Tuesday, 10 October 2017

UVULI WA MAUTI


Baba Yangu alifariki kwa ugonjwa wa Moyo.kwenye kitanda cha Hospitali,alikuwa anaagaagaa kwa maumivu makali huku nikiwa nimesimama karibu Naye “Mwanangu niombee,niokoke”alisema kitu ambacho hakuwah kuniomba hapo kabla.sikuwah kuwahi kumwona akiomba,au mtu amuombee.Hakuwahi kukiri dini yake ni dhaifu waziwazi,sikujua nini kimemtokea au aliona nini.jambo moja tu Kutii.

Nikaomba……sikuweza kumaliza maombi yangu……nikiwa katika maombi akakata Roho!Nikawa shahidi mkimya alipoiaga Dunia.katika maumivu makali ndani ya moyo wangu nikatulia pembeni nakutafakari “wala sijishughulishi na mambo makuu,wala na Mambo yashindayo Nguvu zangu.Hakika nimeitunza nafsi yangu,na kuinyamazisha kama mtoto aliyeachishwa,Ndivyo Roho yangu ilivyo kwangu…”Zaburi131;1,2 Daudi alimsihi Mungu kwa ajili ya mwanae aliyekuwa taabani,Alifunga na kwenda nyumbani kwake na kulala chini kwa siku nyingi lakini mwanae alikufa.
Baadae Daudi aliamka kutoka chini,Akaoga,akajipaka mafuta na akabadili mavazi yake,akaingia nyumbani mwa Bwana akaomba.kisha akaenda nyumbani kwake,na akataka wamwandalie Chakula,Naye akala.

Watumishi wake wakamwambia “Ni neno gani hili ulilolitenda?Ulifunga na kulia kwa ajili ya mtoto alipokuwa Hai;lakini mtoto alipokuwa amekufa,uliinuka Ukala chakula!

Akasema,Mtoto alipokuwa hai,nalifunga,nikalia.kwa maana nalisema ‘ni nani ajuaye kama BWANA atanihurumia,mtoto apate kuishi. ‘lakini sasa amekufa,nifungie nini?Je naweza kumrudisha tena?mimi nitakwenda kwakwe lakini yeye Hatanirudia mimi”2 sam 12;16-23.

Baba alikuwa mwislam tangu kuzaliwa,lakini katika dakika chache atake kuombewa,je aliona nini?lakini nilipata tumaini kwa dakika za mwisho ndipo alipomkiri Yesu.sasa ugonjwa wa moyo umeondoa uhai wake,lakini alikufa katika BWANA’.Heri wafao katika Bwana.ufunuo14;13 sasa namshukuru Mungu kwa kumpatia Baba maisha ya umilele,yalimfanya afe katika Bwana.

Nikakumbuka tena”mtoto alipokufa daudi aliinuka kutoka chini,akaingia nyumbani mwa Bwana akamwabudu Mungu. Hicho ndicho Mungu anataka nifanye sasa.Hivyo nitamsifu Bwana kwa kile alichokifanya kwa Hekima yake!

Katika kukaa pembeni ya mwili wa Baba na mawazo mengi sana,nilipokea jumbe kwamba ,shangazi,mjomba na Babu wamefariki kwa ajali,Moyo uliumia sana.

Gafra nilitambua kuwa nilikuwa nakaza macho Bila kuongea Neno,nikatambaaa na kusujudu mpaka chini kwa maumivu makali sana,Tone la chozi likatiririka Hadi kwenye mashavu yangu na kudondoka chini!niliumia na sikuweza kuinuka,nilibebwa na kupelekwa nyumbani kupumzika.
John ambaye alikuwa mchungaji wa karibu na Familia Yetu,alikuja nyumbani na kutueleza kilichotokea kwenye ajali.kifo kilitokea jana, “Dereva alikuwa kwenye mwendo kasi ndipo akakumbana na Roli na kuvaana uso kwa uso”niliiumia sana.

