Wednesday, 12 September 2018

Wewe Ni Nani: Tai au Ndege Mvumaji?

Makala moja katika jarida la   Reader’s Digest  ilisema: Ndege mvumaji na tai hupaa juu ya majangwa ya mataifa. Kile  ambacho tai  wote  huona ni nyama iliyooza, kwa sababu  hicho  ndicho  wanachotafuta.  Wananawiri  kwa lishe  hiyo.  Lakini  ndege  wavumaji  hupuuza  nyama  ya mizoga  inayonuka. 

Badala  yake, hutafuta  maua  yenye rangi  za  kupendeza  ya  mimea  ya  jangwani.  Tai  huishi kwa  kutegemea  kitu  kilichokuwako  zamani.  Wanaishi kwa  kutegemea  yaliyopita.  Wanajishibisha  kwa  kula wanyama waliokufa na wasiokuwako tena.   Lakini ndege wavumaji  huishi  kwa  kutegemea  kilichoko.  Wanatafuta maisha  mapya.  Wanajishibisha  kwa  vitu  vipya  na  kwa maisha.  


Kila ndege  hupata kile anachotafuta.  Sote hufanya hivyo.2 Tofauti  kati  ya  tai  na ndege  mvumaji ni sawa sana na tofauti iliyoko kati ya wasiwasi na matumaini.  Kama tai, wasiwasi  hula vitu  visivyokuwa  na  uhai:  mtazamo  hasi, kuona  giza  mbele,  hofu,  dukuduku.  Ni njia mbaya ya kuishi,  kutafuta  uendelevu katika  mizoga  na  vitu  vinavyokufa.  

Lakini matumaini  yako tofauti.  Kama  vile  ndege  mvumaji,  matumaini  ni mazuri sana. Matumaini hutafuta  maisha  mapya, hula vitu vipya na ambavyo havijaoza. Kama  mtoto  wa Mungu, ni haki yako kufurahia maisha yako, lakini  ili uweze kufanya hivyo, utahitaji  kuchagua kuwa  na mtazamo chanya, na kutafuta  kile kilicho kipya na ambacho hakijaoza. Kuwa na mtazamo chanya  kunamaanisha  kwamba unajizatiti  kutafuta vitu vizuri. Unaamini na kutafuta  wakati  wote  yale  mambo mazuri ambayo Mungu amekupangia,  si  kutafuta  na kutarajia  janga linalofuata. 

Haitoshi  tu  kuondoa  mtazamo  hasi—huo  ni  mwanzo  tu.  Una fursa ya  kuondoa mtazamo hasi...na kuchukua mtazamo  mpya na mzuri wa maisha! Nakumbuka  wakati  Mungu  alipokuwa  anakabiliana  nami vikali  kuhusu athari  za mtazamo hasi  na kunipa changamoto niache  kuwaza  na  kunena  mambo  mabaya.  Nilifanya  hivyo  kwa miezi michache na nikadhani  ninaendelea  vizuri  sana,  lakini  bado sikuona  mabadiliko  yoyote  mazuri  katika  hali  zangu.    Nilipokuwa nikitafakari hali hiyo, nilihisi  Mungu alikuwa ananionyesha kwamba ingawa nilikuwa  nimepiga hatua  katika kuachana na mtazamo hasi, bado nilikuwa nimeshindwa kuanza mchakato  wa mtazamo chanya. Mungu anataka si tuache tu  kutenda  mambo yasiyo sahihi,  lakini pia anataka tufanye  mambo yaliyo sahihi.  Mtume wewe, lakini mimi afadhali niwe ndege mvumaji kuliko kuwa tai. 

Kuwa na Matumaini!

Ikiwa  umewahi kukabiliana na wasiwasi  au dukuduku  katika maisha yako, huu unaweza  kuwa wakati  wa ushindi  kwako. 

Unaweza  kuamua  kuishi  maisha yako ukiwa umejaa  matumaini katika Mungu, na ukiwa umesisimka  na kuwa na mtazamo chanya juu  ya  mpango  alio  nao  juu  ya  maisha  yako.  Wasiwasi  si  sehemu  ya DNA yako.  Ni  adui  unayeweza  kumshinda  kwa  msaada  wa  Bwana. Wakati  hali  ngumu  zinapoinuka,  huna  haja  ya  kushtuka  na kusambaratika;  unaweza  kujaa  amani  na  utulivu.  Bwana  ndiye Mwamba wako, na atakutia  nanga  ili usiweze  kupeperushwa huku na huko na dhoruba  za maisha. 

Kwa hiyo endelea  mbele  na uwe  na matumaini.  Unaweza kuwa  ndege  mvumaji,  si  tai.  Unaweza kuona mema  katika kila hali  kuliko kuona yale  mabaya.  Ukikumbana  na dhoruba na ule  upepo mkali ukufanye uhisi  woga, usijali...Baba yako wa Mbinguni ndiye rubani wako!

Jimmy J
Mwana Mageuzi.

2 comments: