Monday, 4 June 2018

KUPATA UPONYAJI  KUTOKA KWA PIGO AU MSIBA

 
“Roho wa Bwana yu juu yangu,  kwani amenipaka mafuta niwahubirie maskini  Habari  Njema.  Amenituma niwatangazie mateka watapata uhuru,  vipofu watapata kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa. Luka 4:18 

Haijalishi kilichotokea katika maisha  yako kusababisha huzuni na upweke, unaweza kuwa na uhakika kwamba Mungu atakuongoza  katika  kupokea uponyaji wako. Naye atakuonyesha wakati ambapo utakuwa  unakubalia hisia zako kwenda mrama au kupoteza usawa wako - iwapo utakubali kumsikiza Roho wake. Haiwezekani kwetu kukadiria kiasi cha wakati ambao unafaa kutumika katika kuomboleza kwa sababu hali na watu ni tofauti. Lakini, hata kama itachukua muda mrefu kiasi gani, kutakuwa na wakati ambapo Bwana atasema,  “Sasa ni wakati  wako  wa kuamka na uendelee mbele. Ni lazima  uachane na hayo ya kale nawe  umalize mbio  ambayo  nimekuwekea katika  maisha  yako. 



Sitakuacha,  wala sitakupungukia, hivyo kuwa shujaa na hodari, na usonge mbele!” Kila Tukio ni Tofauti Kwa kawaida, miezi sita ya  kwanza wakati  wa kuomboleza ndio muda mgumu kabisa. Muda huu unaweza kupita au kupungua miezi sita kulingana na hali ya mambo. Kuna mambo tofauti katika kila msiba ambayo ni tofauti kwa kila moja.

Ughafla  wa  msiba  au  ajali.  Mtu  akiwa  mgonjwa  kwa  muda mrefu, jamii inaweza kuwa imeanza kujitayarisha katika nia na mawazo yao kwa kifo cha mpendwa wao. Iwapo kifo ni cha  ghafla  na  hakikutarajiwa,  basi  pigo  linaweza  kuwa  kubwa zaidi na gumu kukabiliana nalo. 

Uwepo  au ukosefu wa jamii  kukufariji. Kwa mfano,  ikiwa mme au mke amekufa, inakuwa afadhali ikiwa kuna watoto walioachwa ambao wanaweza kumfariji mzazi aliyeachwa. Iwapo mtoto amekufa, basi watoto wengine  wanaweza kusaidia kujaza pengo aliloacha. Hali ya uhusiano kati  ya mwenye kufa na aliyeachwa. Ikiwa uhusiano ulikuwa mwema na wa karibu, basi kipindi cha kuomboleza kinaweza kuwa kirefu na kigumu kuliko kama uhusiano haukuwa wa kuridhisha sana. 

Utu wa mwenye kuachwa. Hii ni kweli hasa wakati mke au mume anaachwa na mwenzi wake. Watu wengine huwategemea wengine sana  na hii huwachukua muda  mrefu zaidi kuchukua uongozi na kuendelea na maisha. 

Kina cha uhusiano kati ya mwenye kuomboleza na  Yesu Kristo. Hili ni jambo la msingi.  Mara  nyingi, msiba  au ajali huwafanya watu waanze kutafuta uhusiano na Bwana, ambao huleta faraja. Lakini mtu ambaye tayari anamjua Bwana, “na nguvu  za  ufufuo  wake”  (Wafilipi  3:10),  kwa  kawaida  hupata uponyaji wa haraka kuliko  mtu ambaye hakuwa na uhusiano na Bwana au ambaye uhusiano wake naye ulikuwa wa juu juu tu. Kama mfano wa kukueleza ninachomaanisha  kuhusu vipindi tofauti  vya kuponywa  kutokana  na msiba. 

Ningependa  kushiriki nawe mifano miwili ambayo ninaijua mimi mwenyewe.
Mfano wa kwanza: Ninamjua mwanamke mmoja  Mkristo ambaye alikuwa na uhusiano wa karibu  na Bwana na kutembea  naye  kwa miaka mingi. Walikuwa wameoana na mumewe kwa muda  wa miaka ishirini na tano au zaidi. Ingawa mumewe  alikuwa Mkristo, hakuonyesha matunda yoyote katika  uhusiano wake na Bwana.  Yeye hakumtendea mke wake mema, na hii ilikuwa imeendelea  kwa muda wa miaka mingi. Mtu huyu aliiweka biashara yake mbele ya kitu kingine chochote. 

Alikuwa mchoyo na mwenye kujipenda kiasi cha hata kumdhulumu mke wake na kukataa kumtimizia mahitaji yake. Mwanamke huyu alipokuwa anaendelea kutembea na Bwana, Mungu alimpa ombi maaulum  kwa ajili ya mume  wake, alimwonya kuwa iwapo hangetubu na kumgeukia Mungu, basi angekufa baada ya miezi sita. Mwanamke yule  aliendelea kuomba,  naye  mume akaendelea kupuuza maonyo  na mwito wa Bwana.  Kwa sababu ya ukaidi wake, alimfungulia shetani mlango naye akayafupisha maisha yake. Mtu huyo aliishia kufa kutokana na mshituko wa moyo. Ingawa  kifo chake  kilikuwa jambo  gumu  kwa mkewe,  haingeweza kulinganishwa na mtu aliyekuwa na uhusiano mwema na mumewe.  Mungu alikuwa amemuonya mwanamke  huyu, na hii ilikuwa imemtayarisha. Niligundua kuwa wakati aliochukua  kupokea uponyaji ulikuwa mfupi sana. Kulikuwa na mambo ambayo ilimbidi ashughulikie - mambo  ya kifedha  na  kadhalika  –  lakini ilimchukua  muda  mfupi kuweza kuanza maisha mapya. 

