Hakuna mageuzi yaliyoubadilisha ulimwengu yaliyotendeka kiajali. Katika baadhi ya mageuzi, yalianza na watu wachache tu waliojadili kuhusu mabadiliko yanayohitajiwa. Iwapo matukio haya ya kihistoria yalizaliwa na ghasia za kawaida au yalipangwa, hayakufanyika tu. Yalifanywa maksudi, kwa kunuiwa, kupendwa na kwa mkakati maalum. Yalianza hivi kwamba mtu fulani alikataa kufanya kitu, mtu fulani “akaachilia mambo yafanyike,” mtu fulani alikataa kusikiza na akapuuza ilhali maovu yalikuwa yamezidi. Mageuzi hutokea kwa sababu mtu fulani huamua kuchukua hatua.
Biblia imejaa maagizo yanayotuhitaji sisi kuyatekeleza. Agizo la kutekeleza badala ya kusikiza ni rahisi, lakini mamilioni ya watu hupuuza. Pengine wanafikiri mambo yatakuwa bora wakijitegemea. Hayawezi. Hakuna kizuri kitendekacho kiajali. Wakati fulani nilijifunza kwamba maisha yangu yamebadilika na kuwa bora. Kutamani kitu hakutoi matokeo tunayotarajia, bali lazima tuwe wakakamavu kufanya kile kinachohitajiwa kufanywa ili kuyapata tuyatakayo. Hatutampata mtu aliyefaulu ambaye katika maisha yake alitarajia kufaulu na hatimaye akafaulu. Vile vile, hatutampata mtu asiyefanya jambo lolote na kisha akafaulu maishani. Mfano huu pia unahusu kuwa sehemu ya Mageuzi ya Upendo.
Ikiwa tunataka kuwapenda watu kama Yesu alivyoagiza, ni lazima tufanye hivyokwa lengo. Haiwezi kutendeka kiajali. Biblia inasema tulitafute lililo jema siku zote (Wathesalonike 1 5:15). Tafuta ni neno lenye nguvu linalomaanisha “matamanio makuu, kimbilia, fuata.” Ikiwa tutatafuta nafasi, tuna hakika tutapata na hilo litatulinda kutokana na kukaa tu bila kufanya kitu na kutozaa matunda. Ni lazima tujiulize ikiwa tuko imara na timamu au kusikiza na kutotekeleza jambo? Mungu yuko imara na timamu! Ninashukuru kwamba Yeye yuko, lau sivyo mambo katika maisha yetu yangelizorota haraka.
Mungu hakuumba tu ulimwengu na kila kitu tunachokiona na kufurahia ndani yake, Yeye pia anaendelea kuudumisha kwa sababu anajua kwamba mambo mazuri hayatokei kiholela, yanatokea kutokana na matendo yafaayo (Waebrania 1:3). Matendo yanayoongozwa na Mungu yanatuweka kuwa mbali na hali ya kutokuwa na lakufanya na kutozaa matunda na hivyo basi kuwa kama kinga kwetu. Kuwa imara kufanya mambo yafaayo kutatuzuia kufanya mambo mabaya. Inaonekana hatuhitaji kujaribu kwa bidii kufanya kile ambacho ni makosa; maumbile yetu hufuata mwelekeo huu ikiwa hatutachagua kile ambacho ni sawa kufanya. Kwa mfano, hatuchagui ugonjwa, kile tunachofaa kufanya ni kuwa karibu nao na tutaweza kuambukizwa. Lakini ni lazima tuchague afya. Kuwa na afya, lazima kila mara nifanye uchaguzi bora kuhusu mazoezi, usingizi, na lishe. Lazima nichague kutokuwa na mawazo ya kunitia wasi wasi au kuwa na hamaki kwa sababu najua kufanya hivyo kutanifanya nihisi uchovu na pengine kusababisha dalili nyingine zinazoonekana. Kuwa na afya, lazima niwekeze vilivyo katika afya yangu, lakini ninaweza kuwa mgonjwa kwa urahisi kwa kutofanya kitu ili kujitunza.
No comments:
Post a Comment