Je, Mungu anakuonaje? Anakupenda zaidi ya jinsi unavyoweza kuelewa, na ana mpango mzuri kwa maisha yako. Huko peke yako kwa sababu yuko pamoja nawe wakati wote.
Msamaha wa Mungu ni mkuu kuliko dhambi yoyote uliyotenda. Huruma zake ni mpya kila siku. Mungu amekupa wewe kama muumini, nguvu, na huna haja ya kuishi maisha ya kushindwa.
Mungu aliangalia kila kitu alichokiumba na akasema ni chema sana (Mwanzo 1:31). Wewe ni sehemu ya vitu alivyoumba, wewe ni mzuri sana. Lakini tunaweza kuona vigumu kuamini maneno hayo. Siongei kuhusu mwili wako. Mtume Paulo alisema, “Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema.” (Warumi 7:18). Miili yetu ina kasoro, na sote hufanya makosa. Mungu anaposema “Wewe ni mzuri,” anaongea juu ya kuumbwa upya kwako kwa kiroho!
Maana tu kazi yake [mwenyewe], tuliumbwa katika Kristo Yesu, [tumezaliwa upya] ili tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo. Waefeso 2:10
Ni muhimu sana tukielewa uhalisia wa kuwa kiumbe kipya na tuanze kujitambulisha nao.
Watu wengine hutenda mabaya kwa sababu wanafikiri kwamba ni wabaya—wanaamini ni wabaya. Mara kwa mara watu huishi wakiwa wamekwama katika mtindo mbaya wa maisha kwa sababu hawaamini kwamba wamewekwa huru kupitia Kristo. Wanaangalia jinsi walivyokuwa wakati wote na hawaelewi nguvu halisi za kuzaliwa upya
—Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya (2 Wakorintho 5:17).
Hata ingawa ni vigumu kuelewa na kuamini kweli, Mungu sasa anatuona kuwa watu wenye haki kupitia Yesu.
Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye. 2 Wakorintho 5:21
Mimi kama mtu niliyehisi “nimekosea” katika sehemu kubwa ya maisha yangu, kujifunza kuhusu mafundisho ya haki kupitia Kristo kulikuwa kunaniweka huru ajabu na bado hata sasa kunaniweka huru. Napenda kuwasaidia watu waelewe hili ili waache kujikataa wenyewe kwa sababu wanaona hawawezi kuwa wakamilifu kila siku. Uhusiano wetu mzuri na Mungu hautegemei yale tunayofanya, lakini unategemea aliyofanya Yesu. Tunapojifunza zaidi na zaidi juu ya upendo, kukubalika, na neema ya Mungu, tutatambua kwamba matumaini huwa msaidizi wetu wa wakati wote. Siwezi kukumbuka ni lini mara ya mwisho nilihisi sina matumaini! Tunaweza kujifunza kumtumaini Mungu na kuwa na imani wakati wote kwamba tunakua na kubadilika, Mungu anaona upendo wetu na jinsi tunavyojituma kwake na bado anatuona tuko katika uhusiano mzuri naye.
Kuna tofauti kubwa kati ya wewe ni nani na kile unachofanya. Ndiyo maana ninawahimiza watu watenganishe “nani” na “kufanya.” Wewe ni mwana wa Mungu. Umezaliwa mara ya pili. Umejazwa Roho wake. Badala ya kuangalia mwili wako, pata mtazamo wa Mungu na uangalie roho yako. Jione katika kioo cha Neno la Mungu, na kisha usisimke kuhusu wewe ni nani katika Kristo Yesu. Pia ninakuhimiza pia upate mtazamo wa Mungu katika majaribu yako. Yaone kwa namna ambayo Mungu huyaona. Yeye anayaona kuwa ya muda mfupi tu.
Hakuna tatizo linalodumu milele, kwa hiyo kuwa na matumaini kwa sababu ushindi wako uko karibu kuliko unavyoweza kufikiria. Unapoangalia kwa miwani ya Mungu, itakubidi useme “Hali hii haitadumu milele na nitadumu zaidi ya hali hiyo!
