Ndugu zetu Waislamu wanapenda sana kudai kuwa Yesu alikuja kwa ajili ya Wayahudi peke yao na sio kwa ajili ya ulimwengu wote. Na andiko wanalolitumia tena na tena ni la Mathayo 15:24 pale Yesu alipozungumza na mwanamke Mkananayo: Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo. Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea
Wa nyumba ya Israeli. Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie. Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. (Mathayo 15:22-‐26) Kwa nini Yesu alisema maneno makali kiasi hiki? Tangu mwanzo Mungu (huyu sasa sio Allah tena; huko tumetoka na tumekuja kwa Yahwe) aliweka wazi kabisa mpango wake wa ukombozi wa mwanadamu utakavyokuwa.
1. Alimwita Ibrahimu atoke kwa nyumba ya baba yake na taifa lake ili akaanzishe uzao mpya na taifa jipya.
Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki. (Mwa 12:1-‐2)
2. Mungu pia akampa Ibrahimu ahadi hii: na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu. (Mwa 22:18). Ibrahimu alizaa wana wengi.
-‐ Kwa Hajiri ni Ishmaeli.
-‐ Kwa Sara ni Isaka.
-‐Kwa Ketura Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Sua.
-‐ Kwa Sara ni Isaka.
-‐Kwa Ketura Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Sua.
Lakini wote waliondolewa nyumbani mwa Ibrahimu, akaachwa Isaka peke yake. Kuhusu Ishmaeli tunasoma: Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akimtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-‐sheba. (Mwanzo 21:14).
Na kuhusu wake wengine, tunasoma: Lakini wana wa masuria aliokuwa nao Ibrahimu, Ibrahimu akawapa zawadi, naye akawaondoa katika mahali alipokaa Isaka mwanawe, wakati wa uhai wake, waende pande za mashariki, mpaka nchi ya Kedemu. Kwa nini alifanya hivyo?
Mungu aliweka wazi mpango wake kwa Ibrahimu, hasa siku ambayo Sara alimwambia amfukuze Hajiri na mwanawe Ishmaeli: Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa. (Mwanzo 21:12)
3. Ndio maana Yesu alipoongea na mwanamke Msamaria pale kisimani, alisema hivi: Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. (Yoh 4:22) Kwa nini anatumia neno ‘watoka’? Ni kwa sababu unaanzia pale kuelekea mahali fulani.
4. Kwa hiyo, wokovu ilibidi uanzie Israeli. Baada ya kutimizwa yale ambayo yalitabiriwa kufanyika Israeli, ndipo kipawa kile kingemwagikia ulimwenguni mwote.
5. Tunajuaje hayo? Ni kwa kurudi tena kwenye ahadi ya Mungu ya tangu mwanzo kwa Ibrahimu: na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia (Mwa 22:18).
Kwa hiyo, kile ambacho Yesu alikuwa anamwambia mwanamke Mkananayo ni kwamba, “Muda wako bado. Subiri chakula kiive hapa Uyahudi ndipo kitapakuliwa na kila mtu atakaribishwa mezani.
Yesu ni Mwokozi wa ulimwengu wote na sio wa Waarabu peke yao au wa Wayahudi peke yao. Sikia maneno yake:
- Marko 28:18-‐19 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu
Yohana 8:12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, mimi ndimi nuru ya ulimwengu Yohana
12:47 Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu.
Yohana 3:17 Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.
Isaya 49:6 naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.
CHANGAMKA KABLA USIKU HAUJAINGIA MAANA MUDA UMEENDELEA SANA.
No comments:
Post a Comment