Ni dhahiri katika mawazo yetu kuonekana tuko hali bora kuliko wengine au kufanya vyema kuliko wanavyofanya. Uchoyo ni kuhusu kuwa wa kwanza katika kila jambo, na ingawa hakuna makosa ya kutaka kufanya vyema zaidi, ni makosa kufurahia kuwaona wengine wakikosa kufaulu ili sisi tufaulu.Ninaamini kwamba uchoyo wa aina yote ni mbaya na kwamba unasababisha matatizo.
Katika sehemu hii, nataka niyalete mawazo yako kwa aina tatu maalum za uchoyo ambao kwa kawaida unapatikana katika ulimwengu wa leo na matokeo mabaya yanayotokana na uchoyo huo.
Dhuluma za kingono: Annah ana umri wa miaka kumi na mitatu. Baba yake humwambia yeye ni mwanamke sasa na kwamba wakati umefika kwake kufanya yale ambayo wanawake hufanya.Anapomaliza kumuonyesha kile anachomaanisha kuwa yeye ni mwanamke, yeye huona haya, huwa na hofu na kujiona mchafu. Ingawa baba yake humhakikishia kwamba kile anachofanya ni jambo zuri, yeye hushangaa ni kwa nini humtaka aliweke jambo hilo kuwa siri na ni kwa nini linamfanya ahisi vibaya.
Huku miaka ikiyoyoma na baba yake akiendelea kumdhulumu na kumbaka, Annah hufunga hisia zake kwa hiyo hahitaji kuhisi uchungu tena.
Baba yake Annah ameuiba utoto wake, ubikira wake, uhalali wake, na bila ya mwingilio kutoka kwa Mungu, ataiba maisha yake ili kupata kile alichokitaka.
Nachukizwa mno na visa vya kina-baba kuwabaka watoto wao na visa vya watu wa familia kujamiiana tunavyosikia, lakini ukweli ni kwamba asilimia 90-95 ya visa hivyo haviripotiwi.
Nilidhulumiwa kingono na baba yangu mzazi kwa miaka mingi. Nilijaribu mara mbili tofauti kumwambia mtu fulani kilichokuwa kikitendeka kwangu na kwa vile hawakunisaidia, niliendelea kuteseka peke yangu hadi nikawa mtu mzima na hatimaye nikaanza kuzungumza hadithi yangu na watu wengine na nikapokea uponyaji kutoka kwa Mungu.Baba yangu alifariki akiwa na umri wa miaka themanini na sita bila ya kuadhibiwa kwa uhalifu alionitendea. Watu aliofanyakazi nao na aliohudhuria nao karamu na dhifa mbali mbali hawakujua alikuwa akimbaka bintiye tangu alipokuwa msichana mdogo.-Annah.
Twaona yale watu wanayofanya na kuwa haraka kuwahukumu, lakini tunajua ```chanzo cha tabia zao?```
Wanawake wengi tunaowahukumu kuwa “matatizo katika jamii” ni wahasiriwa wa kubakwa na baba zao au watu wa familia zao. Kwa mfano:
```•Asilimia 66 ya makahaba wote ni wahasiriwa wa dhuluma za kingono walipokuwa watoto.
•Asilimia 36.7 ya wanawake walio gerezani nchini Tanzania walidhulumiwa walipokuwa watoto.
•Thuluthi moja ya watoto walio dhulumiwa na kutelekezwa baadaye huwadhulumu na kuwatelekeza watoto wao wenyewe.
•Asilimia 94 ya wahasiriwa wa dhuluma za kingono huwa chini ya umri wa miaka kumi na miwili wanapodhulumiwa.
Uchungu unaosababishwa na visa vya kina baba kuwabaka watoto wao na watu wa familia kujamiiana na dhuluma za kingono ulimwenguni ni mkubwa mno na yote yalianza kwa sababu watu ni wachoyo na hawakujali ni nani atakayeumia ilimradi wamepata kile wakitakacho. Ndio, pengine hutaua, hutaiba, hutadanganya, wala kutenda vitendo vya dhuluma dhidi ya watoto, lakini kuna uwezekano kwamba u mchoyo katika njia fulani.
Ikiwa tutakuwa na msamaha wa uchoyo wetu kwa kuwaelekezea kidole cha lawama wale ambao uhalifu wao ni mbaya kuliko wetu, hatutafaulu kukabiliana na matatizo haya katika jamii hivi leo.
Kila mmoja wetu lazima achukue jukumu la kukabiliana na tabia yetu ya uchoyo, haijalishi ni wa kiwango gani au kwa njia ipi tunayoueleza..
Jimmy J.
```Mwana Mageuzi.```
No comments:
Post a Comment