Wednesday, 29 August 2018

Nguvu za Kuendelea Mbele

Nakumbuka  siku  moja  nilipokea  habari  mbaya  sana  muda  mfupi kabla kuaanza kongamano la siku  tatu. Ilikuwa vigumu kuendelea, lakini  nilijua  sina  budi  kuendelea.  Nilihisi  Roho  Mtakatifu  akisema, “Nyanyua  mguu  wako  na  upige  hatua  kwenda  mbele.  Endelea kwenda Mbele!”

Kuendelea  kwenda  mbele  hakukuondoa  uchungu wote  na hali ya kuvunjika  moyo niliyohisi,  lakini  kulinizuia  nisiweze kuzama katika kilindi cha kukata tamaa,  na baada ya majuma machache, hali iliweza kutatuliwa.  Moja ya dalili  za ukomavu  wa kiroho ni kuwa  na nidhamu ya kutimiza ahadi zako, hata ikiwa  unapitia wakati  mgumu.  Nilikuwa  naumia,  lakini  nilihitaji  kuendelea kuwahudumia wengine  waliokuwa wanaumia,  na nilifanya  hivyo, Mungu aliniponya na kusuluhisha tatizo langu.

Thursday, 9 August 2018

Je, Yesu Alikuja kwa ajiri ya Wayahudi Pekee ??

Ndugu   zetu   Waislamu   wanapenda  sana  kudai   kuwa   Yesu   alikuja kwa   ajili   ya  Wayahudi   peke   yao   na   sio   kwa   ajili   ya   ulimwengu  wote.   Na   andiko   wanalolitumia   tena  na  tena  ni   la  Mathayo   15:24  pale  Yesu  alipozungumza   na   mwanamke   Mkananayo:  Akajibu,   akasema,   Sikutumwa   ila   kwa   kondoo   waliopotea   wa  nyumba  ya  Israeli.  

Na   tazama, mwanamke   Mkananayo   wa   mipaka   ile   akatokea,  akampazia   sauti   akisema,   Unirehemu,   Bwana, Mwana  wa  Daudi;  binti   yangu   amepagawa   sana   na   pepo.   Wala   yeye   hakumjibu  neno.   Nao   wanafunzi   wake   wakamwendea,   wakamwomba,  wakisema,   Mwache   aende   zake;   kwa   maana   anapiga   kelele  nyuma   yetu.   Akajibu,   akasema,   Sikutumwa   ila   kwa   kondoo  waliopotea

Sunday, 5 August 2018

Je, Yesu Alikufa...??

Na KWA AJILI YA KUSEMA KWAO MV BUKOBA Ilizama; na kwa hakika MV BUKOBA haikuzama Bali ulizama tu mtumbwi uliofanana na MV BUKOBA na wale wanaosema ilizama wamo katika shaka na jambo hilo la kusema MV BUKOBA alizama mwaka 1996; hawana uhakika isipokuwa wanafuata Dhaka tu. Na wala Meli hii haikuzama Bali mtumbwi unaofanana na MV BUKOBA ndio uliozama. Na kwa yakini MV BUKOBA haikuzama”-Maalim Chaka

Qurani 4:157-158 Suratul An-Nisaa (Wanawake) Na kwa (ajili ya )kusema kwao sisi tumemuua masihi Isa mwana wa Maryamu, mtume wa Mungu. Hali hawakumuua wala hawakumsulubu bali walibabaishiwa (mtu mwingine wakamdhani nabii Isa.) Na kwa hakika wale waliokhitalifiana katika (hakika)hiyo (ya kumuua nabii Isa) wamo katika shaka nalo (jambo hilo kusema kauwawa]. Wao (kabisa) hawana yakini juu ya (jambo)hili (la kuwa kweli wamemuua nabii isa) isipokuwa wanafuata dhana tu.Na kwa yakini hawakumuua. Bali mwenyenzi Mungu alimnyanyua kwake. Na mwenyenzi Mungu ni mwenye nguvu (na)mwenye hikima.

