Allaha alimfufua Yesu kwa ajili yake mwenyewe:
“Bali Mwenyezi Mungu alimtukuza kwake na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima” (Kurani 4:158).
Yeye Aliye Juu sana ana nguvu ya kumfufua Yesu kwa ajili yake mwenyewe, na hili linathibitishwakwenye Injili.

“Baada ya Bwana Yesu kusema nao, alichukuliwa juu mbinguni na kuketi mkono wa kuume wa Mungu” (Marko 16:19).
Kurani inasema kwamba Allah aliitangua mipango ya Mwanadamu:
“Na makafiri walipanga mipango na Mwenyezi Mungu akapanga mipango, na Mwenyezi Mungu ndiye bora wa wenye kupanga" (Kurani 3:54).
Hekima ya Mungu inafunuliwa na Roho Mtakatifu. Biblia inafafanua juu ya mipango ya Mungu aliye juu:
Hekima ya Mungu inafunuliwa na Roho Mtakatifu. Biblia inafafanua juu ya mipango ya Mungu aliye juu:
"Bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangeliijua, wasingalimsulubisha Bwana wa utukufu; lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu). Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao. Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukupokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni" (1 Wakorintho 2:7-13).
Kutokana na Kurani ile siku ambayo Yesu alifufuliwa ilibarikiwa. “Na amani iwe juu yangu siku niliyozaliwa. Na siku ya kufa. na siku ya kufufuliwa kuwa hai” (Kurani 19:33).
Ni vizuri kuuamini ukweli wa kwamba Yesu alikufa na akafufuka na kuwa hai. Biblia inasema:
"Ninaomba pia “macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, ili mpate kujua tumaini mliloitiwa, na utajiri wa urithi wa utukufu wake katika watakatifu jinsi ulivyo, na ubora wa uweza wake mkuu usiolinganishwa kwa ajili yetu sisi tuaminio . Uweza huo unafanya kazi ndani yetu, ni sawa na ile nguvu kuu mno ambayo aliituma alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, akamketisha mkono wa kuume katika mbingu, juu sana kuliko falme zote na mamlaka enzi na milki na juu ya kila jina litajwalo si katika ulimwengu huu tu bali na katika ule ujao” (Waefeso 1:18-21).
Mungu alimfufua Yesu kutoka kwa wafu na kuwa na ushindi dhidi ya wale wasioamini. Ushindi huu ulikuwa mkuu mno, kwani aliye juu ni Mwenye uweza wote.

Pale Mwenyezi Mungu aliposema: “Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na nitakunyanyua kwangu, na nitakutase na wale waliokufuru, na nitawaweka wale waliokufuata juu ya wale waliokufuru, mpaka siku ya kiyama. Kisha marejeo yenu yatakuwa kwangu. Nikuhukumuni katika yale mliyokuwa mkihitilafiana”(Kurani 3:55).
Injili inatuambia kwambaYesu alikufa na akafufuka kutoka wafu. "Ni kweli Bwana amefufuka" (Luka 24:34).
Manabii wa zamani sana bado wamo kwenye makaburi yao. Lakini YesuKristo amefufuka kutoka kwa wafu. Ukweli wa kwamba Yesu amefufuka ni ushahidi tosha kwamba yeye ni Mwokozi wa ulimwengu.
Njoo kwa YESU.
No comments:
Post a Comment