Wakristo wengi wanapenda kuchagua kuhusu ni yupi wanayemsaidia na wanayemtia moyo. Wanawatafuta watu kama wao. Baadhi ya watu hata wanaamini kwamba wanapaswa kuwasaidia watu wengine wanaoamini kile wanachoamini na kufikiria kama wanavyofikiria. Hiyo siyo njia inayopaswa kuwa. Siyo njia Yesu alivyofanya.
Miaka kadhaa iliyopita nilisoma hadithi kuhusu mtu fulani aliyeanguka kwenye shimo na hangeweza kutoka na jinsi watu wengine walivyomhudumia mtu huyo.
Mtu mbaguzi alikuja akasema, “Ninakusikitia huko chini.”
Mtu asiye mbaguzi akaja akasema, “Aha, ni jambo la kueleweka kwamba mtu angelianguka huko chini.”
- Mfarisayo akasema, “Ni watu wabaya wanaoanguka kwenye mashimo.”
- Mtaalam wa hesabu akafanya hesabu jinsi mtu huyo alivyoanguka kwenye shimo hilo.
- Mwandishi wa habari alitaka kupata habari ya kipekee kuhusu mtu huyo katika shimo. Mwanamgambo akasema, “Unastahili shimo lako.”
- Mkristo mmoja akasema, Iwapo ungekuwa umeokoka hungeanguka kwenye shimo hilo.”
- M’Armenia mmoja akasema, “Uliokolewa na bado ukaanguka kwenye shimo hilo.”
- Mtu hodari akasema, “Tubu kwamba humo katika shimo hilo.” Mtu wa kusema yaliyo dhahiri akasema, “sasa hilo ni shimo.”
- Mtaalamu wa Jiolojia akamwambia afurahie mwamba ulioko katika shimo hilo.
- Mfanyikazi wa IRS akamuuliza ikiwa alikuwa akilipa ushuru kwa shimo hilo.
- Mkaguzi wa baraza akamuuliza ikiwa ana kibali cha kuchimba shimo hilo.
- Mtu wa kujihurumia akasema, “Hukuona kitu chochote mpaka ukaona shimo hilo langu.”
- Mdowezi akasema, “Mambo yanaweza kuwa hata mabaya zaidi.” Mtarajia mabaya akasema, “Mambo yatakuwa mabaya zaidi.”
Yesu alipomuona mtu huyo, akaenda hadi chini na akamshika mkono na kumuinua hadi nje ya shimo hilo. Yesu alikuja ili kufa kwa ajili ya watu. Alikuwa na yuko katika kujishughulisha na watu. Na mimi na wewe twahitaji kuwa katika kujishughulisha na watu pia. Kila mara lazima tukumbuke kwamba Mungu anampenda kila mmoja, na twahitaji kuwahudumia wengine kwa njia ambayo Yesu angeliwahudumia. Twahitaji kuwatia moyo ili wawe vile Mungu alivyowaumba kuwa. Ninaamini kwamba kila mmoja anataka kuwa mfariji, na kila mmoja anayemjua Yesu anataka kuwa kama Yesu, hata yule mtu mbaya.
Kwa nini nasema hivyo? Kwa sababu ninaamini kwamba sote twataka kuwa washawishi wema kwa maisha ya wengine. Twataka kuongeza thamani kwa wengine, sio kuchukua kutoka kwao. Kwa hiyo tafadhali niruhusu niwe mfariji wako. Unaweza kuleta tofauti. Unaweza kuongeza thamani kwa wengine. Unaweza kumwakilisha Yesu vyema na siku moja ukasikia maneno, “Vyema sana, vizuri na mtumishi mwaminifu.” Kila mmoja anaweza kuwa mfariji. Si lazima uwe tajiri. Si lazima uwe mwerevu. Si lazima uwe na uhodari wa hali ya juu. Na si lazima uwe navyo vyote. Unahitaji tu kuwajali watu wengine na kuwa tayari kuanza kufanya hivyo. Si lazima ufanye kitu chochote kikubwa au cha kutambulika. Mambo madogo unayoweza kufanya kila siku yana uwezo wa kupata mambo makuu kuliko unavyodhani.
•Shika mtu akifanya kitu fulani kwa njia sawa.
•Mpe mtu fulani sifa ya kweli.
•Msaidie mtu fulani anayehitaji msaada.
•Mpe mtu fulani bega la kuegemea alilie.
*Sherehekea na mtu fulani anayefaulu.
•Mpe mtu fulani tumaini.
Unaweza kufanya hivi. Anza sasa kwa vitendo. Na kumbuka msemo huu ambao ninaupenda sana. “Ninataraji kupitia katika ulimwengu huu lakini mara moja. Jambo zuri lolote ninaloweza kufanya au ukarimu wowote ninaoweza kuonyesha kwa kiumbe chochote, wacha nifanye sasa. Wacha nisitofautiane wala kupuuza, kwani sitapitia haya tena.”
Jimmy J.
#MwanaMageuzi
No comments:
Post a Comment