Wednesday, 1 August 2018

Amini Kilicho Bora

Nimeokoa  nguvu nyingi  ambayo ingetumiwa na hasira kwa  kusema, “ Ingawa  wanachosema  au kunifanyia huniumiza, nachagua  kuamini  moyo wao  uko sawa.” Naendelea kujiongelesha hadi hisia za  hasira yangu zianze kufifia.  Ninasema mambo kama, Siamini  wanaelewa  jinsi  vitendo  vyao  vinavyoniathiri. Siamini wangejaribu kuniumiza kimakusudi. Hawaelewi jinsi  ninavyojisikia wanaposema hivyo. Pengine  hawahisi vyema kimwili  leo au pengine  wana  tatizo la kibinafsi linalowafanya kutojali jinsi walivyo.”

Ninajua  kutokana  na  ujuzi nilio nao  kwamba  kuweka kumbukumbu za  kimawazo  za  makosa  hutuathiri maisha  yetu na hakumbadilishi mtu mwingine.  Mara  nyingi hupoteza  siku tukiwa tumemkasirikia mtu fulani ambaye hata  hatambui kuwa  alifanya kitu kinachotuudhi.Wanafurahia  siku yao  na  sisi  twaipoteza  yetu. Ikiwa  tutaweka  kumbukumbu hizo,  basi  ni kwanini hatuweki kumbukumbu za  mambo  mazuri  watu  wanayosema  na  kufanya kuliko makosa wanayofanya?

Ikiwa  tunataka  kuwapenda watu, lazima  tumwache  Mungu abadilishe jinsi tunavyofikiri kuhusu watu  na  mambo  wanayofanya. Twaweza  kuamini  mabaya na kushuku  kila kitu watu wengine wafanyacho  na kusema, lakini  upendo  halisi  kila mara unaamini kilicho bora. Kile  tunachofikiria  na kuamini  ni  chaguo. Chanzo cha dhiki yetu nyingi katika maisha ni kuwa hatudhibiti au kunidhamisha mawazo  yetu.  Kwa  kutochagua  kunidhamisha  mawazo  yetu, huwa moja kwa moja twachagua kuamini mabaya ya mtu au kushuku. Nabii Jeremiah aliwauliza watu haya, “Mawazo yako mabaya yatakaa ndani  yako hata lini?  (angalia YER  4:14). Mawazo  waliyochagua kufikiria yalikuwa mabaya kwa Mungu.

