Mnamo mwaka 1987, jarida la The Los Angeles Times lilichapisha kisa cha mtu mmoja mwenye umri wa miaka 53 aliyependa kuteleza juu ya theluji. Bwana huyu aliitwa Ed Kenan. Kenan alikuwa mfanya biashara aliyependa mchezo wa kuteleza na alikuwa anafanya mazoezi kisha ashindane katika mashindano makubwa ya kuteleza wakati wa michezo ya Winter Olympics.
Lakini kulikuwa na kitu kisicho cha kawaida juu ya Ed Kenan: Alikuwa kipofu. Miaka saba iliyokuwa imepita, Kenan alipoteza uwezo wa kuona, jicho moja nilipoteza uwezo kisha lingine likafuata. Upasuaji aliofanyiwa mara mbili haukuweza kuzuia retina zake zizipofushe macho yake. Katika kukabiliana na matatizo hayo yasiyoneneka, Kenan alikuwa na uamuzi wa kufanya:
Alikuwa anaweza kukaa gizani, na kujisikitikia, na kukasirika kwamba maisha yamemwendea vibaya, au angeendelea mbele. Kenan alifanya uamuzi—miezi sita baada ya kupofuka, alikuwa anateleza kwenye theluji huko Vail, Colorado, Akasema, “Nilijilazimisha kupona,” “Niliona ikiwa naweze kuteleza chini ya mlima, ninaweza kufanya chochote ninachoamua kufanya.” Mnamo mwaka 1983, Kenan alishinda nishani ya dhahabu katika mashindano makubwa ya kuteleza ya U.S. Association of Blind Athletes Alpine Competition huko Alta, Utah. Miaka michache iliyofuata, aliongeza idadi ya medali, kwa kushinda medali kadhaa za dhahabu na fedha katika mashindano mbalimbali.
Hata upofu haukuweza kumzuia Ed Kenan kuishi maisha mazuri kabisa. Alipoulizwa jinsi alivyoweza kuteleza chini ya mlima na kupitia malango kadhaa kwenye eneo hilo la mchezo, Ed alisema kwamba kuna mtu aliyemwelekeza na mtu huyu alikuwa anaona. Msaidizi wake angeteleza mbele yake kuteremka chini ya mlima.
Wakati Ed alipohitaji kuongeza kasi zaidi, yule mwelekezi wake, angeongea kwa sauti ya juu na kusema“Nenda, nenda, nenda” na walipokaribia yale malango, angepaza sauti na kusema “Riiight turn-Geuka kulia,” “Leeeft turn-Geuka kushoto.” Kile Kenan alichofanya ni kuendelea mbele na kuamini maelekezo ya mwelekezi wake. Alipofuata maagizo, angeweza kufuata mkondo wa kuteleza vizuri sana na kuvuka mstari wa kumalizia mashindano salama.1 Ingawa matatizo unayokabiliana nayo huenda ni tofauti na yale ya Ed Kenan, pengine yanafanana na yako kwa kiasi kidogo tu.
Pengine unajua kupoteza kitu au mtu bila kutarajia ni nini. Pengine unajua uchungu wa kukabiliana na hali ya kuvunja moyo sana. Pengine unakabiliana na majibu ya kutisha kutoka kwa daktari. Pengine mtu au kitu ulichodhani kitakuwepo wakati wote kimetoweka ghafla. Na pengine unajiuliza swali hili Je nikate tamaa sasa, au nitafute njia ya kuendelea mbele? Haijalishi umegubikwa na giza la aina gani, hebu nikukumbushe kwamba huko peke yako. Mungu anaona yale unayopitia, na yuko hapo hapo pamoja nawe. Isaya 30:21 inasema, “na masikio yako yatasikia neno nyuma yako, likisema, Njia ni hii, ifuateni; mgeukapo kwenda mkono wa kulia, na mgeukapo kwenda mkono wa kushoto.” Hiyo inamaanisha Mungu ameahidi kuwa kiongozi wako. Unapokuwa huoni unakoelekea, usiogope. Usijifanye kifaurongo!
Wakati mwingine kwenda mbele kunamaanisha kuamka kitandani na kusafisha nyumba yako, au kwenda kazini; wakati mwingine kunamaanisha kufuata maelekezo fulani kutoka kwa Mungu. Vyovyote vile, iwe rahisi au hali ngumu zaidi, Mungu anataka tuwe watendaji ili tusidorore kiroho! Mungu atakuongoza na utamsikia akisema “Riiight turn-Geuka kulia,” “Leeeft turnGeuka kushoto.” Kadri unavyotumia imani yako zaidi, ndivyo utakavyokuwa na imani zaidi! Yesu alisema, “Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.” (Mathayo 25:29). Alikuwa anaongea juu ya imani iliyohitajika ili mtu achukue hatua badala ya kujificha kwa woga. Endelea mbele—Ni moja ya mambo makubwa zaidi unayoweza kufanya.
Jimmy J.
No comments:
Post a Comment