![]() |
Dada aliyefukuzwa kanisani kwa kuvaa vibaya. |
kiwa utawahukumu watu, huna muda wa kuwapenda. Mama Teresa
Jamie aliingia ndani ya kanisa kwenye kona ya barabara ya Spruce Avenue na barabara ya Twenty-Third huko Harbor, Illinois. Alikuwa akitafuta msaada. Alikuwa ameliona jengo la kanisa kwa muda mrefu na aliwatazama watu wakiingia na kutoka mara mbili au mara tatu kwa wiki. Jamie mara nyingi alikaa kwenye mkahawa upande wa pili wa barabara kutoka kanisa hilo, akinywa kikombe cha kahawa, akishangaa jinsi anavyoweza kukubaliwa ikiwa atakuwa na moyo wa kuingia katika moja ya ibada za kanisa.
Jamie alikuwa katika shule ya watoto ya Jumapili kanisani mara chache alipokuwa mtoto wakati alipohudhuria na jirani mmoja, lakini alifahamu machache sana kuhusu utaratibu ufaao wa kuhudhuria kanisa. Alikuwa hana hakika iwapo anafaa kuingia au atakubaliwa, kwa hiyo alikunywa kahawa yake na kutazama. Alijaribu kuona ikiwa watu wa kanisa walionekana kuwa na furaha yoyote walipotoka nje kuliko walipoingia, lakini wote waliondoka haraka kwa hiyo hakuweza kujua wazi. Mara kwa mara mtu fulani kutoka kwa ibada ya kanisa alikuja kwenye mkahawa baada ya kanisa.
Wachache kati yao walikaa peke yao na kwa kweli walionekana kuwa na upweke kama alivyohisi. Baadhi yao walikuja na watu wengine na walicheka na kuonekana kuwa na furaha, hali iliyompa tumaini kwamba huenda siku moja akawa na moyo wa kuhudhuria ibada.
Jamie alilelewa katika familia ambayo haikumjali sana. Wazazi wake wote walikuwa walevi na ingawa hawakumdhulumu, walimharibia sana kielelezo chake kwa kuwa haraka kumkashifu na kumtafutia makosa. Mara nyingi walimlinganisha na nduguye wa kiume aliyeonekana kuwa mwerevu na mwenye kipawa kuliko yeye katika kila njia. Kila mara alihisi kuwa hapendwi, ana sura mbaya, na ni mjinga, na ni kama hana thamani yoyote hata kidogo. Alipotimu umri wa miaka kumi na mitatu, Jamie alikuwa ameangukia kundi la watu wabaya na alikuwa akinywa pombe na kutumia dawa za kulevya.
Uchungu wa hisia zake ulikuwa mwingi hivi kwamba alitumia dawa za kulevya kuutuliza. Pia alianza kuwa na matatizo ya kula chakula kingi kupita kiasi na kisha kukitapika ovyo –hali iitwayo “bulimia.” Alikuwa anakula chakula kiasi cha kawaida, kingi mara moja, lakini kila mara alijilazimisha kutapika baada ya kula kwa hiyo hangenenepa. Alikuwa hajasahau siku ya kuzaliwa kwake alipotimu umri wa miaka kumi na miwili wakati mama yake alipomwangalia kwa hasira na kusema, “Sikuwa na wakati wa kukuokea keki ya siku ya kuzaliwa, lakini hata hivyo huihitaji.
Umenenepa vyakutosha!” Alikuwa hajawahi kufikiria yeye ni mnene hadi siku hiyo, lakini kila siku tangu siku hiyo, alijiangalia kwenye kioo na kuona msichana alionekana kuwa na uzani wa pauni thelathini kuliko alivyokuwa. Kielelezo chake kiliharibika kupitia mambo ambayo mama yake alikuwa akimwambia kila mara. Gredi za Jamie shuleni hazikuwa nzuri sana na hakuhisi kuwa alikuwa “mwanafunzi wa chuo,” kwa hiyo alipofuzu kutoka shule ya upili alipata kazi kwenye duka la kuuza bidhaa za matumizi ya nyumbani kwenye sehemu hiyo. Hakupata pesa za kutosha za kumwezesha kuondoka nyumbani kwao na kuweza kujitegemea kwa kuwa na makazi yake mwenyewe, lakini aliweza kununua nguo, uraibu wake wa pombe, na dawa zake za kulevya wakati alipotaka kujistarehesha. Wakati wake mwingi wa kupumzika aliepuka kuwa nyumbani kwa kukaa katika mkahawa au kutembea hapo karibu na kwao na akashangaa jinsi familia nyingine zote zilizoishi hapo zilivyokuwa.
