Hili ni swali la muhimu la kujiuliza ili kuondoa shaka mioyoni mwetu,kwa kuwa tunatofautiana uelewa wa mambo mbalimbali kama wanadamu basi yatupasa kusaidia pale tu mtu mwingine anapotatizwa na jambo ambalo liko mbele yake.kwakuwa huwa sipendi kukaa kimya, maana ukimya ni ishara ya ujinga na kutofikia kusudi,lazima nijifunze mambo kadhaa wa kadhaa kuhusu uislam ili nielewe ni wapi sahihi au ni wapi si sahihi?
Mara nyingi uislam umekuwa ukijidandiadandia na kujishikisha pale pasiposhikika na jambo moja dhairi ni kwamba hakuna majibu sahihi unaweza kuyapata toka kwa muislam mara zote hujitaidi kumtetea Allah bila udhibitisho wowote,mambo mengi huwa yanapingana yenyewe ndyo maana Allah anaomba msaada kwa viumbe wake…. Sura Muhammad 47:7Kama mkimsaidia Allah, yeye naye atawasaidia na kuwafanya kuwa imara.Hili jambo linampa Allah udhaifu kwasababu anaomba msaada kwa viumbe wake.
Kama waislam wanavyojaribu kutuaminisha kwamba manabii wote walikuwa waislam ,wakiwemo Musa,Elia,Suleiman nk..lakini sishangai kusema kwamba manabii hao ambao wapo katika uislam ni tofauti na manabii ambao wapo katika Biblia,ingawa waislam hujitahidi kujipakazia kwenye Biblia lakini jambo hilo ni dhahiri kwamba kuna vioja vingi ambavyo vipo kwenye uislam ambavyo vinatofautiana na Biblia,walichokifanya ni kukopia majina tu lakini hadithi ni Tofauti,swali la kujiuliza je uislam si umekuja kupotosha ulimwengu katika ile kweli?
Elimu ya malaika ni jambo gumu kwa uislam na mtume Muhammad ndio maana anasema punda anapolia basi kamuona malaika,waislam wanaamini Mussa alimtwanga maliaka wa mauti na kumtoa jicho.SAHIH BUKHARI, HADITHI 1339] inamuonesha Malaika wa mauti akimlalamikia Mwenyezi Mungu: “Umenituma kwa mja asietaka kufa” Abu Huraira anasema Mwenyezi Mungu alimtuma malaika wa Mauti kuchukua nafsi ya Mussa.Mussa akampiga ngumi ikamtoa Jicho.malaika karudi kwa Mungu kamwambia;umenituma kwa mja wako ambae hataki kufa sasa kanipiga ngumi kanitoa jicho lake mahala pake,Mungu akampa pole na kurudisha jicho mahali pake….sahihi Bukhari,hadithi 1339
Maswali ya kujiuliza.
Je kuna watu wanaotaka kufa na wasiotaka kufa?
Je malaika anaweza pigwa ngumi na binadamu na kutolewa jicho??
Je hii siyo dalili ya udhaifu wa Allah na malaika zake?
Kama niliposema hapo awali kuwa waislam pamoja na Muhammad hawana elimu ya kweli kuhusu malaika,jambo ambalo linawatatiza sana,kimsingi ukweli wa mambo yote upo kwenye Biblia ambao unatuonyesha uwezo wa Mungu na jeshi lake la mbinguni.kwakuwa waislam na Allah hawana elimu juu ya malaika inatulazimu sisi wakristo kuwafundisha kwa kina juu ya jambo Hili.
Je hii siyo dalili ya udhaifu wa Allah na malaika zake?
Kama niliposema hapo awali kuwa waislam pamoja na Muhammad hawana elimu ya kweli kuhusu malaika,jambo ambalo linawatatiza sana,kimsingi ukweli wa mambo yote upo kwenye Biblia ambao unatuonyesha uwezo wa Mungu na jeshi lake la mbinguni.kwakuwa waislam na Allah hawana elimu juu ya malaika inatulazimu sisi wakristo kuwafundisha kwa kina juu ya jambo Hili.
