Wednesday, 17 April 2019

Kuwa na Ndoto juu ya Maisha yako

Muhubiri 5:3 kwa maana ndoto huja kwasababu ya shughuli nyingi....kwasababu baadhi yetu  tunandoto na hatutaki kufanya kazi na wakati mwingine hatuna budi kupitia hali ngumu.

Naamini unapokuwa na ndoto ni kama unapokuwa na ujauzito,kuna wanawake wachache ambao huweza kujifungua bila uchungu lakini si wengi sana.Nafikiri kwamba ukitaka kuzalisha kitu lazima ufahamu kwamba ni zaidi ya kuwa na wazo nzuri,Unakuwa na ndoto,unakuwa na matumaini,unakuwa na mpango lakini lazima uwe tayari kufanya kazi na kupitia yale ambayo unapaswa kupitia ili ndoto yako iweze timia.

Wednesday, 20 March 2019

SAFARI YA MOYO

“Ni nani atakayenitunzia watoto wangu?” analia mama anayekufa, akijua kwamba watoto wake  hivi karibuni watajiunga  na mamilioni ya wengine    kote  duniani  kumtafuta  mama  mpya.  Nimewaona  marafiki wanaougua  saratani  wakilia  maombi  hayo  hayo.  Siwezi  kufikiria  juu  ya afueni kuu ya moyo, au mauguzi makuu yanayosikika nyakati za giza kuu

Nataka  kumpigia  yowe  nimwambie.  “TUTAKUTUNZIA”  Hii  kwa  kweli  ni sehemu  ambayo  twahitaji  kujikakamua,  kuvumilia,  kuomba  na  KUAMINI, na kutoka kwa imani.

Monday, 17 December 2018

Mungu Anakupenda

Usifike mwishoni mwa maisha yako ukiwa umejawa na majuto ya hasara ya maisha yako kwa sababu uliyatumia  kwa. vitu visivyo  na  maaana  kamwe.......

Wakati  ni  karama  ya  ajabu  kutoka  kwa Mungu, na ni muhimu  tuwe waangalifu  sana tunatumia  wakati  wetu kufanya nini.  Wajua, mradi tu tumeshautumia  mda, hatuwezi kuupata tena.  Kuwa na wakati  na Mungu huleta  thawabu  ya ajabu,  lakini  vitu vingine vingi huleta sisimko lisilo na thamani kwa bei ghali.

Monday, 22 October 2018

Barua

Wapendwa wangu Mama na Baba.
    Tangu Niende Chuo kikuu Najua sijachukua Muda wa kuwaandikia na Naomba msamaha kukosa kufikiria kuwaandikia paka sasa.Nitawaeleza Mambo yote katika Barua hii lakini kabla hamjasoma Tafadhali ketini chini,Tafadhali msisome paka Mketi chini.
   Naendelea Vizuri sasa,Jeraha la fuvu la kichwa baada ya kuruka kwa dirisha la Bweni langu Sasa limepona,Niliruka baada ya bweni langu kushika moto muda mfupi.baada ya kuwasili hapa sasa huwa napata maumivu ya kichwa mara moja kwa siku.

Tuesday, 25 September 2018

Mimi ni Mageuzi ya Upendo.

Ninachagua huruma na kusalimisha misamaha yangu. Ninapinga maovu na kujitolea kufanya matendo ya Upendo wa Mungu. Ninakataa kutofanya lolote. Huu ndio uamuzi wangu. MIMI NI MAGEUZI YA UPENDO.- Imani yetu.

Mageuzi ni  jambo la ghafla, kubwa  na lililo  tofauti kabisa na jinsi  mambo yalivyo kama  kawaida.  Mageuzi huchochewa  na mtu mmoja au kundi  dogo sana la watu wasiokubali  kuendelea  kuishi kama  walivyokuwa  siku zilizopita.  Wanaamini  kuwa  lazima  jambo fulani lifanyiwe mabadiliko  na  huendelea  kuimarisha  mawazo yao  hadi pale msingi wao  unapoanzia  na hilo hatimaye huleta mabadiliko kwa njia kubwa.

Wednesday, 12 September 2018

Wewe Ni Nani: Tai au Ndege Mvumaji?

Makala moja katika jarida la   Reader’s Digest  ilisema: Ndege mvumaji na tai hupaa juu ya majangwa ya mataifa. Kile  ambacho tai  wote  huona ni nyama iliyooza, kwa sababu  hicho  ndicho  wanachotafuta.  Wananawiri  kwa lishe  hiyo.  Lakini  ndege  wavumaji  hupuuza  nyama  ya mizoga  inayonuka. 

Badala  yake, hutafuta  maua  yenye rangi  za  kupendeza  ya  mimea  ya  jangwani.  Tai  huishi kwa  kutegemea  kitu  kilichokuwako  zamani.  Wanaishi kwa  kutegemea  yaliyopita.  Wanajishibisha  kwa  kula wanyama waliokufa na wasiokuwako tena.   Lakini ndege wavumaji  huishi  kwa  kutegemea  kilichoko.  Wanatafuta maisha  mapya.  Wanajishibisha  kwa  vitu  vipya  na  kwa maisha.  

