Tuesday, 10 October 2017

MUHAMMAD MTUME BANDIA


Waislam watabisha kuhusu utume bandia wa Muhammad ila wengi tunajua kwa ushahidi kuwa muhaamada alikuwa hajawah na hatakuja kuwah kuwa mtume wa Mwenyenzi Mungu Bali ni mtume Bandia yaani utume wa kutungwa kama taarabu.Tukiangalia historia ya muhaamad...Muhammad alipotimiza umri wa miaka 38kutokana na maisha magumu ,alihama toka nyumbani kwake, akahamia katika mapango(JABAL HIRA) yaliyokuwa hapo karibu na mji wa Makka. Alipofikisha umri wa miaka 40 siku moja alitokewa na kiumbe ambacho Waislamu leo wanakiit Malaika Jibril.

Wahyi (ufunuo) uliokuja kwa Muhammad alisikia makengele,uso kuwa mwekundu,jasho
kumtoka. Katika Bukhar, Hadithi na 2, Juzuu na 1,Al-Lu'lu Kitabu cha 3.Uk. Na.874 Hadithi na1505 "Hadithi ya Aisha r.a mama wa waumini amesema, kuwa Al Harith ibn Hisham r.a alimuuliza mtume wa Allah s.a.w ' Ewe mtume wa Allah hivi wahyi (ufunuo) hukujia vipi?'
mtume wa Allah s.a.w akajibu, " Wakati mwingine hunijia kama mlio wa kengele, na aina hiyo ndiyo ngumu zaidi kwangu, inaondolewa hali hiyo kwangu wakati tayari
nimeshapata wahyi.

Na nyakati nyengine malaika anakuja kwangu akiwa katika mfano wa mtu, kwa hiyo ananieleza na ninayazingatia aliyoyasema." Aisha r.a alisema , Na hakika nilimwona unamshukia wahyi siku ya baridi kali na ilipomuondoka hali hiyo, paji lake la uso lilichuruzika jasho."
Qurani 53:2 - 6 Suratul Najm (Nyota) "Kwamba
mtu wenu huyu Nabii Muhamad (hakupotea kwa ujinga) na wala hakukosa (Na hali ya kuwa anajua). Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake). Hayakuwa haya (anayosema) ila ni wahyi (ufunuo) uliofunuliwa (kwake).Amemfundisha
(malaika) mwenye nguvu sana. Mwenye uweza na yeye (huyu Jibril) akalingana sawa sawa.
Ngoja tuendelee na mawaidha!!

Alipokuwa pangoni alichezewa na Shetani:Katika kitabu kiitwacho " Wakeze Mtume
Wakubwa Na Wanawe" kilichoandikwa na Sheikh Abdullah Saleh Al Farsy uk.12 tunasoma
maneno haya "Basi Mtume akafanya hofu akarejea kwa mkewe akamhadithia; na pale pale homa kubwa kabisa ikampanda akataka afunikwe maguo.Mara akawa anatetemeka kwa nderema na
anaweweseka na kusema "Najikhofia nafsi yangu kuchezewa na shetani na kuniharibu akili
yangu na kunizuga". Bibi Khadija palepale alimdakiza akamwambia; " Wacha hayo; Siyo
yatakayokuwa hayo. Wewe huwezi kuchezewa na mashetani. Shetani hawezi kumchezea mtu
mwenye sifa zako. Wewe unatazama vyema jamaa zako, unachukuwa mizigo ya hata watu
wasiokuwa wako, unawadhihirishia watu sifa zako nzuri ambazo hakuna mwenye nazo.
Unafanya hivi na unafanya hivi. Furahi ndugu yangu. Tua moyo wako, Wallahi! Mimi naona
umekwishakuwa mtume".

