Tuesday, 19 June 2018

Uko Hai au Umekufa...??

Mungu alimwambia  Adamu kwamba ikiwa angalikula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya  basi hakika atakufa. (Mwanzo 2:17.)
Alimaanisha watakufa ndani sio miili yao.  Alimaanisha uhai ulio ndani yao utakufa. Nuru itaondoka  na watakuwa giza.

Hivi majuzi mtu mmoja aliyeishi maisha ya uovu mwingi alikuwa anafanyiwa upasuaji. Alidhani atakufa, na alitaka kulainisha maisha yake na Mungu. Tulipokuwa tukizungumza naye mimi pamoja na Chris rafiki yangu, alisema “Nahisi nimekufa ndani.” Hebu litafakari jambo hili. Alitaka kuzaliwa mara ya pili kwa sababu alikuwa anahofu atakufa kimwili akiwa angali anafanyiwa upasuaji hata ingawa ukweli ni kwamba alikuwa mfu ndani yake maisha yake yote, na aliyakiri hayo kwa kinywa chake mwenyewe.

Je uko hai au umekufa?
Nyoka  alimdanganya Hawa. Alisema “hakika hamtakufa” (Mwanzo 3:4). Kile alichosema kilikuwa kinyume na kile Mungu alikuwa amesema; hivyo basi, ilikuwa ni uongo. Neno la Mungu ni kweli.
Na hapa mwanzo unaona asili ya Shetani. Yeye ni kinyume na yote yaliyo ya Mungu. Mungu anataka wewe uwe na yale mazuri. Shetani anataka kukuharibu.  Hata wakati huu hutekeleza haya kupitia uongo na udanganyifu, sawa na jinsi alivyomfanyia Hawa.
Aliendelea kumlaghai na kumdanganya na kumuuliza maswali ambayo yalimfanya aanze kufikiria  (“fikira” ambazo zinajiinua kinyume cha ukweli wa Mungu). Hatimaye alikubali ushauri wa Ibilisi na  kumshawishi mumewe kufanya vivyo hivyo. Wote wakamuasi Mungu kwa kula tunda ambalo alikuwa amewaagiza wasile.

Matokeo yake yalikuwa jinsi Mungu alikuwa amesema- walikufa kiroho. Mungu alipokuja tena katika bustani ya Edeni kuwatembelea Adamu na Hawa, walijifi cha kwa sababu walikuwa wameogopa.
*Je umekuwa ukijificha kumkwepa Mungu kwa sababu ya uoga?*
Mara tu Mungu alipogundua wanaogopa,  Alitambua kwamba walikuwa wamefanya dhambi.  Walikuwa wameamini uongo wa Shetani. 
Walikuwa wamejaribiwa na kuanguka na sasa walikuwa wamepata matokeo ya kile walichokuwa wamechagua.  ```Woga unatokana na dhambi; ni tunda la dhambi.```
Unaweza kuwa na matokeo ya chaguo lako. Lakini Kumbuka, baadhi ya matokeo hayo ni machungu kinywani mwako! Mungu alianza kukabiliana nao kuhusu dhambi yao, lakini pia papo hapo alikuwa na mpango wa ukombozi na wokovu wao kutokana na hali waliyojikuta wameingia.

Katika Mwanzo 3:15, Mungu alimwambia nyoka kwamba uzao wa mwanamke (mbegu yake)  utaponda kichwa chake, naye (Shetani) ataponda kisigino cha uzao wa mwanamke. Mungu alikuwa akizungumza kuhusu  Yesu, Mwanaye wa pekee ambaye alikuwa tayari anaishi katika ulimwengu wa Roho. Mungu ni wa utatu.
Huwa tunamtaja kama “Utatu”: Mungu mmoja katika watatu - yaani Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Kila mmoja wa utatu ana jukumu muhimu la kutekeleza maishani mwako.

Tayari  Yesu alikuwa anaishi katika ulimwengu wa kiroho, lakini ili kumsaidia mwanadamu kutokana na hali yake mbaya, ilibidi Yesu aje duniani.Ilimbidi aingie katika mwili wa binadamu, mwili kama wako na wangu.  Alihitaji ajinyenyekeze na kuwa binadamu. Kumbuka  Yesu ni Mungu kikamilifu, Mwana wa Mungu.  Kwa usemi mwingine  yeye ni Mungu halisi kutoka kwa Mungu halisi. Alikuwa  Mungu na anabaki kuwa Mungu hata sasa. Mpango ulibuniwa, lakini usingaliweza kutimizwa hadi kufi kia wakati kamili wa Mungu,  kulingana na mpango wake kuhusu mambo yote. 

Waefeso 3:10 (Tafsiri ya  AMPLIFIED) inadhihirisha kusudi la Mungu, ambalo ni kwamba sasa, kwa njia ya kanisa  (1), hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi na  ya sehemu nyingi tofauti isiyoweza kuhesabika ijulikane kwa falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho wa mapepo na mtawala wao Ibilisi, ambaye aliasi.

Kwa lugha rahisi,  tuko vitani- vita kati ya Shetani na Mungu! Tayari imekwisha thibitishwa, na tangu jadi, imethibitishwa ni nani atakeyeshinda vita hivyo. Ni Mungu atashinda. Sherehe ya ushindi imepangwa.

No comments:

Post a Comment