Wapendwa wangu Mama na Baba.
Tangu Niende Chuo kikuu Najua sijachukua Muda wa kuwaandikia na Naomba msamaha kukosa kufikiria kuwaandikia paka sasa.Nitawaeleza Mambo yote katika Barua hii lakini kabla hamjasoma Tafadhali ketini chini,Tafadhali msisome paka Mketi chini.
Naendelea Vizuri sasa,Jeraha la fuvu la kichwa baada ya kuruka kwa dirisha la Bweni langu Sasa limepona,Niliruka baada ya bweni langu kushika moto muda mfupi.baada ya kuwasili hapa sasa huwa napata maumivu ya kichwa mara moja kwa siku.
kwa bahati nzuri mfanyakazi mmoja alishuhudia moto huo ukiwaka na jinsi nilivyoruka na alikuja na kunipeleka hospitali,Na aliendelea kunitembelea nikiwa huko.Nilipoondoka hospitalini sikuwa na mahali pa kuishi kwasababu chumba changu kiliteketezwa kabisa.
Basi alikuwa mkarimu na kunikaribisha Nyumbani kwake.Nyumba ndogo lakini nzuri sana.
Ni Binti mzuri sana na hata tumepanga kufunga Ndoa,bado hatujaweka tarehe lakini itakuwa Mapema Kabla ya Mimba kuanza kuonekana wazi.Mama na Baba mpenzi wangu ana mimba.Najua jinsi mlivyo nahamu ya kuwa na Mjukuu na hamu ya kumkaribisha mtoto huyu na mtamshughulikia vizuri kama mlivyonifanyia mimi nikiwa mdogo.
Sababu ya Kuchelewa kwa Harusi yetu kwasababu Mchumba wangu ana maradhi lakini si mabaya ambayo yameniambukiza. Kwa jinsi sikuwa mwangalifu.Na hata hivyo namkaribisha katika familia yetu na mioyo mikunjufu.
Ni mtu mkarimu ingawa hajasoma sana lakini ni msichana mwenye Maono.Ingawa ni mtu nwenye dini nyingine na asili tofauti.Najua hautatizwa na jambo hilo sababu mara nyingi mnasema "Mnastahimili tabia na tofauti za Watu".
Mama na Baba kwa kutamatisha nimewaelezea kila kitu lakini ningependa kuwaambia kuwa hakukuwa na Moto katika Bweni langu wala sina kovu katika fuvu la kichwa,sikuwa hospitalini,hana Mimba na wala sina Mchumba maishani mwangu.Hata hivyo nimekuwa nikianguka katika Historia na Sayansi.Nilitaka muone kuanguka kwangu kwa mtazamo unaofaa.
Ni Mimi mwanao Jimmy J.
.................................................................................
Unaweza Kufikiri wazazi hawa Walivyofurahia"Ooooh Asante Mungu kumbe haufanyi vyema masomoni?"Kama tu angewapigia Simu na Kusema "Nimeanguka katika historia na Sayansi" Yamkini wangemkasirikia na Kumzoma na kumpigia kelele Naye angekasirika na Kuanza kulia.
Pengine Unahitaji Kuchukua Muda kidogo na Uangalie tatizo lako katika mtazamo Unaofaa kwa kuzingatia yale yanayoendelea duniani naMatatizo ya watu wengine wanayokabiliana nayo.....
Uhuru wa mwisho wa Mwanadamu ambaye hakuna mtu anayeweza kumpokonya ni uwezo wake wa kuamua Mtazamo ataoshulikia katika hali yeyote.
Wakati mwingine nikiwa katika hali ngumu nasema "Mungu Sipendi hali hii inanitia Uchungu lakini nitakuwa na furaha kwasababu najua nitafaidika na hali hii.Nitakomaa zaidi na Nitafaidika kupitia hali hii.
*Jimmy J*
#Mtazamo
No comments:
Post a Comment