Mfano wa pili:
Mfano  wa pili unamhusisha  shangazi yangu.  Yeye na mjomba wangu walikuwa wamejuana  wakiwa wangali watoto na walifunga  ndoa shangazi yangu alipokuwa na miaka kumi na mitano naye mjomba akiwa na miaka michache kumliko yeye. Katika siku za kukua kwake, shangazi yangu hakuwahi kuwa na mchumba mwingine au kufanya urafiki na mvulana mwingine.Walikuwa hawawezi kupata watoto, na hii iliwaleta karibu sana. Walifanya  kazi  pamoja katika  kiwanda chao cha kuoka  mikate kwa zaidi ya miaka thelathini. Walifanya kila kitu pamoja, wakimtumikia Mungu kama wenzi.

Wote walikuwa wamepitia magonjwa  pamoja  mara  nyingi katika maisha yao na walitumia muda mwingi wakitunzana.  Wakati mwingine, watu wanapokuwa pamoja  na kusaidiana kwa muda mrefu, ndivyo wanavyoendelea kuwa marafiki wa karibu. Walikuwa na uhusiano  wa  kina  kati yao. Walikuwa wanaambatana kama chanda na pete. Walikuwa na nyakati za kufurahia pamoja: wakivua samaki, kupika, kuenda kanisani pamoja, n.k. Ingawa mjomba alikuwa  ameugua kwa muda mrefu, kifo chake kilikuwa  ni pigo kubwa  sana kwa shangazi yangu.  Wakati  huo shangazi alikuwa amelemazwa  na ugonjwa wa kuugua mifupa katika magoti yake lakini hangeweza kufanyiwa upasuaji kwa sababu aalikuwa anugua maradhi ya moyo pia. Kwa sababu hii, ilimbidi  aendelee  kukaa nyumbani peke yake kwa miaka  mingi baada ya kifo cha mumewe na hii iliongeze uzito kwa msiba ule.   Kwa sababu ya hali hii ngumu, uponyaji wake ulichukua miaka kadhaa.
Kuomboleza ni Jambo la Kawaida, Kuishi Ukiwa na Maombolezo si Vyema Kutokana na mifano hii miwili, tunaweza kuona jinsi hali moja ya msiba  inaweza  kuwaathiri watu wawili  kwa njia  tofauti sana. Ingawa hatuwezi kusema kwa hakika muda wa kuomboleza unafaa  kuwa urefu  upi,  ni  muhimu  kwa mwenye  kuomboleza apige hatua kuelekea uponyaji. Mara  ya kwanza, inaweza kuwa vigumu kupiga hatua hizo, lakini ni muhimu  kwamba hata kama ni baada ya muda,  mabadiliko thabiti  yaanze  kuonekana. Kama kidonda kinachopona, mtu anaweza kuhisi uchungu kwa muda mrefu, lakini uponyaji kamili huendelea kuja siku hadi siku. Wakati kidonda  kinapokataa kupona, basi hii huashiria kwamba kuna kitu ambacho kinahitaji kuponywa  kabisa kwanza. Ninaamini ya kuwa hivyo pia ndivyo ilivyo na vidonda  katika hisia na nafsi zetu. Nia na hisia zetu zinahitaji  kupona kama vile sehemu za miili yetu. Mungu alitupatia  hisia kama vile alivyotupatia  miili. Amekutana na mahitaji ya uponyaji wa hisia zetu na pia uponyaji wa miili yetu ndani ya  Yesu Kristo. Hii ni haki yetu kama Wakristo.

Usiamini  uongo wa  shetani.  Atajaribu kukuambia kwamba hutawahi kuushinda uchungu, hutawahi kuwa mzima  tena katika hisia zako. Ingawa ni kweli kwamba pengine utaendelea kumkosa mtu  au  kitu ambacho  umepoteza,  hiyo haimaanishi  kuwa utaishi chini ya huzuni na upweke milele. Baada ya muda, huzuni inafaa kuisha nawe uweze kuingia katika msimu mpya maishani mwako. Iwapo mabadiliko haya hayafanyiki katika muda ulio sawa, hii ni ishara ya kwamba pengine  kuna shida mahali fulani: pengine  una nia mbaya, unakataa  kuukubali ukweli,  au pengine  una hofu kuu ambayo haistahili kuwepo. Ukitumia muda kulitafakari neno na kumtafakari Mungu, haijalishi shida yako  ni ipi,  Mungu atakuonyesha  na kukufunulia mzizi wa shida hiyo.
Usisahau kuwa kuomboleza ni hali ya kawaida, lakini kuishi na roho ya huzuni si vyema.

No comments:

Post a Comment