Biblia inaelezea hadithi kuhusu mwanaume mmoja ambaye hakumfuata Mungu kwa sababu kufanya hivyo lilikuwa ni jambo la usumbufu kwake. Mwanaume huyu aitwaye Feliki, alimtaka Paulo aje na amhubirie injili. Lakini wakati Paulo alipoanza kuzungumza naye kuhusu maisha yaliyonyooka, usafi wa maisha, na kudhibiti hamu alizo nazo, Feliki alishangaa na kuogopa. Alimwambia Paulo aende zake na kwamba atamwita wakati ufaao zaidi (angalia MDO 24:25). “Na Paulo alipokuwa akitoa hoja zake katika habari ya haki, na kuwa na kiasi na hukumu itakayokuja, Feliki akawa na hofu akajibu, Sasa enenda zako, nami nikipata nafasi nitakuita.”
Ninashangazwa mno na jambo hili, sio kwa sababu linafurahisha, bali kwa sababu laonyesha wazi jinsi tulivyo. Hatujali kusikia kuhusu jinsi Mungu alivyo na upendo mwingi kwetu na kuhusu mipango mizuri aliyo nayo katika maisha yetu, lakini wakati anapoanza kutulaumu kwa makosa tunayofanya au kuturekebisha.
kwa njia yoyote, tunajaribu kumwambia kwamba “sasa” sio wakati mzuri. Nina shaka kuwa Yeye huchagua wakati tunaodhani, “ni mzuri,” na nafikiri hufanya hivyo kwa kusudi lake! Wakati wana wa Israeli walipokuwa wakisafiri kupitia jangwani, waliongozwa na Mungu ndani ya wingu mfano wa nguzo wakati wa mchana na ndani ya moto mfano wa nguzo wakati wa usiku. Wakati wingu lilipoenda, pia nao walienda na wakati liliposimama, walikaa mahali walipofika. Jambo la kufurahisha ni kwamba hakukuwa na mtindo au mpango waliofahamu kuhusu ni wakati gani wingu hilo litaenda. Walilazimika kuondoka wakati wingu linaenda (angalia HES 9:15-23).
Biblia inasema kwamba wakati mwingine lilienda wakati wa mchana na wakati mwingine lilienda wakati wa usiku. Wakati mwingine lilipumzika kwa siku chache na wakati mwingine lilipumzika kwa siku moja. Nina shaka kuu kwamba wakati wa usiku waliweka ishara isemayo “Usisumbue” kwenye milango ya mahema yao ili Mungu afahamu kuwa hawakutaka kukatiziwa wapendavyo. Wakati Alipoamua ni wakati wa kupata ufanisi walikusanya virago na kumfuata, na wakati Anapoamua ni wakati wetu kwenda kwenye kiwango cha pili cha safari ndani Yake, hatupaswi kusema, “Huu sio wakati mzuri!” Je, halingekuwa jambo zuri iwapo Mungu angelitoa kalenda ya kila mwezi inayoonyesha siku zote zinazoenda ili wajiandae kimawazo, kihisia na kimwili?
Ninashangaa ni kwa nini Hakufanya hivyo. Je, ni kwa sababu hutukatiza kwa kusudi lake ili aone jinsi tutakavyojibu? Mungu anajua vyema na wakati wake kila mara ni sawa kabisa. Kwa vile sijihisi kuwa tayari kushughulikia jambo fulani maishani mwangu haimaanishi kuwa siko tayari. Mungu ndiye kiongozi wa “njia na namna” ya mipango yetu. Njia zake sio njia zetu, lakini ni za juu na bora kuliko njia zetu (angalia Isaiah 55:9).
No comments:
Post a Comment