Wakati tunapochagua kuamini  kilicho bora,  twaweza  kuacha kila kitu  kiondoke  hasa  kile  ambacho  chaweza kudhuru  uhusiano wetu mzuri.

```Amini Kilicho Bora.```
Mtumishi

Sunday, 29 July 2018

Somo kutoka kwenye Mkahawa

Ninaamini sote  twahitaji  kufikiria makundi ya  kujumuika nayo na kuyapanua.  Twahitaji kuyapanua  vya kutosha ili  kujumuisha watu wa  aina  yote. 

Hivi majuzi nilikuwa na  Rafiki yangu Paul  mwimbaji anayehudumu huko Birmingham, Uingereza, na tulikuwa tukinywa kahawa katika mkahawa mmoja na watu kadhaa. 

Friday, 27 July 2018

Vifungo vya nafsi

Kutumia  muda mwingi pamoja na mtu au kitu  fulani,  huleta uhusiano wa karibu na mtu au kitu hicho. Kama wanadamu, sisi  ni roho, tuna nafsi, na tunaishi katika mwili. Nafsi inaweza kuelezwa kama nia, hisia na hiari yetu. Tunapojihusisha  na mtu au kitu, sisi  hutumia muda  mrefu kumfikiria,  kuwaza  juu  ya  mtu  au  jambo  hilo  na  kufanya  mipango inyayohusu uhusiano huo. Kwa kawaida, mazungumzo yetu huwa juu ya mambo ambayo tunahusika nayo katika  nia zetu, mapendekezo yetu  na hisia zetu. 

Ukiliwazia jambo hili, utaona jinsi ‘nafsi’  zetu zinavyohusika zaidi na watu au vitu tunavyotumia muda na nguvu zetu  kushughulikia. Iwapo mkono wangu ungelifungwa kwenye mwili wangu na kukaa pale kwa muda  wa  miaka  mingi  bila ya kufanya chochote, basi matokeo yanaweza kuwa ya kutisha. Iwapo ungelifunguliwa mara,  basi ungekuwa umenyauka,  bila nguvu, na tena umelemaa. Singeweza kuutumia mpaka uweze kupata nguvu tena na uwezo wa kufanya kazi. Ingenibidi nitafute njia  mpya za kuufanyisha mazoezi ili misuli ambayo imedhoofika iweze kupata nguvu.

Ukahaba wa Vijana

Makala```

Uza mwili  wako ili  kuwafurahisha wanaume waovu  au ufe njaa.  Ni chaguo baya  sana  ambalo  mtu hapaswi kufanya.
Ingawa  ana  umri  wa  miaka  kumi  na tisa,  Suzi amefanya chaguo  hili tangu  akiwa  na  umri wa  miaka  kumi na  minne. Na  kwa  kila chaguo, moyo wake huvunjika  sana  na roho yake inaharibiwa.  Kwa  yote  aliyopitia,  ni miujiza kwamba bado anahisi chochote.

Anapata  nguvu wakati anapoangalia  macho  ya  bintiye wa  umri wa  miezi  saba,  Aamina,  maana  yake ni “salama,” na Suzi ameamua kuwa atafanya chochote  awezacho kuweka ahadi yake ya kumweka binti yake salama. Hauzi mwili  wake kwa  tamaa  au kujifurahisha.  Anauza mwili wake ili aishi. 

Upendo Wajumuisha, Wala Haubagui

Dada aliyefukuzwa kanisani kwa kuvaa vibaya.
" tunavaa vizuri wakati tunapokuja  kanisani hapa  Holiness  Tabernacle. Hakuna jeans, hakuna viatu vya wazi  kama  champali,  na pia unaweza  kufikiria  kuhusu  mtindo  wa  nywele  ambao  si wa  kuvutia sana.  Unajua, switii, kwamba  Yesu  anatufunza tuwe  wanyenyekevu na sio kujivutia sisi  wenyewe. “Akamwonyesha  Jamie  tabasamu ya kejeli na kurudia kumwambia, “Unakaribishwa wakati wowote"

kiwa utawahukumu watu, huna muda wa kuwapenda. Mama Teresa

Jamie aliingia ndani  ya  kanisa kwenye kona  ya barabara ya  Spruce Avenue  na barabara ya  Twenty-Third huko Harbor, Illinois. Alikuwa akitafuta  msaada.  Alikuwa ameliona jengo la kanisa kwa muda mrefu  na aliwatazama watu wakiingia  na kutoka  mara  mbili au mara  tatu kwa  wiki. Jamie mara  nyingi  alikaa  kwenye mkahawa upande  wa  pili  wa  barabara kutoka  kanisa hilo, akinywa  kikombe cha  kahawa,  akishangaa  jinsi anavyoweza  kukubaliwa  ikiwa atakuwa na moyo wa kuingia  katika moja ya ibada za kanisa.

