Friday, 29 June 2018

Kimbia kwenda Vitani, Usikimbie Vita

Unaposoma  kitabu cha Zaburi, moja ya mambo ya kwanza utakayoona ni  kwamba  Daudi alikuwa mtu aliyejaa  matumaini na matarajio. Unaweza kuyasikia haya katika mashairi yake aliyoandika. Hii hapa mifano michache: Iweni hodari,  na mpige moyo konde,  Ninyi nyote mnaomngoja BWANA! Zaburi 31:24 (imeongezwa msisitizo) Naam,  wakungojao  hawataaibika hata mmoja...  Zaburi 25:3 (imeongezwa msisitizo) Na  sasa,  ninangoja  nini na kutarajia  nini, Ee Bwana? Matumaini yangu ni kwako. Zaburi 39:7 (imeongezwa msisitizo)

Iwe  alikuwa  anachunga  kondoo kondeni, au  kuongoza kikosi  cha askari wasaliti, au  kutawala  kama mfalme  wa Israeli, wakati wote  Daudi aliishi akiwa  na matumaini kwamba  Mungu alikuwa  anaenda  kutenda  kitu  cha  ajabu  maishani  mwake.  Lakini matumaini ya Daudi hayakumruhusu  akae tu bila kufanya kitu chochote.  Ukweli  ni kwamba,  kufanya  kitu  ndiyo  sawa.  Matumaini yake yalimchochea  awe  mtendaji.   Daudi aliamini kwamba Mungu alikuwa atatenda kitu cha miujiza, lakini alijua  kwamba ana ubia na Mungu na kwamba  alihitaji  kutii kikamilifu. 
Hivyo tunamwona Daudi akimwomba Mungu amwonyeshe njia na kisha  kuchukua hatua za  imani  kwa  ujasiri  (1  Mambo  ya  Nyakati 14:10,  1  Mambo ya Nyakati 14:14, 1 Samweli 23:2, 2 Samweli 2:1). Hebu  fikira  ikiwa  Daudi  angekaa  tu,  bila  ari,  na  kukosa  nidhamu wakathi  alipokabiliana  na  Goliathi?  Mfikirie  Daudi  akijisemea Mmm, natumaini  Mungu  ana  kitu. Nitakaa  hapa  tu kwenye mitaro pamoja  na hawa wenzangu. 
Tuwe  na matumaini  kwamba  Mungu  atatuma radi  na kuliua hili  jitu.  Ikiwa angekuwa na mtazamo huo, Mungu angemtumia mtu  mwingine  kumshinda  Goliathi.  Mungu alikuwa anatafuta  mtu ambaye  angekuwa  tayari  kutekeleza  sehemu  yake—mtu  ambaye matumaini yake yangemchochea  kutenda jambo. Daudi alikuwa ndiye mtu huyo! Daudi alipojitokeza mstari wa mbele  kuwaletea  ndugu zake mahitaji  yao,  na  kusikia  lile  jitu  la  Kifilisti  likimtukana  Mungu  na kudhihaki  majeshi ya  Israeli,  hapo hapo, alijawa na matumaini. Aliwauliza wale  waliokuwa karibu naye, “Je!  Atafanyiwaje yeye atakayemwua  Mfilisti  huyo,  na  kuwaondolea  Israeli  aibu  hii?”  (1 Samweli  17:26).     
 
Hakuwa  anawaza  kuhusu  kushindwa;  hakuwa anawaza  kuhusu  kutofaulu;  hakuwa  anawaza  yale  magumu yaliyokuwa  yanawakabili—alikuwa  na  matumaini  kwamba angefaulu na kwamba angevishinda vita hivyo.Matumaini hayo yalimfanya Daudi atende  jambo.  Kati ya wakati  ule  alipohisi kuwa na matumaini na wakati  ule  ushindi ulipopatikana,  angalia  hatua  za  utendaji  alizozichukua:  Daudi alipinga ukosoaji kutoka kwa kaka yake aliyejaribu kumdunisha  na kumvunja  moyo  (kif.  28-30);  alimshawishi  Mfalme  Sauli  amruhusu kwenda  kupiga  vita  (kif.  32-37);  alijaribu  kuvaa  silaha  za  Sauli  lakini akaamua  kutozitumia  (kif.  38-39);  alichagua  mawe  matano  kama risasi  za  kombeo  lake  (kif.  40);  alimdharau  Goliathi,  na  akatabiri ushindi  (kif.  45-47);  na  akakimbia  kwenda  vitani  (kif.  48).  

Daudi hakuwa  na mtazamo wa  Mmm, natumai  mambo  yatakwenda  vizuri. Hebu  natusubiri  tuone.  Alikuwa  na mtazamo wa  Matumaini  yangu ni katika  Mungu. Natwende  tukashinde  vita  hivi!  Daudi  hakuturoka vita  au kujificha  kama  walivyofanya  wale  askari;  alikimbia  kwenda  vitani akiwa amejaa  matumaini  na imani kwamba Mungu  angempa ushindi dhidi ya  lile  jitu.  Daudi  alikuwa na  matarajio  mazuri kwamba kitu kizuri kitatokea!

No comments:

Post a Comment