Rafiki yangu mmoja alikuwa akiongea nami kuhusu mwanaume mmoja kijana katika kanisa lake ambaye alikuwa na meno yaliyokaa vibaya. Yalikuwa yamekaa vibaya hivi kwamba alikataa kutabasamu kwa sababu alifedheheka wakati mtu yeyote alipoyaona. Kiukweli Nilimhurumia wakati niliposikia hadithi yake na sikuweza cha kufanya.
Ni mara ngapi tunaposikia kuhusu kitu kama hicho, tunaposikia huruma na kisha tukaondoka bila hata kufikiria iwapo au la twaweza kufanya kitu cha kusaidia? Nafikiri si mara nyingi. Twahitaji kuelimishwa na kufunzwa mara kwa mara. Twahitaji kubuni tabia mpya. Badala ya kudhani kuwa hakuna kitu tunachoweza kufanya, twapaswa kufikiri kuhusu hali hiyo. Kumbuka, Waraka wa kwanza wa Yohana 3:17 inasema: “Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje Ndani yake huyo?.
Kila wakati tunapofanya jambo la kuimarisha maisha ya mtu mwingine au kupinga maovu, twapeleka tumaini katika kile kinachoonekana kuwa jamii iliyokosa tumaini. Twaweza kushinda uovu kwa wema, kwa hiyo tusichoke katika ari yetu ya kufanya hivyo..
Mtumishi.
Jimmy J.
Jimmy J.
No comments:
Post a Comment