Sunday, 17 June 2018

JE,  UNAFAA  KUAMINI  NINI?

Amini kwamba  Yesu  alifanya kile Biblia inasema.  Amini kwamba ni kweli yeye ni Mwana wa Mungu, aliyezaliwa na bikira. Aliichukua dhambi ya mwanadamu. Alikuwa dhabihu yetu na akafa Msalabani. Hakubaki kwa wafu.  Alikaa kaburini siku tatu.  Wakati huo aliingia jehanamu na kumshinda Shetani. Haya yote aliyafanya kwa hiari yake mwenyewe kwa sababu alimpenda Babake (Mungu) na kwa sababu Mungu na  Yesu walitupenda wewe na mimi sana kiasi ya kwamba ncha ya mpango wowote wa kuleta wokovu ungefi kiwa katika harakati za kuleta ukombozi.

Haikujalisha ni hatua gani iliyostahili kuchukuliwa, mradi tu watu wa Mungu wawe huru tena.  Hilo ndilo jambo lililokuwa muhimu kabisa. Yesu  alilipa deni  ya dhambi zetu msalabani na kwenda Jehanamu kwa niaba yetu. Hatimaye, sawa na jinsi Mungu alivyokuwa ameahidi, siku ya tatu,  Yesu alifufuka kutoka kwa wafu.

Kilichotokea Msalabani 
Yesu alipokuwa ameangikwa msalabani, alichukua dhambi yetu. Mungu hawezi kukaa kwenye dhambi.  Yesu alipochukua dhambi yetu, alitengwa na uwepo wa Babake. Jambo hili lilikuwa limemfanyikia  Amini kwamba  Yesu  alifanya kile Biblia inasema. Amini kwamba ni kweli yeye ni Mwana wa Mungu, aliyezaliwa na bikira. Aliichukua dhambi ya mwanadamu. Alikuwa dhabihu yetu na akafa Msalabani.
Hakubaki kwa wafu.  Alikaa kaburini siku tatu.  Wakati huo aliingia jehanamu na kumshinda Shetani. Haya yote aliyafanya kwa hiari yake mwenyewe kwa sababu alimpenda Babake (Mungu) na kwa sababu Mungu na  Yesu walitupenda wewe na mimi sana kiasi ya kwamba ncha ya mpango wowote wa kuleta wokovu ungefi kiwa katika harakati za kuleta ukombozi. Haikujalisha ni hatua gani iliyostahili kuchukuliwa, mradi tu watu wa Mungu wawe huru tena. 

Hilo ndilo jambo lililokuwa muhimu kabisa. Yesu  alilipa deni  ya dhambi zetu msalabani na kwenda Jehanamu kwa niaba yetu. Hatimaye, sawa na jinsi Mungu alivyokuwa ameahidi, siku ya tatu,  Yesu alifufuka kutoka kwa wafu. Kilichotokea Msalabani Yesu alipokuwa ameangikwa msalabani, alichukua dhambi yetu. Mungu hawezi kukaa kwenye dhambi.  Yesu alipochukua dhambi yetu, alitengwa na uwepo wa Babake. Jambo hili lilikuwa limemfanyikia  Adamu pia katika bustani ya Edeni.  Alipofanya dhambi, uwepo wa Mungu ulimwondokea.

Mungu hawezi kuishi na dhambi. Dhambi hujenga ukuta kati ya mwanadamu na Mungu. Yesu alikuwa akibeba dhambi zako na za watu wengine wote alipokuwa akihisi hali hii ya kutokuwepo kwa uwepo wa babake. Alisema “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”

Angalia Mathayo mtakatifu 27:46).  Yesu alijua itatendeka hivi, lakini  tisho la kutengwa lilikuwa jambo la kugutusha kupita kiasi alipotenganishwa na  uwepo ung’aao wa Mungu Baba, na hilo ndilo jambo lililomfanya kupaza sauti ya kilio hiki. Aliitoa Roho yake kwa Babake na akafa.  

Kwa hiyo wakauchukua  Mwili wake na wakaulaza kaburini na  Roho yake ikaenda jehanamu kwa sababu hapo ndipo tungestahili kuenda. Kumbuka mwanzo wa kitabu hiki, nilisema ukifa, ni mwili wako unaopatwa na mauti. Nafsi na Roho yako huenda mbinguni au jehanamu. Hakuna tumaini la kwenda mbinguni kwa yeyote yule isipokuwa aamini ukweli huu. Huwezi kwenda mbinguni isipokuwa uamini kwa moyo wako wote kwamba  Yesu aliteswa kwa ajili yako. Alichukua mahala pako, na kuchukua adhabu uliyostahili kupata.  Alichukua dhambi zako.  

Alilipa deni lako. Alikufanyia hayo kwa sababu anakupenda. 
Yohana Mtakatifu 3:16 inasema “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yesu alienda jehanamu kwa ajili  yako. Alikufa  kwa  ajili  yako. Alilipa deni ya dhambi zako. Mungu alikuwa mwaminifu kwa Yesu. Mungu alifanya kile alichokuwa amemwambia  Yesu atafanya. Alimfufua kutoka kwa wafu. Lakini hadi wakati hayo yalitimia, alikuwa peke yake kwa siku tatu akitimiza mahitaji ya koti za haki na kuyashinda majeshi ya kuzimu. Alichukua funguo za mauti na kifo. 
Aliwahubiria wafungwa waliokuwa wamesetwa huko paradiso.  Aliwatoa kwa ushindi.Siku ya tatu, alifufuka kutoka kwa wafu. Baada ya kufufuka kwake aliingia mbinguni akiwa na damu yake na kuiwasilisha kama kumbukumbu ya milele kwamba damu isiyokuwa na dhambi ilimwagika kulipia dhambi ya mwanadamu kwa sababu uhai uko katika damu (Mambo ya  Walawi 17:11).
Turudi Kwa Kuamini Je ni kitu gani kingine unachohitaji kuamini? Amini alifanya haya kwa ajili yako. Amini hayo moyoni mwako.  Akili yako haiwezi kuelewa haya ninayokuambia, lakini amini kwa moyo wako.