Nilitoka nje na kukuta umati wa ndugu na marafiki,kila mtu akilia,Nilihisi undani wa majonzi yao.
“Wamama wengi walilia baada ya kukuona wewe”alisema John
Niliwaza peke yangu kwa hunzuni”Machozi sio ishara ya woga,kutokutoa machozi vilevile sio ishara ya ujasiri.Katika majonzi manzito wengine hulia,wengine hawalii.

Askari Kijana alikufa vitani.mke wake hakulia hata baada ya kuona Mabaki yake. “alipaswa Kulia Bali hakupaswa kufa”mtu mmoja alisema ujasiri wa marehemu ulidhihirishwa na mke wake.aliwakaziamacho bila machozi.sio kuona mabaki ya mwili wa mmewake wala masimulizi ya tabia ndyo yangemfanya alie;Ni pale nilipomwona mtoto wa kuhuzunisha aliyemfanya kumwaga moyo wake “Nadhani nasikia pia kulia,sio kwasababu naona mabaki ya wafu,bali ni pale napoona kilio cha wafiwa…

Katika mawazo makali,nilijiuliza “kwanini Nashangaa?kifo cha mtu hakinistui?labda sijali kuwepo au kutokuwepo kwa mtu;au upendo wangu kwa watu si mkubwa kama ninavyofikiri?kama mke wangu au mmoja wa wanangu akifa,je naweza kuchukulia kifo kirahisi Hivyo?wakati mwingine nazungumza na marafiki zangu juu ya Habari hizi za mashaka..[katika hali ya majonzi sana]

Nilikuwa nimechoka katika kila njia.Nilijisikia kama mtu mwenye Homa,Nilitaka kulala angalau kwa kitambo kidogo,nilikuwa nafikiri kifo cha mwingine kinaweza niathiri kiasi hichi. “Hebu tusahau vifo vya wengine…..”Nikasemezana mwenyewe. “Je utachukuliaje kifo chako mwenyewe?”Akili yangu haitakuwepo pale katika kutafakari juu ya hali Hiyo.Siku moja nitakutana na kifo uso kwa uso.kama kifo changu ni Leo ningekuwa na mwelekeo gani?Je ningepata amani ya kifo changu mwenyewe?Nikiwanimejinyoosha kitandani nikaingia kwenye mawazo mapana sana ya fikra yangu zilizokuwa zimeniweka kwenye kitanda cha Mauti….je Niko tayari kwa ajili ya mwisho wa maisha Haya?

Asubuh ya jumapili haikuwa nzuri kwangu maana nilizoea siku Hiyo huwa yakupendeza sana kwangu lakini jumapili hii haikuwa hivyo,miili ya marehemu ililetwa nyumbani,Baba,shangazi,mjomba na Babu miili yote iliwasili.

Nilijisikia uzito mwilini mwangu,kama vile kuna mtu alliyekuwa ananivuta kuja duniani,joto la mwili wangu lilipanda kwa kiasi kikubwa,Dactari ambaye ni rafiki yangu alipoona hivyo,akanipatia dawa.Sikutaka kumeza dawa yeyote,Hata kidonge kimoja!Nikahisikama kila kitu kwenye mwili wangu kinazunguka……watu nyumba,miti..kila kitu!hata hvyo nilimeza vidonge.

Majeneza yalifunguliwa,miili ya marehemu ilitolewa nje…sauti za vilio zikasikika kila mahari!sikuwezakumtizama mtu yeyote Yule!!nilikuwa na hangaikia mzunguko wa macho yangu.Hatimaye nikaingia ndani ya Nyumba.nikakaa kwenye kochi,lakini nikashindwa.nikahisi uzito ndani na nje,Nilikuwa natetemeka ndni ya Mwili wangu,wakati mifupa yangu ikiingua…

“Ha,Hupaswi kulala chini namna Hiyo,”Nikajisemea mwenyewe”Tazama ni siku ya mwisho ya Baba Yangu..wewe ndiyo unapaswa kuwajibika…amka!”Nikaamka,Nikatoka nje nikalipia Gari lililokuwa limechukua miili ya marehemu.