Katika tukio hili lililompata Muhammad akiwa pangoni , ndipo Waislamu wote ulimwenguni
wanapolieleza kuwa hapo ndipo Muhammad s.a.w alipoletewa wahyi (ufunuo) na kupewa
unabii na utume. Lakini unapotafakari juu ya ujumbe huo utaona kuwa hata yeye mwenyewe
hajui nini kilichokuwa kimemtokea kule pangoni. Ndiyo maana tunasoma kuwa alipofika
nyumbani kwake mkewe Bi. dija ma. Kha Khadija dija Khadija Muhammad Khadija Khadija
alimweleza mke Khadija we kilichomtokea kuwa ni "Shetani" hakumsema malaika yeyote kama
Waislamu wanavyotaka kutuaminisha leo. Kwa sababu kama angekuwa kamatuma kama tunavyosoma ndani ya Biblia ,asingesita kujitambulisha kwa Muhammad kuwa yeye ni nani. Hii ni hoja ya kwanza.

Hoja ya pili tunaona kuna mtu anaitwa Waraqah ibn Naufal, binamu yake na mke wa Muhammad s.a.w Bi Khadija. Yeye Waraqah anamwambia Muhammad huyo aliyekutokea ni malaika Jibril.Basi jibashirie kuwa wewe ni mtume umma huu huu !!!!! Je alikuweko pangoni wakati Muhammad s.a.w akitokewa na kiumbe asichokijua?

Hoja ya tatu tunaona hata huyo mkewe Muhammad anamwambia mumewe utume huo !!!!!!! Je na yeye alikuweko pangoni?Kama hakuweko ni nani aliyemwambia kuwa yule ni
malaika Jibril ikiwa Muhammad mwenyewe aliyetokewa alisema nimetokewa na Shetani?Tafakari
Katika kitabu kiitwacho Tafsir Al-Kashif, cha Muhammad Jawad Mughniyyah, uk74 paragrafu
ya 7 inasomeka" Hakuna njia ya kumjua Iblis,Shetani na Jini, isipokuwa kwa njia ya wahyi(ufunuo) tu" Qurani Suratul Sad 38:69 Muhammad amenukuliwa akisema "Sikuwa na ilimu ya viumbe watukufu(Malaika)…

Kwa sababu ya Muhammad s.a.w kutowajua malaika kwake yeye anasema unapomwona
punda akilia basi kamwona Shetani.
Katika Kitabu kiitwacho Mkweli Mwaminifu, Juzuu 3-4
Hadith 789 uk 38 " Punda akilia kamwona Shatani"
Jambo hilo ni tofauti na jinsi Biblia Takatifu inavyoeleza kuhusu punda. Mungu anaweza kumtumia hata punda kuongea na wanadamu ili kuwajulisha ujumbe wake. Katika kitabu cha Hesabu 22:22-31 tunasoma habari ya Balaamu jinsi Mungu alivyomtumia punda kumwambia Balaamu asiendelee na safari yake , baada ya punda huyo kumwona malaika wa Bwana akiwa ameshika upanga na amesimama mbele yao akiwa amezuia njia aliyotakiwa kupita. Punda alimwambia Balaamu ule msitari wa 30-31 "Yule punda akamwambia Balaamu, Je mimi si
punda wako, nawe umenipanda maisha yako
yote hata leo?Nimezoea kukutenda hayo?
Akasema La!. Ndipo Bwana akafunua macho ya
Balaamu, akamwona malaika wa BWANA
amesimama njiani, ana upanga mkononi
mwake, umekwisha kufutwa; naye akainama
kichwa, akaanguka kifudufudi"

Inaonekana kwa tukio hili lililomtokea Balaamu,Mungu alimfunua macho yake akamwona malaika.
Lakini kwa Muhammad yeye anachokiona ni Shetani tu. Na ndiyo maana anasema punda akilia amemwona Shetani Kwa hiyo kama ufunuo wa Muhammad unaanza na Shetani kama vitabu sahihi vya dini ya Kiislamu vinavyoeleza, kwa mujibu wa ufafanuzi wa kitabu hicho cha Tafsir Al Kashif, inaonesha kwamba ufunuo, unabii na hata utume wa Muhammad una walakini mkubwa ukilinganisha na ujumbe wa manabii na mitume waliotajwa ndani ya Biblia Takatifu. Katika Biblia shetani ametajwa kuwa anaweza kujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

