Tuesday, 10 October 2017

TAHADHARI ZA MKRISTO NA MTUMISHI


Mara nyingi tumejifunza kutoogopa chochote kwa sababu ya Biblia inasema mara365 kwamba tusiogope.Ni vema kutoogopa kwasababu Hofu ni aduii muhimu wa Imani.lakini katika Imani tahadhari ni muhimu kwa sababu kuishi bila tahadhari unaweza kuishi bila Utaratibu.Nakuishi Bila utaratibu kunaweza kutupeleka kwenye Uharibifu.Ndio maana Yesu alisema Jiangalieni na pia akasema jilindeni na choyo,kwahyo kujiangalia na kujilinda ni Muhimu.

Katika maisha ya kila siku yapo mambo ya kupambana nayo na yapo mambo ya kuepuka na yapo ya kukimbia.Neno usiogope kupambana na pia usiogope kuepuka inapobidi kuepuka usione aibu ukajiingiza kwenye mtego ulio peupe usiogope kuepuka linapotokea jambo lipasalo kupambana kwa maombi na kwa namna iliyosahihi usiogope kupambana.Na likitokea jambo la Hatari ya kimwili Na kiroho na unaona njia ya kuepuka ni kukimbia.wala usiogope kukimbia,kumbuka Yusuph alipokaribiliwana dhambi ya kufanya zinaa ilimbidi kukimbia.wala hakuogopa kukimbia zinaa,Ujasiri kwenye dhambi ni Ujasiri wa kipumbavu.

Kwahiyo naposema mambo yatupasayo kuogopa maana yake ni kujihadhari na hayo katika maisha Yetu ya Ukristo na Utumishi.Tuingie kwenye uchambuzi Hakinifu juu ya hizo Tahadhari za mristo na mtumishi.

1.Tahadhari ya kwanza ya mkristo na mtumishi ni kuogopa kuwa na Jina la kuwa Hai wakati umekufa kiroho,kufa kiroho ni kupotezaa uhusiano mnzuri na Mungu wako na kubaki na kiini macho cha ukristo bandia sio na kiinii cha Uzima.na watumishi hawa utumika kuwapendeza watu wanao watazama Badala ya Kumpendeza Mungu wako aliyekuokoa na kukuita katika utumishi.Unabaki unamtumikia Mungu na Bila kutumika pamoja na Mungu,Rum8;28,ukishafeli eneo hilo unaishia kuwa mtu wa watu badala ya kuwa mtu wa Mungu,Hilo mimi nimeona ni jambo la kuepuka na kukimbia.Ufunuo3;1

2.Jambo la pili la kuogopesha mkristo na mtumishi ni Kule kuhubiri wengine Baadaye ukawa Mtu wa kukataliwa na Mungu.Angalizo kwa mtumishi ni Hili,mtumishi wa Mungu Hatakiwi kujivunia Huduma au karama Hata kama ungekuwa mtu unayetumiwa sana na Mungu.usisahau ya kuwa Huduma hiyo siyo ya kwako,ni Ya Mungu amekuwekea cha kuzingatia ni unyenyekevu kwa kadri unavyozidi kujinyekesha Mbele za Mungu ndio Mungu anazidi kukuinua kutoka imani hata Imani na utukufu hadi Utukufu,siyo wewe utayejiinua ila Mungu atakaye kuinua.asilimia za unyenyekevu ndio zitakazozaa asilimia za kuinuliwa kwako.1kor9;27 kumbuka utukufu wa Mungu hauna mwisho.Hapo ulipofika siyo mwisho,ukajiona umefika juu sana ukazembea kumrudishia Mungu utukufu wake katika kila jambo ambalo anakutumia kwalo.Hapo ndipo utajikuta unaanza kupoteza ushirika na Mungu.Ni jambo la kutisha sana kutenda mengi sana kwa ajili ya Mungu halafu Mungu anakuambia sikujui.HII INATISHA.

3.Mtumishi wa Mungu anapaswa kuishi kwa tahadhari juu ya kufilisika Kiroho na Kihuduma,isharaya ku filisika kiroho na kuhudumia ni kama ifuatavyo;-
-kupoteza Furaha na shauku ya kumtumikia Mungu.
-kuacha Upendo wa kiMungu kwa watu wa Mungu.
-Kujaa chuki na Fitina nakutokuwa na msamaha hata kwa jambo Dogo.
-kujaa Udini na usio wakawaida na kujaa chuki ya kimadhehebu isiyo ya kawaida na pia kujaa ukali hata kwenye mahubiri,uvivu wa kuomba na hata kama ukiomba maombi yako yanakuwa makavu yasiyokuwa na uvuvio,au umande wa Baraka.

4.Tahadhari nyingine Mkristo kuepuka kumwaibisha Yesu ili nayeye asije kukuaibisha mara dufu.Unawezaje kumwaibisha Yesu ni kule kuishi maisha yasiyo na ushuhuda mnzuri katika jamii,ni kumtukanisha Yesu kwa matendo yasiyokuwa ya ukristo.swali la kujiuliza Je Yesu anaweza kuaibika??La Hasha ukimwaibisha Yesu ujue aibu hiyo itakurudia maradufu wewe mwenyewe ..math10;32.

Tafakari
Chukua Hatua..
Itaendelea…

No comments:

Post a Comment