Makala```
Uza mwili wako ili kuwafurahisha wanaume waovu au ufe njaa. Ni chaguo baya sana ambalo mtu hapaswi kufanya.
Ingawa ana umri wa miaka kumi na tisa, Suzi amefanya chaguo hili tangu akiwa na umri wa miaka kumi na minne. Na kwa kila chaguo, moyo wake huvunjika sana na roho yake inaharibiwa. Kwa yote aliyopitia, ni miujiza kwamba bado anahisi chochote.
Anapata nguvu wakati anapoangalia macho ya bintiye wa umri wa miezi saba, Aamina, maana yake ni “salama,” na Suzi ameamua kuwa atafanya chochote awezacho kuweka ahadi yake ya kumweka binti yake salama. Hauzi mwili wake kwa tamaa au kujifurahisha. Anauza mwili wake ili aishi.
Anaishi na kufanya kazi yake katika chumba cha upana wa futi nne na urefu wa futi tisa. Amefanya kazi kwa miaka mitano… hana siku za kupumzika… Anafunga macho yake na kumfikiria Aamina, ilhali wanaume wapatao kumi na watano kwa siku huudhulumu mwili wake ili kuridhisha tamaa zao mbovu.
Uchungu huo haufikiriki, lakini ndiyo njia pekee anayojua ya kumpa chakula na mahali pa kulala.
Wakati anapofikiria kuhusu jinsi anavyompenda Aamina, hawezi kuelewa jinsi mama yake alivyomtelekeza wakati alipokuwa na umri wa miaka mitano. Kabla ya kuja kwa kile kinachojulikana kama wilaya ya taa nyekundu ( yaani eneo la ukahaba) , alikuwa anakufa njaa. “ Nilikuwa na tumaini, lakini tumaini hilo liko mbali nami. Ninajua Mungu yuko nami na ananipenda. Sijui njia nyingine yoyote ya kuishi.”
Tumaini linaloonekana kwa mbali likidumu kwa siku moja wakati maisha yasipomgharimu moyo wake, roho yake, na kuuharibu mwili wake. Hivi leo, matumaini hayo yatahitaji kusubiri. Mteja wake mwingine amewasili sasa hivi. Takwimu zasema:
• Umri wastani wa kuingia katika ukahaba kote ulimwenguni ni miaka kumi na mitatu hadi miaka kumi na minne.
• Asilimia 75 ya makahaba wako chini ya umri wa miaka Ishirini na tano.
Nilipelekwa kwenye danguro moja lenye vyumba vitatu vidogo vikiwa na vitanda vitatu kila chumba. Hakukuwa na faragha kwenye sehemu ya vitanda hivi hata kidogo. Wasichana au wanawake waliwahudumia wanaume katika vyumba hivi vidogo hasa wakati wa usiku, wakitumai kupata pesa za kutosha kuweza kula na kuwalisha watoto wao ikiwa walikuwa nao, na wengi wao walikuwa nao. Watoto wao walikuwa wapi wakati wao wakifanya kazi? Ama pengine walikuwa wakicheza karibu na ukumbi ambako wanaweza kufika kwa urahisi kwenye vyumba vya mama zao waliko au walipewa pombe ili kuwafanya walale ili wasiwajali mama zao.
Bila ya msaada, wengi wa watoto wa kike…wasichana wadogo…wataingizwa katika maisha ya ukahaba mara tu wanapokuwa wakubwa. Wanawake hawa hawaishi namna hii kwa sababu wanataka kuwa hivyo; hawana lingine la kufanya. Hawana elimu na wamelelewa katika hali ya umaskini ambao wengi wetu hatuwezi kuelewa ulivyoanza. Baadhi yao kwa kweli wanasimamiwa na wanaume ambao, kwa malengo yao, huwafanya kuwa kama wafungwa na kuwapiga ikiwa hawaleti pesa za kutosha.
Ninaweza kuongeza kwamba baadhi ya wanawake waliokomaa waliokwama katika ukahaba ni wajane. Ama waume zao wamefariki au kuawa katika baadhi ya visa na kuwaacha bila chochote cha kuwasaidia, kwa hiyo kwa mara nyingine tena wakalazimika kufanya kile wanachofikiria kinaweza kuwapa pesa. Twaweza kujifunza kufanya kilicho sawa ili kuwasaidia walionyanyaswa ulimwenguni. Kile tunachohitaji ni habari na ari na twaweza kuleta tofauti ifaayo katika maisha ya watu wengi. Ikiwa kila mmoja wetu atafanya sehemu yake twaweza kuanza mageuzi ya upendo.
Tafakari
Jiunge na mwana Mageuzi.
Jimmy J.
No comments:
Post a Comment