Hakuwa na marafiki wa kweli-watu anaoweza kuwaamini na kumhesabu kuwa yeye yupo. Watu waliokuwa katika maisha yake walikuwa watumiaji, wala sio watoaji, na wengi aliwaogopa. Siku moja hatimaye alijihisi kuwa mwerevu vyakutosha kuingia ndani ya kanisa ilhali watu wengine walikuwa wamekusanyika ndani. Aliingia kwenye umati, akitumai kuwa hangetambuliwa, lakini akiwa na hamu ya kupata mtu wa kumkaribisha na kusema, “Tuna furahi kuwa nawe siku ya leo.” Aliwatambua watu waliokuwa wakimwangalia na baadhi yao walikuwa wakinong’onezana, lakini hakuna mtu aliyeonekana kuwa na urafiki. Jamie alikuwa amevaa visivyo kwa mavazi yanayopendwa na watu wengi na nywele zake zilikuwa na karibu rangi tatu tofauti. Zilikuwa nyeusi, zikiwa zina rangi nyekundu na rangi ya dhahabu. Alikuwa amevaa jeans kubwa na shati kubwa. Hakufanya hivyo kwa kupenda; alikuwa akijaribu kuficha kile alichofikiria kuwa mwili wake mkubwa. Alikuwa amevaa viatu vya wazi vya ngozi sawa na champali, ambavyo hakuna mtu aliyekuwa amevaa kanisani-hasa katika kanisa hilo! Jamie alikaa kwenye mstari wa mwisho na hakuelewa chochote kilichokuwa kikiendelea. Watu walikuwa mara wakisimama na kusoma mambo kwenye kitabu kilichowekwa vizuri kwenye kiti kirefu cha kanisani mbele yao; kisha walikaa tena.
Watu waliimba, kinanda kuchezwa na maombi na sahani la kukusanyia pesa lilipitishwa karibu na baadhi ya watu wakaweka pesa ndani yake. Mwanaume mmoja ambaye hakuonekana kuwa mwenye furaha na amekasirika kidogo alitoa mahubiri ya dakika ishirini, ambayo hakuyaelewa kabisa. Alifikiri kuwa alikuwa kasisi, lakini hakuwa na uhakika.
Hatimaye, ibada ilionekana kumalizika kwa sababu wote walisimama tena na kuimba wimbo mmoja zaidi. Alifikiri pengine mtu fulani angesema kitu kwake walipoondoka. Kwa kweli, mtu angesema kitu fulani! Kasisi alisimama mlangoni akiwasalimia watu kwa mkono walipokuwa wakiondoka kanisani na wakati Jamie alipomfikia hakutabasamu wala hata kumwangalia macho kwa macho. Alielewa kuwa anafanya kazi yake na hangelisubiri imalizike. Alipokuwa akiteremka kwenye ngazi, akatambua kuwa mwanamke mmoja anaonekana anamsubiri yeye hapo chini mwisho wa ngazi. Alihisi kuwa na furaha ya mshangao akifikiria kuwa mtu fulani amemtambua hatimaye. Mwanamke huyo alimtambua ndiyo, lakini alitambua kila kitu alichofikiria kuwa makosa kuhusu vile Jamie alivyoonekana, kwa hiyo akasema, “Jina langu ni Margaret Brown. Je, wewe unaitwa nani? Jamie alijibu kwa kusema jina lake na Margaret akaendelea kusema, “Unakaribishwa kila mara hapa, lakini nilifikiri nitakusaidia kwa kukufahamisha kwamba tunavaa vizuri wakati tunapokuja kanisani hapa Holiness Tabernacle. Hakuna jeans, hakuna viatu vya wazi kama champali, na pia unaweza kufikiria kuhusu mtindo wa nywele ambao si wa kuvutia sana. Unajua, switii, kwamba Yesu anatufunza tuwe wanyenyekevu na sio kujivutia sisi wenyewe. “Akamwonyesha Jamie tabasamu ya kejeli na kurudia kumwambia, “Unakaribishwa wakati wowote.” Jamie hakuweza kwenda kwenye mkahawa siku hiyo; ilibidi aende mahali pengine na kuwa peke yake ili alie. Alihisi kwamba sasa Mungu amemkataa pia, na alimaliza siku iliyosalia akiwaza juu ya kujiua. Alikuwa amefika mwisho chini ya shimo na alihisi kuwa hana sababu hata kidogo ya kuendelea kuishi. Majina haya yamewekwa. Lakini ulimwengu umejaa akina Jamie na makanisa ya Holiness Tabernacle na wanawake wa kidini kama Bi. Brown. Kumejaa Wakristo wanaoingia na kutoka makanisani kila wiki.
Wengi wao huenda na hawawezi kuvumilia hadi ibada imalizike. Ni watu wa kupinga, kuhukumu, na wabaguzi sana! Mungu Anampenda kila mmoja kwa Usawa Yesu pengine hakuwa katika kanisa la Holiness Tabernacle siku ambayo Jamie alikwenda kwa sababu hangefurahia pia. Lakini angelikuwa huko, angeliwatazama akina Jamie waliokuja siku hiyo. Angelikaa kando yake au kutembea karibu naye hadi mbele ili kukaa naye, na angeliuliza ikiwa ni mgeni.
Angelimweleza kila kitu asichokielewa. Angelitabasamu mbele yake kila mara alipomwangalia na, kumjua, angelimpongeza kwa mtindo wake wa kipekee wa nywele kwa sababu Yeye hupenda aina mbali mbali! Angelimwalika avuke upande wa pili wa barabara ili kunywa kikombe cha kahawa pamoja naye na kundi alilokwenda nalo kama kawaida na wakati Jamie alipoondoka angelitarajia kurudi tena juma lijalo. Lakini Yesu hakuwako siku hiyo kwa sababu hakuna aliyetenda kama vile angetenda. Hakuna aliyemwakilisha vyema; na hakuna aliyemuiga Mungu.
No comments:
Post a Comment