MALAIKA WA MAUTI NI NANI?
Kwa mujibu wa Biblia malaika hawa Huitwa “Muharabu” destroyer au Malaika wa mauti kama wanavyowaita waislam 1Koritho 10; 10 malaika huyu hushughulika maalumu na kusababisha maafa pale watu wanapokuwa wameasi Hesabu 16; 41-49, ni wazi kuwa huyu ni mjumbe wa Mungu kwa sababu maalumu za hukumu mara nyingi hutumia tauni katika kuangamiza kama ilivyokuwa kwa mapigo ya tauni za aina mbalimbali katika mapigo yale kumi kule Misri Kutoka 10; 12-13 niliaminilo ni hili ingawa Bwana anasema maana nitapita....
Bwana anazungunza kuwa atapita na kuipiga Misri, je unafikiri Bwana ndiye aliyekuwa anapita Hapana ni Malaika wake maalumu wa kushughulika na hukumu alipita akiwa ametumwa na Bwana,Mara nyingi Mungu anaporuhusu hukumu huhesabika moja kwa moja kuwa ni yeye anayehusika kuleta tauni au mapigo kwa sababu yeye ndiye ameruhusu lakini ni muhimu kufahamu kuwa malaika wake hushika Upanga na kuanza kupiga kwa Tauni ona mfano 1Nyakati 21: 14-22 Mstari wa 15 unaonyesha kuwa Bwana alituma malaika wake na jina la malaika huyu ni Aharibuye (Auaye) malaika huyu hutenda kazi ya kuua anapotumwa na mara nyingi mapigo yake huzimwa kwa sadaka aidha ya kuteketeza au uvumba wa chetezo
malaika huyu ndipo hasira yake hupoa, kwa namna Fulani malaika huyu huweza kutumiwa kwa mauaji kama wa upande wa shetani wanavyomtumia jinni makata.huenda mwandishi wa Zaburi ya 35 ambaye ni Daudi alikuwa akiomba kwa Bwana malaika wa aina hii awashughulikie adui zake Zaburi 35;1-28 mstari wa 8 kuna neno “Uharibifu na umpate” ni wazi kuwa muomaji anaomba malaika huyu wa kuharibu alete uharibifu dhidi ya adui, katika mazingira Fulani ni ruhusa kuwatumia aku kumtumia malaika huyu wa kuharibu na kusababisha uharibifu dhidi ya yale yaliyo kinyume nasi, kuna uwezekano mkubwa kuwa malaika huyu alitumiwa na Eliya kushusha moto kutoka mbinguni na kuharibu vikosi viwili vya maakida waliomuita bila nidhamu 2Wafalme 1;9-15 ni wazi kuwa hatimaye malaika huyo alimsihi Eliya kukubali ombi la Akida wa tatu kwa sababu alikuja kwa unyenyekevu. Malaika wana nguvu za kupita kawaida lakini sio wenye nguvu zote nguvu zao zinazidi zile za kibinadamu Zaburi 103;20Kwahiyo mwanadamu hana uwezo wa kumtwanga malaika paka kumtoa jicho kama waislam wanavyoamini.
MASWALI YANGU KWAKO MUISLAM
Je ni kweli binadamu huamua kufa au kutokufa?
Malaika wa mauti aliyetumwa na Allah alikuwa na umbo gani paka kupigwa na kutolewa Jicho?
Je malaika wa mauti huja kwa kila mtu au kwa Yule mkosaji tu??
Kwanini Mussa alimtwanga malaika wa mauti kiasi kile na kumtoa jicho?
Malaika wa mauti aliyetumwa na Allah alikuwa na umbo gani paka kupigwa na kutolewa Jicho?
Je malaika wa mauti huja kwa kila mtu au kwa Yule mkosaji tu??
Kwanini Mussa alimtwanga malaika wa mauti kiasi kile na kumtoa jicho?
Ukishindwa kujibu maswali haya basi usishupaze shingo kuja kwa Yesu upate uzima wa milele.
Sheikh mstaafu.
No comments:
Post a Comment