako ya kukuchosha.
Napenda neno hili
Mwanzo 15:4
Nalo neno la Bwana likamjia likinena,huyu hatakurithi,bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakurithi.sasa kulikuwa na tatizo kubwa kwasababu Sara alikuwa amepita uwezo wa kuzaa hii inamaainisha Sara alikuwa teali amepitia mabadiriko kimaisha na Abrahamu hakuwa na uwezo wa kufanya kazi aliyohitajika kufanya.Sara alikuwa na miak 90 na mwingine 100 na... na hapo Mungu anasema "eeeeh wewe nitakubariki na kukuzidisha na utakuwa hivi na vile...."Naye anasema "sina hata mtoto,na Mungu akamwambia mstari wa 5
"Akamleta nje,akasema,tazama sasa mbinguni ,kazihesabu nyota,kama ukiweza kuzihesabu .Akamwambia,ndivyo utavyokuwa uzao wako."
Na Abrahamu akamwamini Mungu,Kuna kitu ambacho sitaki tukose,Je ni kwanini Mungu alimtoa Nje ya hema yake? Kwasababu muda mwingine unapolizingatia tatizo sana ukiwa hema lilelile,kuta zilezile,bili zilezile,Na kusema sina pesa na mgongo unauma,watoto wenye kelele,neti chafu,vyombo vichafu,jokofu limeharibika tena,nazeeka,mara kiatu kimelegea.Unamtazama mtu mliyeoana nywele zake haziko tena,unakitambi ndyo sio?
Mungu anasema toka nje huko uliko na upate maono,toka nje na utazame niliyoyafanya,tazama niliyoyaumba..Na wengineo mnahitaji kutoka Nje ya hema zenu mnapoona mnazama,Nenda matembezini,nenda kidumbwi cha maji,nenda utazame milima,ikiwa amna mlima,nenda utazame kilima kidogo.🤓
Fanya kitu,nenda ukutane na mtu atayekutia Moyo,nenda kanisani,nenda ukasikilize mziki mzuri lakini usiketi tuu na kuamini kamwe hakuna kizuri kitachokutendekea,Kizuri kitakosa kukutendekea kama usipoamini ndani ya roho yako.Ikiwa Mungu anaweza kumtendea mwingine anaweza kukutendea nawewe pia...
Yoeli 2:28
Wazee wenu wataota ndoto na Vijana wataona maono
Matendo ya mitume 2:18
Nitamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu。wake na waume wataotumiwa na Mungu kwa njia kubwa.
Natumai Yesu ataponichukua atakuta nimefanya hivyo.unajua nini kipawa changu ni mdomo wangu kwahiyo hata kama nisipoweza kusimama nitaweza kuzungumza.
Kuwa na ndoto juu ya maisha yako.
Mtumishi jimmy J
No comments:
Post a Comment