2 Wakorintho 11:13-15 "Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. Wala si ajabu, maana shetani mwenyewe
hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakajigeuza
wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao".
Muhammad akiwa Medina aliulizwa na Wayahudi ikiwa ufunuo wake umetoka kwa
Mungu wa Kweli kwa kumtaka atoe sifa za manabii. Akijibu swali hilo alisema: Mkweli Mwaminifu Juzuu 3-4 Uk.63.Hadithi Na. 880. "Kasema Mtume (s.a.w):- (Mambo) manne ya sheria za mitume (Kuwa na) na haya,na kujipaka mafuta mazuri,na kuowa (wake),na kupiga mswaki.
Hizi si sifa za Ki-Mungu kwa nabii na mtume bali ni za kibinadamu tu.

Manabii na watu mbalimbali katika Biblia hawakuona haya. Soma Isaya 50:7 " Maana Bwana MUNGU atanisaidia; kwa sababu hiyo sikutahayari, kwa sababu hiyo nimeukaza uso
wangu kama gumegume, nami najua ya kuwa
sitaona haya". Zaburi 34:5 " Wakamwelekea
macho wakatiwa nuru, Wala nyuso zao
hazitaona haya" Zab 119:46 "
Nitazinena shuhuda zako mbele ya wafalme, Wala sitaona aibu" Warumi 1:16 " Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao
wokovu, kwa kila aaminiye kwa Myahudi
kwanza , na kwa Myunani pia" 1Petro 4:16 "
Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali
amtukuze Mungu katika jina hilo.

Zaidi ya hayo tunaona Muhammad alirogwa. Kurogwa ni hali ya mtu kuathirika na nguvu za
giza yaani uchawi.. Je nabii au mtume wa Mwenyezi Mungu wa Kweli anaweza kurogwa?
Katika Qur'an Suratul Ban-Israel, 17:47 "Tunajua sana, sababu wanayosikiliza, na wanaponong'ona,wanaposema hao madhalimu.Nyinyi hamfuati isipokuwa mtu aliyerogwa"
Pia katika Suratul Falaq, 113:1-5 " Ninajikinga kwa mola wa ulimwengu wote na shari ya Alivyoviumba, na shari ya giza la usiku liingiapo, na shari ya wale wanaopulizia (vivia)
mafundoni (wakavunja) mashikamano yaliyo baina ya watu yaani shari ya mafatani, Na shari ya hasidi anapohusudu" Tunasoma tukio hilo katika ufafanuzi wake uliyomo ndani ya Qur'an chapa ya nane uk.977unaofafanua Sura ya 113-114 "Athari ya uchawi juu ya mtume (s.a.w).

Swali la pili lijitokezalo kuhusu sura mbili hizi ni kwamba kwa mujibu wa hadithi uchawi ulifanywa dhidi ya mtume(s.a.w) naye akawa mgonjwa, na ili kuiondoa athari hiyo ya uchawi Jibril (a.s) alikuja nakumpa maelekezo Mtume (s.a.w) ya kusoma sura mbili hizi. Watafiti wengi zamani na wa sasa wamelifanyia upinzani jambo hilo, kwamba ikiwa hadithi zitakubaliwa, basi mfumo wote wa sharia utakuwa ni wa kutiliwa shaka, kwa sababu kama mtume (s.a.w) aliweza kuathirika kwa uchawi, na kwa mujibu wa hadithi hizi kweli uchawi huo ulionesha athari yake, basi hatuwezi kukaidi au kukana hadi kiwango gani maadui waliweza kumfanya Mtume (s.a.w)aseme na atende mambo kwa nguvu ya uchawi,na katika mafundisho yake mambo mangapi yatoka kwa Allah na mangapi yatokana na athari ya uchawi juu yake. Si hiyo tu, bali pia wasema kuwa baada ya kuyatambua hayo kuwa ni kweli katu haitawezekana hata kule kukaidi kuwa(s.a.w) alishawishiwa kudai utume kwa mauzauza ya kinjozi kuwa alimjia malaika.