Thursday, 26 July 2018

Matarajio Mapya na Makubwa Zaidi

Tunasema mwanamke mjamzito anatarajia “kujifungua.”  Hivyo huanza kuandaa  mipango  mapema.  Anatenda  sawa  na  matarajio yake—hununua  nguo,  chupa,  kuandaa  chombo  cha  kumlazia mtoto, na kuandaa mahali pa kumweka ili akue.
Tunapaswa kutenda kama watu walio na matarajio. Sharti  tuamke asubuhi na tuandae mipango ili Mungu afanye  kitu cha ajabu. 

Kwa msaada  wa Mungu, tunaweza kuwaza hivi  Huenda leo ndiyo siku. Siku ni hii Bwana  amefanya, na kitu kizuri hakina  budi kutendeka  kwangu .  Hata ikiwa Mungu hatakupa kile kitu ulichokiomba,  jaribu kupanua mtazamo wako. Pengine  unaomba kitu na huku Mungu ana  kitu kingine kizuri  zaidi.  Usiombe  tu  kitu  kizuri;  amini  na  uwe  na  matumaini  ya makubwa zaidi. Amka  kila  siku  na  useme,  “Nina  matarajio  mazuri  na  ya  kwamba  kitu  cha  ajabu  kitatendeka  leo.  

Acha Kuzungumzia Shida Zako

Je,  umewahi  kugundua  kwamba  Yesu  hakuzungumzia  shida zake?  Angeweza  kufanya  hivyo;  Alikabiliana  na  mambo  yale yale  tunayokabiliana  nayo  mimi  na  wewe.  Yesu  alikuwa  na  ratiba iliyojaa  shughuli. 

Yesu  alikumbana  na  watu  wajeuri  na  wanaoudhi. Yesu  alikabiliana  na  hali  ngumu.  Bila  kutaja  kwamba  alifahamu fika  kwamba  atateseka  sana  na  kufa  msalabani  kwa  ajili  ya  dhambi za ulimwengu. Lakini  ukisoma  Injili,  hutamsikia  Yesu  akisema  chochote  cha kukashifu  au kinachoweza  kuitwa kulalamika au kunung’unika. Bila  shaka  alijua  nguvu  za  maneno.  Wakati  wa  mateso  na  kifo chake ulipokaribia,  aliwaambia  wanafunzi wake  kwamba hatakuwa akiongea  nao kwa muda mrefu  kuanzia wakati  huo na kuendelea (Yohan 14:30).  

Uchoyo

Ni dhahiri katika mawazo  yetu kuonekana tuko hali bora  kuliko wengine  au kufanya vyema kuliko wanavyofanya. Uchoyo ni  kuhusu  kuwa wa  kwanza katika kila jambo, na ingawa hakuna makosa ya kutaka  kufanya vyema  zaidi,  ni makosa  kufurahia  kuwaona  wengine wakikosa kufaulu ili sisi tufaulu.Ninaamini  kwamba  uchoyo wa aina yote ni  mbaya na kwamba unasababisha matatizo.

Katika  sehemu  hii, nataka  niyalete mawazo yako kwa  aina tatu maalum za  uchoyo ambao  kwa  kawaida unapatikana  katika  ulimwengu wa  leo na  matokeo  mabaya yanayotokana na uchoyo huo. 

Shinda Uovu kwa Mema

Kinachohitajika kuwezesha uovu kupata ushindi ni watu wema kutulia na kutofanya chochote. Jimmy J.

Kutofanya lolote ni  rahisi, lakini  pia ni  hatari sana. Mahali ambapo hakuna pingamizi ya kuzuia uovu, uovu huongezeka haraka.  Sote mara nyingi huangukia mtego wa kulalamika kuhusu mambo yaliyo kasoro  katika jamii yetu na maishani, lakini  kulalamika hakufanyi kitu isipokuwa  kutuvunja  moyo  hata  zaidi.  Hakubadilishi kitu,  kwa sababu hakuna uwezo ufaao ndani yake.


Hebu  fikiria  ulimwengu  ungekuwa vipi  iwapo yale Mungu aliyofanya ni kulalamika kuhusu  kila kitu kilicho kasoro  tangu alipouumba. Lakini Mungu halalamiki. Yeye anaendelea kuwa mzuri  na kutekeleza  haki. Anajua  anaweza  kushinda uovu na uzuri! Uovu una nguvu kwa kweli, lakini uzuri una nguvu zaidi.

Twahitaji  kukoma na kutambua kwamba  Mungu  anafanya kazi  kupitia  watu Wake.  Ndio,  Mungu ni mzuri wakati wote.  Lakini Amechagua  kufanya  kazi hapa  duniani  kupitia watoto  wake.. wewe na mimi.  Ni jambo la kunyenyekeza  kutambua kwamba  anaweza kufanya  mengi iwapo  tungejitolea kupenda na kufanya  mambo mazuri wakati wote.

