"Penzi la kweli halikosi mkwarunzo"......utahuzunika Kwa muda gani? Utaishi kwa majuto kwa Muda gani??Mwenzangu Majuto humaliza nguvu." Laiti ninge.....Laiti nisinge.......kamaa inge...."Looh
Tatizo lako si tatizo lako bali mtazamo wako ndio tatizo lako...chanzo cha tatizo ni mtazamo wala si tatizo!!Haijilishi umefanyiwa nini kwenye maisha yako, haijalishi umefanya nini kwenye maisha yako, Ujachelewa kuingia Mwanzo mpya, Ujachelewa kuingia mwanzo mpya tena.Lakini mustakabali wako huna nafasi kwa maisha yako ya kale. "Nimeharibu maisha yangu nami Nitakaa hapa paka Yesu aje anichukue"hapana hatuwezi kufanya hivyo.
Utalia kwa muda gani kwaajili ya maisha yako??Utalia kwa muda gani kwaajili ya Mahusiano yako??Hanifaidii chochote kulilia kitu ambacho huwezi badilisha.Tuwe watu wa sasa. "Leo nina Imani Mungu anaweza shughulikia ya jana na Leo nina Imani Mungu anaweza shughulikia ya Kesho."Nadhani huu ndio mtazamo tunapaswa kuwa nao.
Unaweza Kuwa na afya nzuri, Unaweza kuwa na Pesa, unaweza kuwa na Maisha mazuri...unaweza kuwa na heshima, unaweza kuwa na Mahusiano.Haijalishi ni kiwango kipi ulihuzunishwa hapo awali, unaweza kupenda tena.
Usijitenge tu na kila Mtu kwasababu unaogopa kuvunjwa Moyo.Unajiumiza wewe mwenyewe ikiwa unaishi katika Upweke na kuishi katika Uoga kuweza kuwa na uhusiano na Mtu yeyote na Yamkini naweza kusema kwamba ukijihusisha na watu utavunjwa moyo na tukubali kwamba huo ndio ukweli.Lakini utapona kwasababu Mponyaji anaishi ndani yako... Wafilipi 3 mstari wa 13 Paulo anasema" ndugu usijidhani nafsi yangu kwamba nimekwisha kufika na kulifanya kuwa langu ila natenda neno moja, ni msukumo wangu mmoja........." Unahisi mapenzi yake????? " Nikiyasahau yalio nyuma na nikiyachuchumilia yaliyo Mbele." Ni kama anasema "Ya kale yananifuata na yanajaribu kunishika lakini nachuchumilia, nakaza mwendo ndio ari yangu moja, lengo langu Moja .....Nitaishi maisha ambayo Yesu anataka niishi....Na kusema ukweli hio ndio ari yangu kama mwalimu wa neno.Kusema kweli Nataka nifunze watu jinsi ya kusimama na wamiliki kile Mungu amepanga wamiliki..
Mungu anampango bora Juu ya Maisha yako na huenda Mpango wako wa pili ni bora zaidi kuliko mpango wa kwanza.
No comments:
Post a Comment