” Unapokuwa mahali pagumu na kila kitu kinakuendea vibaya kiasi kwamba unaona huwezi kuvumilia hata kwa dakika moja zaidi, usikate tamaa kamwe, kwa kuwa hapo ndipo mahali na huo ndio wakati ambao mawimbi yatabadilika. —Harriet Beecher Stowe
Mungu anatamani upitie hali hiyo ukiwa pamoja naye. Tunaweza kuchagua kuendelea mbele au kukata tamaa. Mungu hutupa ahadi yake, lakini ni juu yetu kusimama imara na kusubiri hadi kila dhoruba maishani mwetu iondoke.
Bila shaka Mungu hutusaidia. Hutoa neema yake, nguvu zake, na kututia moyo, lakini, hatimaye, lazima tuamue kukaza mwendo au kukata tamaa. Moja ya faida za majaribu ni kwamba Mungu huyatumia kutuimarisha dhidi ya mambo magumu. Usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia...
Isaya 41:10a Hili ni Andiko zuri sana linalotwambia kwamba hata tunapopitia jambo fulani gumu, Mungu atatenda mema kutokana na hali hiyo. Anafanya mambo mengi, lakini moja ni kwamba anatutia nguvu zaidi. Tunaimarishwa dhidi ya mambo magumu. Kwa maneno mengine, mambo ambayo awali yalituudhi, au kututisha au kututia wasiwasi, hayatatusumbua tena kamwe.
Mtu anayefanya mazoezi kwenye ukumbi wa mazoezi kwa kuinua vitu vizito atatumuka misuli, lakini wakati atakapofikia kiwango fulani, njia pekee ya kupata misuli zaidi ni kuinuia vitu vizito zaidi ya vile vya kwanza. Tunapomwomba Mungu ili atuinue katika sehemu fulani ya maisha yetu, tunaweza kumtarajia Mungu atende kitu ndani yetu kabla hajatufanyia kitu kwa nje.
Huenda tukasema kwamba lazima tuzoee kuinua vitu vizito zaidi katika roho. Kwa mfano, tunaweza kumwomba Mungu ili upendo wetu uongezeke zaidi na zaidi, lakini huenda hiyo inamaanisha kwamba tutakuwa karibu na watu wengi zaidi ambao ni vigumu kuwapenda.
Nakumbuka wakati mmoja nikimwomba Mungu anipe uwezo wa kuwapenda wale wasiopendeka! Baada ya majuma machache, nilimlalamikia Mungu katika maombi juu ya watu washindani niliokutana nao, na akanikumbusha kwamba siwezi kujifunza kuwapenda wasiopendeka ikiwa nitakuwa karibu tu na watu wazuri ambao hawawezi kamwe kuniudhi kwa njia yoyote. Tunapomwomba Mungu ili atutumie katika njia kubwa zaidi, sharti tukumbuke kwamba mtume Paulo alisema kwamba amefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wampingao. (1 Wakorintho 16:9).
Shetani hupinga kitu chochote kizuri. Anachukia ukuaji na maendeleo ya aina yoyote, lakini tukiendelea kusimama imara, Mungu atakukomboa na sambamba na kutukomboa atatusaidia kukua kiroho kupitia mambo hayo magumu. Hiyo haimaanishi kwamba Mungu ndiye mwanzilishi wa matatizo yetu, lakini kwa hakika huyatumia kutusaidia katika njia nyingi.
Wakati upo katikati ya hali inayokupa changamoto au ya kuumiza, jaribu kufikiria yale mazuri yanayoweza kutokana na hali hiyo, badala ya kufikiria jinsi hali hiyo ilivyo ngumu. Wakati sababu ya kuwa na matumaini inapotoweka, endelea kutumaini katika imani, kama alivyofanya Abrahamu. Kutokana mtazamo wa Mungu, mambo mazuri yanatendeka hata wakati unapongoja ushindi wako au ukombozi wako. Unakuwa kiroho, unakua katika subira, unavumilia majaribu, na utakapoyapita hayo utainuliwa. Na unamtukuza Mungu kwa kumpenda kwa njia ile ile utakayompenda wakati hali zako zitakapobadilika.
Majaribu yana thamani. Yanaumiza, lakini yana thamani! Sisi sote huyapitia, lakini si wote wanaoyapitia kwa mafanikio. Mara kwa mara napenda kusema kwamba baada ya majaribu (test), watu wengine hupata ushuhuda (testimony), lakini wengine husalia tu “kuomboleza (moanies).”
No comments:
Post a Comment