Tunasema mwanamke mjamzito anatarajia “kujifungua.” Hivyo huanza kuandaa mipango mapema. Anatenda sawa na matarajio yake—hununua nguo, chupa, kuandaa chombo cha kumlazia mtoto, na kuandaa mahali pa kumweka ili akue.
Tunapaswa kutenda kama watu walio na matarajio. Sharti tuamke asubuhi na tuandae mipango ili Mungu afanye kitu cha ajabu.
Kwa msaada wa Mungu, tunaweza kuwaza hivi Huenda leo ndiyo siku. Siku ni hii Bwana amefanya, na kitu kizuri hakina budi kutendeka kwangu . Hata ikiwa Mungu hatakupa kile kitu ulichokiomba, jaribu kupanua mtazamo wako. Pengine unaomba kitu na huku Mungu ana kitu kingine kizuri zaidi. Usiombe tu kitu kizuri; amini na uwe na matumaini ya makubwa zaidi. Amka kila siku na useme, “Nina matarajio mazuri na ya kwamba kitu cha ajabu kitatendeka leo.
Mke/mume wangu atanibariki. Watoto wangu watakuwa na adabu. Naenda kupokea habari nzuri sana kazini. Mungu anaenda kunipa nafasi ya kumbariki mtu. Kuna baraka fulani zitakuja kwa njia ya barua. Leo naenda kupata ushindi.” Usiogope kuamini, amini, na unene baraka juu ya siku yako mara tu unapoamka. Nimeamua kukiita kitabu hiki, “Kitabu cha Matumaini mapya, nitakichapa hivi karibuni.” Ninaamini kila mtu atakayekisoma atakuwa na furaha zaidi kushinda awali.
Matumaini ni kule kuamini kwamba kitu kizuri kiko karibu kutokea! Matumaini huondoa mipaka ya matarajio yetu. Je, unatarajia mambo machache au mengi kutoka kwa Bwana? Unaweza kuwa umefika katikati ukitarajia Mungu afanye kitu. Huenda umefika katikati ukiamini kwamba kutatokea kitu kizuri, lakini nataka kukupa changamoto uamini kikamilifu na kwa moyo wako wote kwamba makubwa zaidi yatatokea kuliko awali.
Nataka kukupa changamoto uamini kwamba Mungu anaweza kukutumia kwa njia ya ajabu. Ikiwa unatunga nyimbo, kwa nini Mungu asikupe wimbo mzuri zaidi kuwahi kutungwa? Ukihubiri Neno, kwa nini Mungu asikupe ujumbe mzuri, wenye upako, hivi kwamba kila wakati unapohubiriwa, wafungwa wanawekwa huru? Ikiwa unalea watoto, kwa nini watoto wako wasije kuwa watu wanaoleta mabadiliko makubwa duniani? Kwa nini usipandishwe cheo kazini? Kwa nini usikutane na mtu yule utakayemuoa au atakayekuoa na kuwa na maisha mazuri sana? Kwa nini usiushinde uchungu uliosababishwa na watu? Kwa nini usilete mabadiliko katika maisha ya watu walio karibu nawe?
Ni wakati wa kuishi ukiwa na kiwango kipya cha matarajio yenye matumaini. Amini kwamba ikiwa kitu kizuri kinaweza kutokea kwa mtu yeyote, basi kinaweza kutokea kwako!
Jimmy J.
No comments:
Post a Comment