Tunahitaji kukumbuka kwamba  maagizo  ya Yesu’  katika  Mathayo 5:16:  “Vivyo hivyo nuru yenu  na iangaze mbele  ya  watu, wapate kuyaona  matendo yenu  mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”

Geuka Kulia, Geuka Kushoto..!

Mnamo mwaka 1987, jarida la  The Los  Angeles Times  lilichapisha kisa cha  mtu  mmoja  mwenye  umri  wa  miaka  53  aliyependa  kuteleza  juu ya  theluji.  Bwana  huyu  aliitwa  Ed  Kenan.  Kenan  alikuwa  mfanya biashara aliyependa mchezo wa kuteleza  na alikuwa anafanya mazoezi kisha ashindane katika mashindano  makubwa ya kuteleza wakati  wa    michezo  ya  Winter  Olympics. 

Lakini  kulikuwa  na  kitu kisicho cha kawaida juu ya Ed Kenan: Alikuwa kipofu. Miaka saba iliyokuwa imepita,  Kenan alipoteza uwezo wa kuona,  jicho moja nilipoteza uwezo kisha  lingine likafuata.  Upasuaji aliofanyiwa  mara  mbili haukuweza kuzuia  retina  zake zizipofushe macho yake. Katika  kukabiliana  na  matatizo hayo yasiyoneneka, Kenan  alikuwa  na  uamuzi  wa  kufanya:

Tafuta Kilicho Kizuri Katika Kila Kitu

Kuna hadithi moja niliwah sikia ya wanaume watatu waliojikuta wanafanya kazi  mahali  pa  kipekee  kabisa.  Wanaume  hawa  walikuwa  wafanya kazi wa kawaida waliokuwa wameajiriwa  ili kusaidia kujenga kanisa  kubwa la  London ambalo  ujenzi wake ulikuwa unaendelea. Kanisa  hili  kubwa  lilikuwa  nimesanifiwa  na  msanifu  majengo maarufu  kwa  jina  Sir  Christopher  Wren  na  lilikuwa  linatarajiwa kuwa kanisa  kubwa lenye  usanifu wa kipekee. Basi mwanahabari mmoja  wa  London  alipokuwa  akiandika  makala  juu  ya  kanisa  hilo kubwa lililokuwa likijengwa aliwauliza  wale  wanaume watatu  swali hili  rahisi:  “Mnafanya  nini  hapa?”  Yule  mwanaume  wa  kwanza akasema  “Ninakata  mawe  kwa  shilingi    10  kwa  siku.”  Yule  wa  pili akajibu  akasema,  “Ninafanya  kazi  hapa  kwa  saa    10  kila  siku.” Lakini  yule  wa  tatu  alitoa  jibu  tofauti  kabisa:  “Ninamsaidia  Sir Christopher  Wren  kujenga  moja  ya  makanisa  makubwa  zaidi  mjini  London.”

Ni  ajabu  sana  jinsi  mtazamo  wako  unavyoweza  kuathiri mtazamo wako  wa maisha?  Kile  unachochagua  kuamini  ni muhimu.  Yule  mfanya  kazi  wa  kwanza  aliamini  pesa  ndiyo  kitu cha msingi. Alipoulizwa juu  ya  kazi yake, jambo la  kwanza aliloliongelea  ni  kiwango cha pesa (jinsi  kilivyokuwa  cha chini) alichokuwa  analipwa. Mfanyakazi wa pili aliamini muda wake ndio uliokuwa muhimu zaidi. Alipoulizwa aeleze  alichokuwa akifanya, bila kusita aliongea  kuhusu  saa nyingi  alizokuwa anatumia kuwa kazini. 

Upendo Hutafuta Njia.

Kushindwa hakutanishinda kamwe mimi ikiwa ari yangu ya kufaulu ina nguvu za kutosha. Og Mandino

Hamu ni motisha  yenye nguvu. Imekabiliwa na ukweli  kwamba ikiwa  kwa  kweli nataka  kufanya  kitu fulani, nitatafuta  njia ya kukifanya.  Watu mara  nyingi huniuliza  jinsi  ninavyofanya  kila kitu ninachokifanya,  na  mimi  husema,  “ni kwa  sababu nataka  iwe hivyo.”  Hutambua kwamba Mungu  amenipa neema na huweka hamu moyoni mwangu,  lakini ni ukweli kwamba  nataka  nifanye mambo  fulani yanayonitia  moyo  kuyafanya.  Ninataka  kufanya  kile Mungu  anachotaka  mimi  nifanye; ninataka  kuwasaidia  watu na nataka  kutimiza  lengo langu,  au kama  mtume  Paulo asemavyo, “Nataka kukamilisha safari yangu.”