Tuesday, 11 September 2018

Mungu Anampenda kila mtu.


Wakristo wengi wanapenda  kuchagua  kuhusu ni yupi wanayemsaidia  na wanayemtia moyo. Wanawatafuta watu kama wao. Baadhi  ya watu hata wanaamini  kwamba  wanapaswa kuwasaidia  watu wengine  wanaoamini  kile wanachoamini  na kufikiria  kama  wanavyofikiria.  Hiyo  siyo  njia    inayopaswa  kuwa. Siyo njia  Yesu alivyofanya. 

Miaka kadhaa iliyopita nilisoma hadithi kuhusu mtu  fulani aliyeanguka  kwenye shimo na hangeweza  kutoka  na jinsi watu wengine walivyomhudumia mtu huyo. 
Mtu mbaguzi alikuja akasema, “Ninakusikitia huko chini.”
Mtu  asiye  mbaguzi  akaja  akasema,  “Aha,  ni  jambo  la  kueleweka kwamba mtu angelianguka huko chini.”

Monday, 10 September 2018

Mpango wa Pili.

"Penzi la kweli halikosi mkwarunzo"......utahuzunika Kwa muda gani? Utaishi kwa majuto kwa Muda gani??Mwenzangu Majuto humaliza nguvu." Laiti ninge.....Laiti nisinge.......kamaa inge...."Looh

Tatizo lako si tatizo lako bali mtazamo wako ndio tatizo lako...chanzo cha tatizo ni mtazamo wala si tatizo!!Haijilishi umefanyiwa nini kwenye maisha yako, haijalishi umefanya nini kwenye maisha yako, Ujachelewa kuingia Mwanzo mpya, Ujachelewa kuingia mwanzo mpya tena.Lakini mustakabali wako huna nafasi kwa maisha yako ya kale. "Nimeharibu maisha yangu nami  Nitakaa hapa paka Yesu aje anichukue"hapana hatuwezi kufanya hivyo.

Sunday, 9 September 2018

Je, Twahitaji Ufufuo au Mageuzi?

Kila mmoja anafikiria juu ya kuubadili ulimwengu, lakini hakuna anayefikiria kujibadili yeye mwenyewe. Jimmy J

Wakati kitu fulani kinapofufuliwa, mambo  ya  zamani  yanaletwa tena kuwa hai, mawazo  mapya yanaletwa  yanaletwa kuwa kitu. Wakati jamii inaposhuhudia  maslahi  mapya  ya  kidini,  huo  huitwa ufufuo. Kamusi ya  MerrianWebster Collegiate inaelezea  ufufuo kama “mkutano wa hisia za juu  sana wa kiinjilisti  au msururu wa  mikutano.”  Katika  maisha  yangu  ya utu uzima kama  Mkristo, nimewasikia  watu wakiongea  kuuhusu  na kuombea ufufuo. Lakini sina  hakika  kwamba  ufufuo  ndio tunaohitaji.  

Tuesday, 4 September 2018

Vaa Miwani Yako Ya Mungu

Natuvae  kile  ninachoita  “Miwani  ya  Mungu,”  ili  tuangalie  mambo fulani  kwa  mtazamo  wa  Mungu.  Yeye  anaona  mambo  kwa  njia tofauti  sana kuliko  tunavyoona kwa sababu anaona mwisho  kutoka mwanzo. 

Je, Mungu anakuonaje? Anakupenda zaidi  ya  jinsi unavyoweza kuelewa,  na ana mpango mzuri kwa maisha yako. Huko  peke yako kwa sababu yuko  pamoja nawe  wakati  wote. 

Msamaha wa Mungu ni mkuu  kuliko  dhambi yoyote  uliyotenda. Huruma zake ni mpya kila siku.  Mungu amekupa wewe  kama muumini, nguvu, na huna haja ya kuishi  maisha ya kushindwa.
Umefanywa  kiumbe kipya kabisa katika Kristo, umepewa maisha  mapya, na unaweza kuyaacha yote  yaliyopita  na utazamie  kwa hamu mambo yaliyo mbele  yako. 

Monday, 3 September 2018

Usingoje Kesho

"....tazama,  wakati  uliokubalika  ndio  sasa;  tazama,  siku ya  wokovu ndiyo sasa.) 2 Wakorintho 6:2 “
Jana ni historia, kesho  ni siri, leo  ni zawadi kutoka kwa Mungu, ndiposa tunaiita present-zawadi.” —Bil Keane

Siku  moja  mwandishi  aliyeitwa  Leo  Buscaglia  alisimulia  hadithi kuhusu  mama yake na kile alichoita “chakula cha jioni  cha familia na cha mateso.” Ulikuwa usiku  ule  wa kwanza baada  ya  baba  yake kurudi nyumbani  na akasema kwamba inaonekana kana kwamba itabidi  afilisike  kwa  sababu  mwenzi  wake  kibiashara  alikuwa ametoroka na pesa  za kampuni.  Mama yake  Buscaglia  alienda kuuza  vito ili anunue chakula kwa  ajili ya karamu ya kukata na shoka.  

