Kuna hadithi moja niliwah sikia ya wanaume watatu waliojikuta wanafanya kazi mahali pa kipekee kabisa. Wanaume hawa walikuwa wafanya kazi wa kawaida waliokuwa wameajiriwa ili kusaidia kujenga kanisa kubwa la London ambalo ujenzi wake ulikuwa unaendelea. Kanisa hili kubwa lilikuwa nimesanifiwa na msanifu majengo maarufu kwa jina Sir Christopher Wren na lilikuwa linatarajiwa kuwa kanisa kubwa lenye usanifu wa kipekee. Basi mwanahabari mmoja wa London alipokuwa akiandika makala juu ya kanisa hilo kubwa lililokuwa likijengwa aliwauliza wale wanaume watatu swali hili rahisi: “Mnafanya nini hapa?” Yule mwanaume wa kwanza akasema “Ninakata mawe kwa shilingi 10 kwa siku.” Yule wa pili akajibu akasema, “Ninafanya kazi hapa kwa saa 10 kila siku.” Lakini yule wa tatu alitoa jibu tofauti kabisa: “Ninamsaidia Sir Christopher Wren kujenga moja ya makanisa makubwa zaidi mjini London.”
Ni ajabu sana jinsi mtazamo wako unavyoweza kuathiri mtazamo wako wa maisha? Kile unachochagua kuamini ni muhimu. Yule mfanya kazi wa kwanza aliamini pesa ndiyo kitu cha msingi. Alipoulizwa juu ya kazi yake, jambo la kwanza aliloliongelea ni kiwango cha pesa (jinsi kilivyokuwa cha chini) alichokuwa analipwa. Mfanyakazi wa pili aliamini muda wake ndio uliokuwa muhimu zaidi. Alipoulizwa aeleze alichokuwa akifanya, bila kusita aliongea kuhusu saa nyingi alizokuwa anatumia kuwa kazini.
Lakini mfanya kazi wa tatu aliamua kutazama mbele zaidi kupita zile pesa alizokuwa akipata na muda aliotumia. Hakuona mradi huu kuwa kazi kama kazi zingine. Aliiona kuwa ni fursa ya ajabu—nafasi ya kujenga kanisa kubwa sana. Aliona yale mazuri kabisa katika hali yake, na hiyo ilimfanya asisimke na afurahie kazi iliyokuwa mbele yake. Ninaamini moja ya mambo ya thamani kabisa unayoweza kufanya ili uishi maisha yaliyojaa matumaini, yenye furaha, ya ushindi ni kuamini yale mazuri katika kila hali. Hilo si jambo rahisi la kufanya wakati wote. Ni jambo la kawaida kupata makosa na kupata wa kulaumiwa—miili yetu hufanya hivyo moja kwa moja. Lakini kuona na kuamini yale yaliyo mazuri ndio uamuzi bora zaidi. Ni uamuzi unaoufanya kubadilisha hali ya maisha yako kutoka hali mbaya hadi hali nzuri. Badala ya kufikiria mabaya zaidi ndiyo yatakayotokea, amini kuwa mazuri zaidi yatatokoea.
Muwazie mazuri zaidi mfanya kazi mwenzako. Liwazie mazuri zaidi kanisa lako. Mwazie mazuri zaidi mkeo au mumeo. Iwazie mazuri zaidi afya yako. Wawazie mazuri zaidi watoto wako. Waza mazuri zaidi kuhusu maisha yako ya usoni. Utashangaa jinsi mtazamo wako wote wa maisha utakavyobadilika kwa kuwawazia mazuri watu wengine na hali zako katika maisha. Yesu alitupa amri mpya, nayo ni tupendane sisi kwa sisi kama alivyotupenda yeye. Neno la Mungu linatufundisha kwamba upendo wakati wote hutumaini yote (1 Wakorintho 13:7).
Kusema kweli, Maandiko yanasema kwamba upendo “huwa tayari wakati wote kuamini yote” ya kila mtu. Kila asubuhi waza kwamba kila kitu kitakwenda vizuri siku nzima. Nadhani ni kitu ambacho lazima tukifanye kwa kukusudia! Unaweza kuwa kama wale wafanyakazi wawili wa kwanza ambao walienda kazini kila asubuhi na kuona tu mshahara mdogo na saa nyingi za kazi mbele yao. Walikuwa na mitazamo iliyokosa hamasa na kuyaona maisha kuwa kitu kisichopendeza. Au unaweza kuwa kama yule mfanyakazi wa tatu aliyeona nafasi nzuri badala ya kuona ni kazi tu. Aliamini kwamba kile alichokuwa anafanya ni muhimu, na kila siku alisisimka kuhusu kazi yake. Ni suala la mtazamo tu. Watu wote watatu walifanya kazi moja, lakini mmoja tu ndiye aliyeifurahia.
Kila wakati ninapoona vigumu kuwa na mtazamo chanya juu ya kile ninachokifanya, hunisaidia sana kukumbuka kwamba ninamtumikia Kristo.
Lolote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu. Mkijua [kwa hakika] ya kuwa mtapokea kwa Bwana [si kwa wanadamu] ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo (Masihi). Wakolosai 3:23-24
Jimmy J.
No comments:
Post a Comment