Thursday, 26 July 2018

Upendo Hutafuta Njia.

Kushindwa hakutanishinda kamwe mimi ikiwa ari yangu ya kufaulu ina nguvu za kutosha. Og Mandino

Hamu ni motisha  yenye nguvu. Imekabiliwa na ukweli  kwamba ikiwa  kwa  kweli nataka  kufanya  kitu fulani, nitatafuta  njia ya kukifanya.  Watu mara  nyingi huniuliza  jinsi  ninavyofanya  kila kitu ninachokifanya,  na  mimi  husema,  “ni kwa  sababu nataka  iwe hivyo.”  Hutambua kwamba Mungu  amenipa neema na huweka hamu moyoni mwangu,  lakini ni ukweli kwamba  nataka  nifanye mambo  fulani yanayonitia  moyo  kuyafanya.  Ninataka  kufanya  kile Mungu  anachotaka  mimi  nifanye; ninataka  kuwasaidia  watu na nataka  kutimiza  lengo langu,  au kama  mtume  Paulo asemavyo, “Nataka kukamilisha safari yangu.”


Waweza  kuuliza, “Je, iwapo  sina hamu hiyo?”  lazima  unayo hamu ya  kufanya  mapenzi ya  Mungu au  ungekiweka  fundisho hili chini baada  ya kusoma mlango wa  kwanza.  Ikiwa una uhusiano na  Mungu  kupitia  Yesu Kristo,  basi  una hamu  ya  kufanya  mazuri kwa  sababu amekupa  Moyo  Wake na  Roho  Yake.  Ezekieli  11:19 anaahidi hivi: “nami  nitawapa  moyo mmoja, nami nitatia roho mpya  ndani yao;  nami nitauondoa  moyo  wa  kijiwe katika  miili  yao, nami nitawapa  moyo wa  nyama;  [unaosikia na kujibu unapoguswa na Mungu  wao].” 

Twaweza kuwa walegevu, tusiotenda lolote, au  wachoyo na  tunahitaji kukabiliana na  maswala  hayo  wakati mwingine, lakini  kama  watu wamwaminio Mungu haiwezekani kuwa na moyo wa Mungu na usimwogope na kuwasaidia watu. Nadhani swali ni:  Unataka  iwe  kiasi gani?  Je, unataka yakutosha uwache mambo mengine ili upate? Hivi majuzi mwanaume mmoja  aliniambia jinsi alivyokosa furaha.  Aliendelea kuniambia kwamba  anajua  Mungu anamuita aje mahala  pakuu zaidi lakini anaonelea  kwamba  hanuii kujitolea inavyohitajika.  Nilihisi  vibaya kwa  ajili yake kwa  sababu sitaki akose furaha  iliyo upande mwingine  wa  kujitolea. Ninaomba  abadili mawazo yake.

Ikiwa  kweli  twataka  kufanya  kitu, tunatafuta  njia ya kukifanya. Ni  hadi tutakapokubali haya, tutatumia maisha yetu tukidanganywa  na  vijisababu   vyetu kuhusu ni kwa  nini hatuwezi kufanya  mambo.  Visababu ni hatari,  na  ninaamini ni moja  ya  sababu kuu  zinazotufanya tusiendelee  kama  tunavyotarajia.

Pengine ungependa kujaribu, lakini unatoa  kisababu kuhusu ni kwa  nini huwezi. Pengine unataka kuwa na muda zaidi na familia yako, lakini una sababu kuhusu  ni kwa  nini  huwezi. Unaweza  kutambua kuwa  unahitaji  kujitolea zaidi kuwasaidia  wengine na  ungetaka kufanya hivyo, lakini  kila mara kuna sababu (Visababu)  ni  kwa nini  huwezi kufanya.  Shetani ndiye anayetupatia  visababu; ni hadi tutakapotambua kwamba  hali hiyo inatufanya  tudanganyike na tusimwogope Mungu, tutakwama  katika  hali ya  kukosa  furaha,  na kutozaa matunda maishani.

Jimmy J.

No comments:

Post a Comment