Ninaamini sote twahitaji kufikiria makundi ya kujumuika nayo na kuyapanua. Twahitaji kuyapanua vya kutosha ili kujumuisha watu wa aina yote.
Hivi majuzi nilikuwa na Rafiki yangu Paul mwimbaji anayehudumu huko Birmingham, Uingereza, na tulikuwa tukinywa kahawa katika mkahawa mmoja na watu kadhaa.
Nakumbuka kuangalia mtindo wa nywele wa msichana aliyekuwa akitusubiri na kusema kweli, lilikuwa ni jambo la kushangaza ambalo sijawahi kuona. Kichwa chake chote kilikuwa kimenyolewa isipokuwa kwa kile kiitwacho mtindo wa ‘Mohawk’ kwenda chini kati kati, na zilikuwa na rangi nyeusi, samawati, nyekundu na nyeupe. Pia pua Yake , ulimi wake, mdomo, sehemu kadhaa kwenye masikio yake alikuwa amedungwa. Ninakumbuka kuhisi vibaya mno kwa sababu hakuwa na chochote sawa na mimi.
Tulikuwa tofauti kabisa hivi kwamba siwezi kufikiria chochote cha kusema kinachohusiana nami. Nilitaka kuagiza kahawa yangu na nijaribu kutomwangalia sana. Paul, kwa upande mwingine, alianza kuzungumza naye na jambo la kwanza alilosema ni, “ninaupenda mtindo wa nywele zako. Je, unawezaje kuzifanya zisimame namna hiyo?” Aliendelea kuzungumza naye na hali bora ya uhusiano ambayo haikuwa awali ikaanza kujidhihirisha. Katika muda mfupi sote tukawa huru na ningeweza kuhisi sote tunaanza kuungana katika mazungumzo na kumjumuisha katika kundi letu.
Nilijifunza funzo kubwa siku hiyo- kwamba mimi si wa “kisasa” kama ambavyo ningependa kufikiria. Pengine mimi ndiye niliyekuwa tofauti. Kwanini twajiweka sisi kuwa viwango kwa kile kinachokubalika na kudhani kwamba mtu yeyote aliye tofauti nasi lazima awe ni tatizo? Ni mtindo upi wa nywele ulio sawa, au mtindo wa nguo?
Siku moja nilianza kufikiria kuhusu kile ambacho Musa lazima alikiangalia aliporejea kutoka kwenye mlima Sinai, ambako alimaliza siku arobaini mchana na usiku akipokea Amri Kumi kutoka kwa Mungu. Nina hakika nywele zake zilikuwa zimeharibika, ndevu zake zilihitaji kunyolewa, na nguo yake na viatu zilikuwa chafu.
Ninajua ya kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa mtu wa ajabu. Aliishi jangwani peke yake na kuvaa ngozi za wanyama na kula asali na nzige. Wakati alipojitokeza, alipiga ukelele akisema, Tubuni ninyi wenye dhambi, kwa kuwa Ufalme wa Mungu u karibu!”
Biblia inatufunza kwamba tunapaswa kuwa waangalifu jinsi tunavyowahudumia wageni kwa sababu huenda tunawakaribisha malaika bila kujua (angalia EBR 13:2). Inasema tunapaswa kuwa wakarimu, wenye uhusiano mzuri, kuwa na urafiki, na neema kwao na kushiriki starehe ya nyumba zetu.
Watu wengi katika jamii hivi leo hata hawazungumzi na wageni, mbali na kuwa na urafiki nao. Ninajua, ninajua; pengine unasema, “Jimmy, tunaishi katika ulimwengu tofauti hivi leo! Hujui unayezungumza naye!” Ninatambua kuwa ni lazima utumie hekima, lakini usiruhusu hofu ikufanye usiwe na urafiki na uwe baridi. Kwa kweli unaweza kumtafuta mtu mpya kanisani, mahali pa kazi, shuleni, au katika mazingara yako na useme jambo!
Kwa kweli waweza kuzungumza na mama mzee aliyekaa katika ofisi ya daktari unaposubiri kuitwa kumuona. Anaonekana yuko na upweke; kwanini usimpe dakika kumi za kuzungumza naye na uwache akuambie kuhusu hali yake. Pengine hutamwona tena, lakini atakukumbuka. Aha, na kweli, Mungu atafurahia kile ulichomfanyia. Ndio, ni kitu kidogo, lakini ulimjumuisha!
Ikiwa ufufuo wa kweli utakuja katika kanisa lako, utafurahia kweli au utaondoka kwa sababu watu wengi watakuwa kama Jamie alivyokuwa au ni wabaya sana? Huenda watakuja kutoka kwenye makao ya muda na wasiwe na harufu nzuri, au huenda wananuka pombe na mambo mengine yasiyofaa.
Watu walioumia duniani kila mara hawaonekani wakiwa katika hali ya kupendeza wala kuwa na harufu nzuri. Wakati mwingine huonekana wakiwa katika hali nzuri lakini sio kila mara na ni lazima tukome kuwahukumu kwa jinsi tunavyowaona na Kuwa tayari kutazama mbele zaidi jinsi watu wanavyoonekana na utafute kujua ni kwanini iwe hivyo.
Jimmy J.
No comments:
Post a Comment