Sikiza moyo wako (roho yako). Warumi 10:9 inasema kwamba ikiwa utakiri kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana na uamini kwa moyo wako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka (zaliwa mara ya pili). Kufikia hapa, ikiwa umeamua kwamba unaamini yale ninayokuambia na unataka kumpokea  Yesu, unahitaji kusema kwa sauti:   Ninaamini Yesu ni Mwana wa Mungu. Ninaamini  Alikufa kwa ajili yangu. Ninaamini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Warumi 10:10 inasema kwamba ni kwa moyo mtu huamini  hata kupata haki.  Neno haki humaanisha anafanyika kana kwamba hajawahi kutenda dhambi; inamaanisha kutakaswa, na kuwa na haki mbele za Mungu. Ni kwa kumwamini  Yesu pekee na yote aliyoyafanya kutakao kufanya uhesabiwe kama mwenye haki.
Hakuna kiasi chochote cha matendo mema kitakachokupa haki mbele za Mungu.  Kuenda kanisani pekee hakutakupa haki. Kwanza, lazima upate haki kupitia kwa imani, ndiposa matendo mazuri yafuate kama ishara ya kubadilika rohoni.

Roho yako lazima iwe sawa kwanza. Lazima uamini kwa moyo wako, yaani mtu wako wa ndani. Warumi 10:10 inaendelea kusema unahitaji kukiri kwa kinywa chako ili kuthibitisha  Wokovu. Kuthibitisha yamaanisha “kustawisha.” Kusema kile unachoamini hukithibitisha kuwa chako. Ni kana kwamba inasisitiza ni chako.
Mukhutasari
Ili uzaliwe mara ya pili lazima uamini:
•  Mungu yupo. (Mwanzo 1:1;  Waebrania 11:6)
•  Yesu ni Mwana wa Mungu, aliyezaliwa na bikira, akazaliwa kwa mwili na damu. (Mat.1:18; Mat.1:23).
•  Yesu ni Mungu, mmoja wa Utatu, mmoja wa Mungu Mwenyezi. (Wakolosai2:9,10; Waebrania  1:5-8)
•  Alikuja katika mwili ili amsaidie mwanadamu (Yohana 1:1; Yohana 1:14; Luka 4:18-21).
•  Alichukua dhambi zako zote mwilini mwake msalabani. (Isa 53:4,5; 1Wakorintho 5:21)
•  Alikufa kwa ajili ya dhambi zako. (Waebrania 2:9)
•  Alienda kuzimu na kupata ushindi pale, alimshinda adui. (Matendo 2:31)
•  Siku ya tatu, alifufuka  kutoka kwa wafu. (Luka 24:1-7; Matendo 2:32)
•  Sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba huko mbinguni. (Waebrania 10:12)
•  Yuko tayari kumkubali yeyote atakayemwamini. (Warumi 10:13; Yohana  1:12)
•  Atakuja na kuishi ndani yako kwa uwepo na nguvu za Roho Mtakatifu, akiishi katika roho yako ya kibinadamu, akikufanya hai tena kwa Mungu. (Warumi 8:14-16)* Hii ndiyo maana ya kuzaliwa mara ya pili. Ukiamini haya basi unaweza kufanya yafuatayo:
•  Kubali wewe ni mwenye dhambi anayehitaji Mwokozi.  (Warumi  3:23,24).
•  Kiri dhambi zako kwa Mungu sasa. (1Yoh 1:9).
•  Kuwa na nia ya kutubu - nia ya kugeuka kutoka kwa dhambi zako kwa hiari yako mwenyewe na kuwa na nia ya kumuishia Mungu - maisha mapya. (Matendo ya Mitume 3:19).

Tuombe Katika waraka wa  Yakobo 4:2 Bilia inasema kwamba “Hamna kitu kwa kuwa hamuombi.”  Muombe Yesu aingie moyoni mwako; muombe akusamehe dhambi zako.  Atakusamehe na kuja kuishi rohoni mwako. Roho yako itakuwa hai kwa Mungu. Ufuatao ni mfano wa ombi ambalo unaweza kuomba. Hata hivyo na kuhimiza umwambie Mungu yaliyo Moyoni mwako kwa kutumia maneno yako mwenyewe. 

*  Unahimizwa uangalie maandiko haya ikiwa una Biblia.Waacha neno la Mungu likushawishi
Mungu Baba, naamini Yesu Kristo ni Mwana wako, Mwokozi wa ulimwengu. Naamini  Alikufa msalabani kwa ajili yangu, na alibeba dhambi zangu zote.  Alikwenda kuzimu na kushinda kifo na kaburi. Naamini Yesu alifufuka kutoka kwa wafu na sasa ameketi mkono Wako wa kuume. Nakuhitaji Yesu. Nisamehe dhambi zangu, niokoe, kuja uishi ndani yangu. Nataka kuzaliwa mara ya pili. Kama unaamini ukweli huo na umefuata mwongozo tuliozungumzia: Pongezi, Umezaliwa mara ya pili!

No comments:

Post a Comment