Kwa Namna Fulani nilimudu hali hiyo mpaka mazishi yakaisha,mara nyingi nilitaka kuanguka,John alikuwa amenishikiria mikono yangu.Kila mtu alinitazama kwa Huruma.
Kifo cha cha ndugu zake kimemdhoofisha(walisema)Nilijua mwili wangu ni dhaifu kuliko akili yangu.Taratibu zote zikaisha.nikakamilisha taratibu zote za fedha na kanisa.

Baada ya kufika nyumbani sikuongea na mtu yeyeyote,Nilianguka kitandani nikalala.
“mwache Alale jamani”kila mtu alifikiri hivyo.kwakweli usingizi ule ulikuwa ni zaidi ya kulala.kwa masaa kumi na saba sikujua kinaendelea.Ilikuwa ndoto ya mchana?Hakuna njia sikuona maono yeyote…sikuwa najitambua kwa kitu chochote…..

JE UKIFA UTAENDA WAPI?
Je unafikiriaje kuhusu kifo?je unafikiriaje kuhusu Kifo?Je umejiandaaje kuhusu kifo?Je kifo hakitakuwa kibaya kwako au kitakuwa kinzuri kwako?

Kifo kinatupeleka kwenye uwepo wake wa milele!itakuwa utukufu kiasi gani kuishi katika uwepo wake wa milele!itakuwa utukufu kiasi gani kuishi kwenye uwepo wake milele.Paulo alitamani kuacha mwili wake na kuwa na kristo.Anasema hiyo ni Bora zaidi.[Fil1;23]
“Kama Vile nilivyotazamia sana,na kutumaini,kwamba sitaaibika kamwe Bali kwa uthabiti wote,kama siku zote na sasa hivyohivyo kristo ataadhimishwa kwenye mwili wangu;ikiwa kwa maisha yangu,au ikiwa mauti yangu”.Paulo akasema.alikuwaamesongwa katika hali ya mwili.Kuishi ni KRISTO NA KUFA NI FAIDA……Nichague nini?Sitambui Ninasongwa katika mambo mawili…..”

Je upo upande gani!uchague maisha au Kifo?Bila shaka hakuna uchaguzi katika mambo hayo mawili maana maisha yetu yapo katika yeye…wale waliishi katika kristo ni Faida maana hao wanauzima wa milele. “itamsaidia nini mtu akiupata ulimwengu wote akipata Hasara ya nafsi yake?” mark8;36
Je unachagua Faida au Hasara?haya ni mambo mawili ya kutafakari kulingana na maisha yako,je umeamua kuishi na kristo upate faida hata utakapokufa ? au kuishi maisha ya ulimwengu upate hasara ya nafsi yako? Tafakari

“Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu,Bwana,enendeni vivyo hivyo katika yeye:wenye shina na wenye kujengwa katika Yeye mmefanywa imara kwa imani” kor 2;6-7

Rafiki yangu,uhusiano wako na Yesu unapopewa kipaumbele,anapofanyika msaada wako wakaribu,Hutaogopa chochote.utaegemea kifuani kwake,kifo wala mauti havitakuweka chini.Utakuwa kwenye mikono salama.

Natumaini tunamwomba Yesu kwa ajili ya urafiki wa undani na naye…sasa!
Hebu tumwambie;

Yesu nahitaji kukua katika urafiki usioshindwa na usio na kikomo.Katika maisha na katika kifo na hitaji uwe pamoja nami,nataka nikuone kila wakati maishani mwangu.nataka nikuone nikusikie,na nikuguse kiundani zaidi..sikia maombi yangu eeeeh Bwana,Ameen!!
Sheikh mstaafu.
Mtumishi wa kristo.

No comments:

Post a Comment