Sunday, 2 September 2018

MAGEUZI YA UPENDO

Mageuzi.   Neno lenyewe linaibua  tumaini, linawasha  hamu na kuvutia uaminifu  kama  neno  ambalo halijawahi kupatikana kwenye msamiati wa  binadamu. Katika historia,  wazo  la maguezi limemimina  mafuta kwenye moto na kusisimua ujasiri kwa waliovunjika moyo.

Mageuzi yamewakusanya pamoja  wale wanaotafuta  sababu kubwa  kuliko  wao  wenyewe na  yamewapa wanawake na wanaume waliokosa  mwelekeo hapo  awali, sababu ya kujitoa mhanga.
Wamewazaa  viongozi mashuhuri  na kuwalea wafuasi mashuhuri, wameubadili kabisa ulimwengu. Mageuzi ni  jambo la ghafla, kubwa  na lililo  tofauti kabisa na jinsi  mambo yalivyo kama  kawaida.  

Wednesday, 29 August 2018

Nguvu za Kuendelea Mbele

Nakumbuka  siku  moja  nilipokea  habari  mbaya  sana  muda  mfupi kabla kuaanza kongamano la siku  tatu. Ilikuwa vigumu kuendelea, lakini  nilijua  sina  budi  kuendelea.  Nilihisi  Roho  Mtakatifu  akisema, “Nyanyua  mguu  wako  na  upige  hatua  kwenda  mbele.  Endelea kwenda Mbele!”

Kuendelea  kwenda  mbele  hakukuondoa  uchungu wote  na hali ya kuvunjika  moyo niliyohisi,  lakini  kulinizuia  nisiweze kuzama katika kilindi cha kukata tamaa,  na baada ya majuma machache, hali iliweza kutatuliwa.  Moja ya dalili  za ukomavu  wa kiroho ni kuwa  na nidhamu ya kutimiza ahadi zako, hata ikiwa  unapitia wakati  mgumu.  Nilikuwa  naumia,  lakini  nilihitaji  kuendelea kuwahudumia wengine  waliokuwa wanaumia,  na nilifanya  hivyo, Mungu aliniponya na kusuluhisha tatizo langu.

Thursday, 9 August 2018

Je, Yesu Alikuja kwa ajiri ya Wayahudi Pekee ??

Ndugu   zetu   Waislamu   wanapenda  sana  kudai   kuwa   Yesu   alikuja kwa   ajili   ya  Wayahudi   peke   yao   na   sio   kwa   ajili   ya   ulimwengu  wote.   Na   andiko   wanalolitumia   tena  na  tena  ni   la  Mathayo   15:24  pale  Yesu  alipozungumza   na   mwanamke   Mkananayo:  Akajibu,   akasema,   Sikutumwa   ila   kwa   kondoo   waliopotea   wa  nyumba  ya  Israeli.  

Na   tazama, mwanamke   Mkananayo   wa   mipaka   ile   akatokea,  akampazia   sauti   akisema,   Unirehemu,   Bwana, Mwana  wa  Daudi;  binti   yangu   amepagawa   sana   na   pepo.   Wala   yeye   hakumjibu  neno.   Nao   wanafunzi   wake   wakamwendea,   wakamwomba,  wakisema,   Mwache   aende   zake;   kwa   maana   anapiga   kelele  nyuma   yetu.   Akajibu,   akasema,   Sikutumwa   ila   kwa   kondoo  waliopotea

Sunday, 5 August 2018

Je, Yesu Alikufa...??

Na KWA AJILI YA KUSEMA KWAO MV BUKOBA Ilizama; na kwa hakika MV BUKOBA haikuzama Bali ulizama tu mtumbwi uliofanana na MV BUKOBA na wale wanaosema ilizama wamo katika shaka na jambo hilo la kusema MV BUKOBA alizama mwaka 1996; hawana uhakika isipokuwa wanafuata Dhaka tu. Na wala Meli hii haikuzama Bali mtumbwi unaofanana na MV BUKOBA ndio uliozama. Na kwa yakini MV BUKOBA haikuzama”-Maalim Chaka

Qurani 4:157-158 Suratul An-Nisaa (Wanawake) Na kwa (ajili ya )kusema kwao sisi tumemuua masihi Isa mwana wa Maryamu, mtume wa Mungu. Hali hawakumuua wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa (mtu mwingine wakamdhani nabii Isa.) Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika (hakika)hiyo (ya kumuua nabii Isa) wamo katika shaka nalo (jambo hilo kusema kauwawa]. Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo)hili (la kuwa kweli wamemuua nabii isa) isipokuwa wanafuata dhana tu.Na kwa yakini hawakumuua. Bali mwenyenzi Mungu alimnyanyua kwake. Na mwenyenzi Mungu ni mwenye nguvu (na)mwenye hikima.