Twaweza kumfanya Roho Mtakatifu ahisi kuhuzunika kupitia hasira yetu, kupandwa na ghadhabu, kutosamehe, uchungu, kubishana, na wasi wasi. Biblia inatuhimiza tuwache mambo mabaya ya aina yoyote. Inanihuzunisha kufikiria kwamba ninaweza kumhuzunisha Roho Mtakatifu wa Mungu. Wakati ninapokumbuka jinsi nilivyokasirika kwa urahisi wakati fulani, najua nilimhuzunisha, na sitaki kufanya hivyo tena. Njia pekee ninayoweza kujiepusha na jambo hili ni kuwa mkakamavu kuhusu kuachilia hisia mbaya nilizo nazo kwa wengine mara tu zinaponijia.
Twapaswa kuwa watu wenye manufaa, wa kusaidia, na kuwa wakarimu kwa wengine, kusameheana na kuwa huru kama Mungu katika Kristo alivyotusamehe (angalia EFE 4:30-32). “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi. Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.” Hasira yetu humfanya Roho Mtakatifu kuhuzunika sio tu kwa sababu Mungu anatutaka tupendane bali kwa sababu najua inavyotuathiri, na anataka tufurahie maisha ya uhuru.
Twapaswa kumuiga Mungu na kufuata mfano wake. Yeye si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, na husamehe haraka. Hasira yetu haiimarishi usafi anaotutaka Mungu tukae ndani yake. Kama vile upendo halisi haujalishi jinsi tunavyohisi, msamaha wa kweli pia haujali hisia. Mambo yote haya mawili yanategemea uamuzi tunaofanya, sio hisia tulizo nazo. Nimejifunza kwamba ikiwa nimechagua kusamehe, hisia zangu hatimaye zitafuata uamuzi niliofanya.
Kuwasamehe wengine huniwezesha kuongea nao kuliko kuwanyamazia na kuwafungia nje ya maisha yangu. Huniruhusu kuwaombea na kuongea baraka kuwahusu kuliko mambo mabaya, na maovu. Twazingatia sana hisia zetu. Badala yake, twapaswa kukumbuka kwamba hisia zetu hubadilika haraka. Kisichobadilika ni upendo.
No comments:
Post a Comment