Pia wanasema hadithi hizi zapingana na Qur'an, na kama ilivyo katika Qur'an kuwa tuhuma hiyo batili kwa makafiri ilivyotajwa kuwa mtume s.a.w amerogwa naye ameathirika na uchawi: wanaposema hao madhalimu, 'Ninyi hamumfuati isipokuwa mtu aliyerogwa'." (17:47), lakini hadithi hizi zinathibitisha madai ya makafiri kuwa kwa kweli aliathirika na kuongozwa na uchawi……
Kadri historia inavyohusika,ukweli kuwa kiasi fulani cha athari ya uchawi juu ya Mtume (s.a.w) ni hakika iliyothibiti; na kama kwa ustadi wa ubishi inawezekana kuthibitisha kuwa kweli.Limesimuliwa jambo hilo na Bukhari,Muslim, Nasai, Ibn Majah, Ahmad, 'Abdur Razzaq, Humaid, Baihaqi, Tabarani, Ibn Sa'd,Ibn Marduyah, Ibn Abi Shaibah, Hakim, Abd bin Humaid na Muhadithina wengine toka kwa Bi.'Aisha (r.a), Zaid bin Arqam, Ibn 'Abbas kupitia silsila nyingi mno kiasi kwamba jambo lenyewe limefikia hali ya ufululizo kamili, isipokuwa kila Hadithi, yenyewe ni ripoti kamili.

Hii ni uthibitisho mwingine mzito unaoonesha kuwa utume wa Muhammad una utata. Ikiwa na wao Waislamu kwa mujibu wa hadithi hizi hawajui ni mambo mangapi Muhammad
aliyoyasema yanatoka kwa Allah na mangapi aliyasema akiwa ameshinikizwa na wachawi ,
Je ufunuo na utume wake utakuwa umetoka kwa Mungu wa Kweli? Tafakari !!Ndani ya Biblia Takatifu hakuna kurogwa kwa mtu wa Mungu.

Hesabu 23:23 " Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israel. Sasa habari za Yakobo na Israel zitasemwa , Ni mambo gani aliyoyatenda
Mungu!"
Kwa mujibu wa kitabu cha Biblia Takatifu,
manabii na mitume wa kweli wa Bwana Mungu wanatoka katika taifa la Israel.Kitabu cha Ezekiel 13:9 " Na mkono wangu utakuwa juu ya manabii wanaoona ubatili, na
kutabiri uongo;hawatakuwa katika mashauri ya watu wangu, wala hawataandikwa katika
maandiko ya nyumba ya Israel, wala hawataingia katika nchi ya Israel; Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana MUNGU" .Pia kwa mujibu wa kitabu cha Qur'an manabii na mitume ni lazima watoke kwa Yakobo ambaye ni mtoto wa Is-haqa ambaye naye ni mtoto wa Ibrahim.
Qur'an Suratul Al-Ankabuut,(Buibui), 29:27 " Na tulimpa (kumzaa nabii) Is-
haqa na (kumjukuu nabii) Yakubu na tukauweka katika kizazi chake unabii na (kupata) kitabu,na tukampa ujira wake katika dunia; naye katika akhera kwa yakini atakuwa miongoni
mwa watu wema".

Aya hii, inaendelea kusisitiza kuwa ni kupitia kizazi cha Yakobo ndiko uliko unabii na kupata kitabu. Kwa bahati mbaya Muhammad ibn Abdullah, hatoki katika kizazi hicho wala kwa
Ishmael kama wanavyodai Waislamu . Kwa sababu Ishmael ni Mwebrania kama baba yake mzee Ibrahim alivyo Mwebrania (Mwanzo 14:13)na Muhammad ni mwarabu kutoka kabila la Maqureysh. Kwa kutambua hilo ndipo tunamwona Muhammad akiwaonya watu wengine wajiepushe na watu wa kabila lake.

