Wednesday, 1 August 2018

Amini Kilicho Bora

Nimeokoa  nguvu nyingi  ambayo ingetumiwa na hasira kwa  kusema, “ Ingawa  wanachosema  au kunifanyia huniumiza, nachagua  kuamini  moyo wao  uko sawa.” Naendelea kujiongelesha hadi hisia za  hasira yangu zianze kufifia.  Ninasema mambo kama, Siamini  wanaelewa  jinsi  vitendo  vyao  vinavyoniathiri. Siamini wangejaribu kuniumiza kimakusudi. Hawaelewi jinsi  ninavyojisikia wanaposema hivyo. Pengine  hawahisi vyema kimwili  leo au pengine  wana  tatizo la kibinafsi linalowafanya kutojali jinsi walivyo.”

Ninajua  kutokana  na  ujuzi nilio nao  kwamba  kuweka kumbukumbu za  kimawazo  za  makosa  hutuathiri maisha  yetu na hakumbadilishi mtu mwingine.  Mara  nyingi hupoteza  siku tukiwa tumemkasirikia mtu fulani ambaye hata  hatambui kuwa  alifanya kitu kinachotuudhi.Wanafurahia  siku yao  na  sisi  twaipoteza  yetu. Ikiwa  tutaweka  kumbukumbu hizo,  basi  ni kwanini hatuweki kumbukumbu za  mambo  mazuri  watu  wanayosema  na  kufanya kuliko makosa wanayofanya?

Ikiwa  tunataka  kuwapenda watu, lazima  tumwache  Mungu abadilishe jinsi tunavyofikiri kuhusu watu  na  mambo  wanayofanya. Twaweza  kuamini  mabaya na kushuku  kila kitu watu wengine wafanyacho  na kusema, lakini  upendo  halisi  kila mara unaamini kilicho bora. Kile  tunachofikiria  na kuamini  ni  chaguo. Chanzo cha dhiki yetu nyingi katika maisha ni kuwa hatudhibiti au kunidhamisha mawazo  yetu.  Kwa  kutochagua  kunidhamisha  mawazo  yetu, huwa moja kwa moja twachagua kuamini mabaya ya mtu au kushuku. Nabii Jeremiah aliwauliza watu haya, “Mawazo yako mabaya yatakaa ndani  yako hata lini?  (angalia YER  4:14). Mawazo  waliyochagua kufikiria yalikuwa mabaya kwa Mungu.

Wakati tunapochagua kuamini  kilicho bora,  twaweza  kuacha kila kitu  kiondoke  hasa  kile  ambacho  chaweza kudhuru  uhusiano wetu mzuri.

```Amini Kilicho Bora.```
Mtumishi

No comments:

Post a Comment