Makala moja katika jarida la Reader’s Digest ilisema: Ndege mvumaji na tai hupaa juu ya majangwa ya mataifa. Kile ambacho tai wote huona ni nyama iliyooza, kwa sababu hicho ndicho wanachotafuta. Wananawiri kwa lishe hiyo. Lakini ndege wavumaji hupuuza nyama ya mizoga inayonuka.
Badala yake, hutafuta maua yenye rangi za kupendeza ya mimea ya jangwani. Tai huishi kwa kutegemea kitu kilichokuwako zamani. Wanaishi kwa kutegemea yaliyopita. Wanajishibisha kwa kula wanyama waliokufa na wasiokuwako tena. Lakini ndege wavumaji huishi kwa kutegemea kilichoko. Wanatafuta maisha mapya. Wanajishibisha kwa vitu vipya na kwa maisha.
Kila ndege hupata kile anachotafuta. Sote hufanya hivyo.2 Tofauti kati ya tai na ndege mvumaji ni sawa sana na tofauti iliyoko kati ya wasiwasi na matumaini. Kama tai, wasiwasi hula vitu visivyokuwa na uhai: mtazamo hasi, kuona giza mbele, hofu, dukuduku. Ni njia mbaya ya kuishi, kutafuta uendelevu katika mizoga na vitu vinavyokufa.
Lakini matumaini yako tofauti. Kama vile ndege mvumaji, matumaini ni mazuri sana. Matumaini hutafuta maisha mapya, hula vitu vipya na ambavyo havijaoza. Kama mtoto wa Mungu, ni haki yako kufurahia maisha yako, lakini ili uweze kufanya hivyo, utahitaji kuchagua kuwa na mtazamo chanya, na kutafuta kile kilicho kipya na ambacho hakijaoza. Kuwa na mtazamo chanya kunamaanisha kwamba unajizatiti kutafuta vitu vizuri. Unaamini na kutafuta wakati wote yale mambo mazuri ambayo Mungu amekupangia, si kutafuta na kutarajia janga linalofuata.
Haitoshi tu kuondoa mtazamo hasi—huo ni mwanzo tu. Una fursa ya kuondoa mtazamo hasi...na kuchukua mtazamo mpya na mzuri wa maisha! Nakumbuka wakati Mungu alipokuwa anakabiliana nami vikali kuhusu athari za mtazamo hasi na kunipa changamoto niache kuwaza na kunena mambo mabaya. Nilifanya hivyo kwa miezi michache na nikadhani ninaendelea vizuri sana, lakini bado sikuona mabadiliko yoyote mazuri katika hali zangu. Nilipokuwa nikitafakari hali hiyo, nilihisi Mungu alikuwa ananionyesha kwamba ingawa nilikuwa nimepiga hatua katika kuachana na mtazamo hasi, bado nilikuwa nimeshindwa kuanza mchakato wa mtazamo chanya. Mungu anataka si tuache tu kutenda mambo yasiyo sahihi, lakini pia anataka tufanye mambo yaliyo sahihi. Mtume wewe, lakini mimi afadhali niwe ndege mvumaji kuliko kuwa tai.
Kuwa na Matumaini!
Ikiwa umewahi kukabiliana na wasiwasi au dukuduku katika maisha yako, huu unaweza kuwa wakati wa ushindi kwako.
Unaweza kuamua kuishi maisha yako ukiwa umejaa matumaini katika Mungu, na ukiwa umesisimka na kuwa na mtazamo chanya juu ya mpango alio nao juu ya maisha yako. Wasiwasi si sehemu ya DNA yako. Ni adui unayeweza kumshinda kwa msaada wa Bwana. Wakati hali ngumu zinapoinuka, huna haja ya kushtuka na kusambaratika; unaweza kujaa amani na utulivu. Bwana ndiye Mwamba wako, na atakutia nanga ili usiweze kupeperushwa huku na huko na dhoruba za maisha.
Kwa hiyo endelea mbele na uwe na matumaini. Unaweza kuwa ndege mvumaji, si tai. Unaweza kuona mema katika kila hali kuliko kuona yale mabaya. Ukikumbana na dhoruba na ule upepo mkali ukufanye uhisi woga, usijali...Baba yako wa Mbinguni ndiye rubani wako!
Jimmy J
Mwana Mageuzi.
Umenibariki Sana,nimepata mwanga Moya.
ReplyDeleteMwanga mpya
Delete