Sahih Al-Bukhari Vol.1.Hadithi Na. 801 na Al-Lu'lu Kitabu cha 3. Uk.1089.Hadithi Na.1846inasomeka"Hadithi ya Abu Huraira (r.a)amesema ,"Mtume wa Allah (s.a.w)
amesema,Kabila hili la Makuraish litawateketeza watu.' Wakauliza, 'Unatushauri nini?' Akasema, Nashauri watu wajitenge nalo."
Kumzamisha nzi kwenye kinywaji
Bukhar vol. 4 Hadith 537 " Narrated Abu
Huraira: The Prophet said: If a house fly falls in the drink of any one of you, he should dip it (in
the drink) for one of its wings has a disease and the other has the cure for the disease"
Tafsiri: Ilisimuliwa na Abu Huraira: Nabii alisema kama nzi akiangukia ndani ya kinywaji
cha mmoja wenu, anapaswa kumzamisha kabisa (ndani ya kinywaji) kwa kuwa bawa lake moja lina ugonjwa na bawa lake jingine lina dawa Mitume wa Yesu ndani ya Biblia Takatifu
walikwisha kutuonya kuhusu uchafu huo. Katika 2 Kor 7:1 "Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza
utakatifu katika kumcha Mungu"

Miongoni mwa mafundisho ya Muhammad ni kwamba kuna mambo kumi yanayokamilisha
Uislamu nayo tunayasoma katika kitabu kiitwacho Mkweli Mwaminifu , Kilichoandikwa
na Sheikh Said Moosa Al-Kindy wa Muscut,Juzuu 3-4 Uk 63.Hadithi Na.880 " Kasema
Mtume (s.a.w) (Mambo) kumi ya Uislamu (yanayokamilisha Uislamu):Kukata
masharubu,na kuziweka ndevu,nakuziweka ndevu (kutozinyoa) ndevu,na kupiga
mswaki,kusafisha ndani ya pua kwa maji,na kukata kucha,kuosha mikono baina ya vidole,na kung'oa (au kunyoa) nywele za kwapani,na kunyoa nywele za mbeleni (mavuzi),na
upungufu wa maji. La kumi,kasema sahaba aliepokea hadithi hii kuwa nimesahau,lakini
kasema bila shaka la kumi ni "kutahiriwa."
Kwa mujibu wa Biblia manabii na mitume
wanathibitishwa kwa njia ya miujiza.

Kutoka 14:21" Musa akanyosha mkono wake juu ya bahari,BWANA akaifanya bahari irudi nyuma kwa upepo wa nguvu utokao mashariki,usikukucha,akaifanya bahari kuwa nchi kavu".
Matendo 19:11-12 "Mungu alifanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida . Hata
wagonjwa wakaletewa leso na nguo zilizotoka mwilini mwake magonjwa yao yakawaondokea,
pepo wachafu wakawatoka". Tazama pia Matendo 16:16-18, 20:7-12 na Matendo
13:6-12.

Qur'an nayo inathibitisha kuwa manabii na
mitume ni lazima wafanye miujiza.
Qurani 40:78 Suratul Al-Muumini [Waumini]
inasomeka "Na kwa yakini tumewatuma mitume kabla yako wengime katika wao tumekusimulia
(majina yao na habari zao) na wengine hatukukusimulia na haikuwa kwa mtume yoyote kuleta muujiza wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu"

