Kupitia Qur’an Na Biblia.
Kelele nyingi zimesikika miongoni mwetu, Waislam wakijaribu
kutuaminisha juu ya kile wanachoamini, Wanaendelea kushikilia mitazamo
yao kuhusu Uungu wa Yesu,Chanzo cha maswali yote wanayouliza juu ya
Bwana Yesu kinaanzia mara tu Yesu alipovaa mwili wa kibinadamu tendo
hilo kwa fikra za haraka tu linaweza kudhaniwa kuwa ndilo linaloshusha
mamlaka yake ya asili kama Mungu. Pamoja na hayo mimi binafsi nichoelewa
ni kuwa tendo hilo kamwe halishushi mamlaka bali linafunika mamlaka
aliyokuwa nayo kwa kadri ya sababu Ifuatayo:-
Mungu aliwahi kujifunua wazi katika nyakati za nyuma na wanadamu wakaangamia
Fuatilia:- kutoka 19:20-21 Bwana akaushukia mlima, juu ya kilele cha
mlima; Bwana akamwita Musa aende hata kilele cha mlima; Musa akapanda
juu. Ndipo Bwana akamwambia Musa, Shuka chini, uwaonye watu wasije
wakapasua njia waje kwa Bwana kutazama, kisha wengi miongoni mwao
wakaangamia.
“swali la kujiuliza”
Je! Mungu aje katika hali gani ili mwanadamu aweze kuikabili?
“Jibu”
Ni lazima aje katika hali inayofunika uwazi wa mamlaka yake iliyo ya utisho kwa mwanadamu mdhambi.
Na anapokuwa katika hali ya ubinadamu ndipo anapoona njaa, kulia,
kutembea, kusinzia na hali zote za ubinadamu anakuwa nazo na ndo maana
Yesu ni Mungu 100% na mwanadamu 100%
Fuatilia kutoka 33:18,20
(Musa) Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako…. Kisha akasema, Huwezi
kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi
Sababu hiyo ya
kimsingi ndiyo inayofanya Bwana Yesu kuchukua mwili wa kibinadamu
kupitia Mariam kama tulivyo kwishaona.
Hivyo mwili ya Bwana Yesu
ulisitiri mamlaka kuu ya Uungu wake ambayo hainge kuwa busara kuufunua
na kufanya binadamu kuangamia badala ya kuokolewa naye. Kwa kauli
nyingine ni kuwa Mungu (Yesu) alitumia mwili huo ili kuwafikia waja wake
kama tulivyoona hapo nyuma jinsi Mungu alivyojifunua hata kwa kichaka
kwa kadri ya Qur-an tukufu.
“Ubinadamu ni njia ya Mungu kusema na waja wake:”
Qur-an 42:51 ……….. Mungu husema na wajawake kwa njia ya:-
Ilhamu – sauti ya ndani ya moyo ya Mungu
Nyuma ya pazia – ishara ya kufunika mamlaka.
Kwa kadri ya Aya hiyo tunaona Qur-an ikitaja “Pazia” kama chombo cha
mawasiliano ya Mungu kwa wanadamu, pazia hii umaanisha ni kitu
kinachofunika ili kuzuia kuonekana kwa uhalisi wa jambo kwa lugha
nyingine Mungu wakati Fulani huamua kufunika uhalisi wake kwa kujifunua
nyuma ya “Pazia”.
“Pazia ni nini Kibiblia?”
Waebrania 10:20 ……….. ipitayo katika “Pazia” yaani mwili wake.
Katika Biblia Pazia huashiria mwili wa Bwana Yesu, hivyo hiyo ni njia
ya kimawasiliano kati yake na binadamu inayofunika mamlaka yake ya Asili
ya Uungu ili binadamu kumudu kukutana naye.
1Timotheo 3:16 Mungu alidhihirishwa katika mwili
Ebrania 10:5 Mwili uliniwekea tayari
Filipi 2:7 alijifanya hana utukufu …….. akawa na mfano wa mwanadamu.
Kwanini aitwe Mwana naye ni Mungu?
Tendo la Bwana Yesu kuitwa Mwana wa Mungu linaanzia kwenye chanzo cha kutwaa mwili.
Yohana 1:14 naye neno akafanyika mwili akakaa kwetu nasi tukaona utukufu wake utukufu
kama wa Mwana pekee atokae kwa baba …………..
Andiko hii linaonyesha hatua kuu mbili yaani:-
Kufanyika mwili
Kuitwa mwana atokae Mbinguni.
Sababu kuu
Tendo la Yesu kuamua kuchukua jukumu la kutuokoa lilimladhimu siyo
kufunika Utukufu wake (Uungu ) tu kwa mwili bali pia kubadili
kitambulisho chake cha mamlaka
“Fatilia mfano huu”
Maji yanaweza
kugeuka katika hali mbalimbali katika kile ninachojua maji hayo mara
yanapo badiri hali tu pia tendo hilo huambatana na kubadilli jina, yaani
mfano maji yanapoganda hayaitwi tena maji bali huitwa barafu
Swali:- Je barafu si maji?
Jibu:- la barafu ni maji ila yamebadili asili kwa muda na baadae hurejea.
Sababu ya Bwana Yesu kuitwa mwana inatokana na kusudi lake tu la kuja
Duniani Kutukomboa hivyo alifanyika barafu toka asili ya maji
(alifaninyika mwana toka asili ya Uungu kama njia ya Ukombozi) lakini
asili yake ya Uungu inabaki palepale.
Fuatilia ushauri mwingine juu ya Uungu wa bwana Yesu katika mafungu yafuatayo:-
Yohana 14:7-10……… aliyeniona mimi amemwona Baba
Tito 2:13 ……. Yesu Mungu mkuu na mwokozi wetu.
Yohana 20:28 Bwana wangu (Yesu) na Mungu wangu.
Ndugu mpendwa ninaamini hofu na mashaka ya moyo wako juu ya mada hii
yamepingwa na uondolewa kupitia uchambuzi huu, fanya maamuzi yako leo
kwa kujenga upya imani yako juu ya mamlaka ya Bwana Yesu kama tulivyo
jifunza.
Hitimisho
Yesu ni Mungu na hivyo yeyote anayehitaji
kwenda mbinguni, njia pekee na pekee tu ni Kristo Yesu-‘Matendo 4:12
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina
jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa
kwalo.
No comments:
Post a Comment