Mojawapo ya vizuizi vibaya zaidi vinavyotuzuia kuishi maisha ambayo Mungu anataka uishi ni ule mtazamo wa kiakili wa siwezi. Siwezi ni tundu lisilokuwa na msamaha lililotengenezwa ili likuzuie kuinuka na kufikia kilele cha uwezo wako.
Hebu piga taswira ya tai anayependeza na asiye na manyoya mengi—ndege ambaye aliumbwa ili apae kwenye mabawa ya upepo—akiwa amejibanza kwenye tundu, akiwatazama tai wengine wakipaa juu. Haya ndiyo yanayotokea ukiishi na akili yenye mtazamo wa siwezi. Badala ya kuishi maisha uliyoumbwa kwayo, umekwama katika kifungo cha kuwekewa mipaka na mapungufu.
Siwezi kuidhibiti hasira yangu. Siwezi kupata kazi. Siwezi kusahau mabaya niliyotendewa. Siwezi kuendelea. Sielewani na mke/mume wangu. Siwezi kuruhusu mtu aniumize tena. Siwezi kutatua tatizo hili. Siwezi kulea watoto hawa peke yangu. Siamini haya yamenipata. Siwezi...Siwezi...Siwezi. Tunaweza kuongea mpaka jioni. Hakuna mwisho wa mambo ambayo watu hufikiria hawawezi kuyafanya. Lakini umetambua kipengele muhimu katika orodha ya mawazo iliyopita?
Si. Siwezi...Siwezi...Siwezi...Si... Si...Siwezi ni mtazamo wa kiakili ambao unajiangalia mwenyewe. Hautegemei kusaidiwa na watu wengine, na bila shaka hautegemei kusaidiwa na Mungu. Mtazamo wa siwezi huangalia sehemu ambazo tuwadhaifu kabisa na kufanya hitimisho la kukatisha tamaa: Siwezi kukifanya. Hakuna jipya.
Wanawake na wanaume katika Biblia walikumbana na mtazamo huu. Sara alifikiria, siwezi kuzaa watoto; nimezeeka sana (Mwanzo 18:10–12). Musa alifikiria, siwezi kusimama mbele ya Farao; siwezi kuongea vizuri (Kutoka 6:30). Gideoni alifikiria, siwezi kuwaongoza Waisraeli; mimi ndiye mdogo katika nyumba ya baba yangu (Waamuzi 6:15).
Esta alifikiria, siwezi kuwaokoa watu wangu; sitaweza kumwona mfalme (Esta 4:11). Isaya alifikiria, siwezi kutoa unabii; mimi ni mtu mwenye midomo michafu (Isaya 6:5–7). Wanafunzi walifikiria, Hatuwezi kulisha kundi hili lote la watu; tuna mikate mitano tu na samaki wawili (Mathayo 14: 15–18). Katika kila moja ya hali hizi, siwezi lilikuwa kama tundu la kujijengea, likijaribu kuwazuia wanawake na wanaume hawa wasitimize mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha yao. Lakini Mungu kamwe hakunuia kwamba Sara, Musa, Gideoni, Esta, Isaya, au wanafunzi wake wafanye chochote kwa nguvu zao wenyewe, kulingana na uwezo wao wenyewe. Alijua wasingeweza... lakini hilo halikujalisha, kwa sababu yeye aliweza. Kupitia Kristo tunaweza kutenda chochote tunachohitaji kufanya.
Tunaweza kukabiliana na chochote! Nayaweza mambo yote katika yeye [Kristo] anitiaye nguvu. Wafilipi 4:13 Ilikuwa kweli: Sara alikuwa amepita umri wa kuzaa watoto; Musa hangeweza kumshawishi Farao yeye peke yake; Gideoni hakuwa na sifa zinazofaa kuliongoza jeshi; Esta alikuwa hajaitwa kwenda mbele ya mfalme; Isaya alikuwa mtu mwenye midomo michafu; na wanafunzi hawakuwa na chakula cha kutosha kulisha kundi la watu. Lakini lengo la Mungu lilikuwa ni kushinda kila siwezi ili aweze kutimiza mpango na lengo lake. Watu hawa wote walikuwa hawana budi kutambua na kuondoa mitazamo yao ya “siwezi.” Badala ya kuangazia udhaifu wao, walichagua kuangazia nguvu za Mungu, na matokeo yakawa ya ajabu sana. Mungu alitenda mambo ya ajabu katika maisha yao na kupitia imani yao na utiifu wao. Hivyo ndivyo ilivyo hata kwako wewe.
Ninatambua kwamba kuna mambo unayokabiliana nayo leo ambayo yanaweza kukufanya ukajisemea hiki siwezi kukifanya. Siwezi kukabiliana na hali hii tena. Siwezi kuvumilia hali hii tena. Siwezi kusubiri jibu. Siwezi kusamehe kamwe. Kama ungejua yale ninayopiitia, ungeelewa. Siwezi kufanya.
Lakini ningependa kukwambia kwamba Mungu anajua huwezi ... na hiyo haijalishi, kwa sababu yeye anaweza. Yesu akawakazia macho, akasema, Kwa wanadamu haiwezekani, bali kwa Mungu sivyo; maana yote yawezekana kwa Mungu. Marko 10:27
No comments:
Post a Comment