Muhammad hakupewa kufanya muujiza wowote ili kuthibitisha madai ya unabii na utume wake.
Qur'an 29:50 Suratul Al-Ankabuut (Buibui). "Na walisema "Mbona hakuteremshiwa miujiza kutoka kwa Mola wake? Sema miujiza iko kwa Mwenyezi Mungu tu (akitaka atakuteremshieni
na kama hataki basi),nami hakika ni mwonyaji
mbainishaji (dhahiri tu)."
(Taz.Qur,an6:35-37
13:7,)Katika Qur'an iko aya ambayo tunapaswa
tuitafakari wote kwa pamoja.Katika Surat An-Nisaa, (wanawake), 4:79 "Wema uliokufikia
unatoka kwa Mwenyezi Mungu na ubaya uliokufikia unatoka nafsini mwako, mwenyewe umefanya mambo hata yakakufika hayo. Nasi tumekupeleka kwa watu kuwa mtume na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kutosha (hapaitajiwi shahidi mwingine)"Aya hii inaonesha kuwa Muhammad mtume wa Waislamu, alipelekwa kwa watu kuwa mtume,huku Mwenyezi Mungu akiwa shahidi tu. Siku zote shahidi si mtendaji bali ni mwonaji tu wa
tendo lililotendeka.Hoja yetu tungependa kuwajua hao watu waliompeleka Muhammad
kwa watu ni akina nani?. Kwa sababu tumeona kule nyuma baada ya Muhammad kutoka pangoni, mkewe Bi. Khadija anamwambia Muhammad kuwa "utume huo!!!!!!! Na Bwana Waraqah ibn Naufal akimwambia Muhammad kuwa " basi jibashirie kuwa wewe ni mtume wa umma huu" kabla ya Qur'an .Je hao si wale "Nasi tumekupeleka" wanaotajwa kwenye aya hiyo hapo juu? Tafakari!! .
Waislamu hudai kuwa Muhammad ametumwa
na Mwenyezi Mungu wao, ambaye ni Mfalme wa
Wafalme .

KAULI HII INAUPA MOYO WANGU UKAKASI
Lakini tusomapo Biblia Takatifu katika kitabu cha Ufunuo 17:14 " Hawa
watafanya vita na Mwanakondoo, na Mwanakondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni
Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme;na hao walio pamoja naye ndiyo walioitwa na wateule, na waaminifu" Katika Ufunuo 19:11-16 " Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe,na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa-kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita. Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi;
naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa Neno la Mungu. Na majeshi yaliyo mbinguni
wakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa kitani nzuri, nyeupe, safi. Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi.
Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na
paja lake, MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA "Yesu Kristo ndiye Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana.Lakini tunaposoma Hadithi sahihi za Kiislamu zinaeleza kuwa adui mkubwa wa Allah (s.w) Mungu wanayemwabudu Waislamu, ni yule anayeitwa Mfalme wa
Wafalme.

Sahih Al- Bukhari, Vol.8.Hadithi Na.225, Al-Lu'lu Wal-marjan,Juzuu ya 3,Hadithi Na.1385
"Hadithi ya Abu Huraira (r.a) amesema,Mtume wa Allah (s.a.w) amesema,"Majina yaliyo dhalili
mno na mabaya mbele za Allah ni mtu kujiita,Malikil-Amlaak (Mfalme wa Wafalme)."
Hivyo, ufunuo aliopokea Muhammad, ambao anatutaka na sisi Wakristo tuuamini haujatoka kwa Mungu tunayemwamini sisi Wakristo, yaani,Yesu Kristo.Bali kama alivyonukuliwa katika
vitabu vya Kiislamu, unatokana na kuchezewa na Shetani, na kwa sababu hiyo kwetu anakuwa nabii na mtume wa uongo'Biblia Takatifu imetuonya kuwachunguza
mitume na manabii.
Katika kitabu cha Ufunuo2:1-2 " Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika; Haya ndiyo anenayo yeye azishikaye hizo nyota saba katika mkono wake wa kuume,yeye aendaye katikati ya vile vinara saba vya dhahabu.

Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao siyo ukawaona kuwa waongo"Kwa mujibu wa aya hizi Muhammad s.a.w hastahili kuitwa nabii na mtume wa Mungu wa Kweli, bali anaangukia katika kundi la manabii na mitume wa uongo. Hatufai.

Moyo wangu unapata ukakasi napoona waislam wanaendelea kumuabudu mtume Huyu!!
Ndugu Zangu waislam bado mnaendelea kumfuataa mtume huyu Mtume huyu bandia ambaye Hana sifa za kitume???
Njoo kwa Yesu.

No comments:

Post a Comment