Thursday, 26 July 2018

Shinda Uovu kwa Mema

Kinachohitajika kuwezesha uovu kupata ushindi ni watu wema kutulia na kutofanya chochote. Jimmy J.

Kutofanya lolote ni  rahisi, lakini  pia ni  hatari sana. Mahali ambapo hakuna pingamizi ya kuzuia uovu, uovu huongezeka haraka.  Sote mara nyingi huangukia mtego wa kulalamika kuhusu mambo yaliyo kasoro  katika jamii yetu na maishani, lakini  kulalamika hakufanyi kitu isipokuwa  kutuvunja  moyo  hata  zaidi.  Hakubadilishi kitu,  kwa sababu hakuna uwezo ufaao ndani yake.


Hebu  fikiria  ulimwengu  ungekuwa vipi  iwapo yale Mungu aliyofanya ni kulalamika kuhusu  kila kitu kilicho kasoro  tangu alipouumba. Lakini Mungu halalamiki. Yeye anaendelea kuwa mzuri  na kutekeleza  haki. Anajua  anaweza  kushinda uovu na uzuri! Uovu una nguvu kwa kweli, lakini uzuri una nguvu zaidi.

Twahitaji  kukoma na kutambua kwamba  Mungu  anafanya kazi  kupitia  watu Wake.  Ndio,  Mungu ni mzuri wakati wote.  Lakini Amechagua  kufanya  kazi hapa  duniani  kupitia watoto  wake.. wewe na mimi.  Ni jambo la kunyenyekeza  kutambua kwamba  anaweza kufanya  mengi iwapo  tungejitolea kupenda na kufanya  mambo mazuri wakati wote.

Tunahitaji kukumbuka kwamba  maagizo  ya Yesu’  katika  Mathayo 5:16:  “Vivyo hivyo nuru yenu  na iangaze mbele  ya  watu, wapate kuyaona  matendo yenu  mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”

No comments:

Post a Comment