Yesu alipokuwa ameangikwa msalabani, alichukua dhambi yetu. Mungu hawezi kukaa kwenye dhambi. Yesu alipochukua dhambi yetu, alitengwa na uwepo wa Babake. Jambo hili lilikuwa limemfanyikia Adamu pia katika bustani ya Edeni. Alipofanya dhambi, uwepo wa Mungu ulimwondokea. Mungu hawezi kuishi na dhambi. Dhambi hujenga ukuta kati ya mwanadamu na Mungu. Yesu alikuwa akibeba dhambi zako na za watu wengine wote alipokuwa akihisi hali hii ya kutokuwepo kwa uwepo wa babake. Alisema “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” (Angalia Mathayo mtakatifu 27:46).
Yesu alijua itatendeka hivi, lakini tisho la kutengwa lilikuwa jambo la kugutusha kupita kiasi alipotenganishwa na uwepo ung’aao wa Mungu Baba, na hilo ndilo jambo lililomfanya kupaza sauti ya kilio hiki. Aliitoa Roho yake kwa Babake na akafa. Kwa hiyo wakauchukua Mwili wake na wakaulaza kaburini na Roho yake ikaenda jehanamu kwa sababu hapo ndipo tungestahili kuenda.
Kumbuka mwanzo wa somo hili, nilisema ukifa, ni mwili wako unaopatwa na mauti. Nafsi na Roho yako huenda mbinguni au jehanamu. Hakuna tumaini la kwenda mbinguni kwa yeyote yule isipokuwa aamini ukweli huu.
Huwezi kwenda mbinguni isipokuwa uamini kwa moyo wako wote kwamba Yesu aliteswa kwa ajili yako. Alichukua mahala pako, na kuchukua adhabu uliyostahili kupata. Alichukua dhambi zako. Alilipa deni lako. Alikufanyia hayo kwa sababu anakupenda. Yohana Mtakatifu 3:16 inasema “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yesu alienda jehanamu kwa ajili yako. Alikufa kwa ajili yako. Alilipa deni ya dhambi zako. Mungu alikuwa mwaminifu kwa Yesu. Mungu alifanya kile alichokuwa amemwambia Yesu atafanya. Alimfufua kutoka kwa wafu. Lakini hadi wakati hayo yalitimia, alikuwa peke yake kwa siku tatu akitimiza mahitaji ya koti za haki na kuyashinda majeshi ya kuzimu. Alichukua funguo za mauti na kifo. Aliwahubiria wafungwa waliokuwa wamesetwa huko paradiso. Aliwatoa kwa ushindi.
Siku ya tatu, alifufuka kutoka kwa wafu. Baada ya kufufuka kwake aliingia mbinguni akiwa na damu yake na kuiwasilisha kama kumbukumbu ya milele kwamba damu isiyokuwa na dhambi ilimwagika kulipia dhambi ya mwanadamu kwa sababu uhai uko katika damu (Mambo ya Walawi 17:11).
Turudi Kwa Kuamini Je ni kitu gani kingine unachohitaji kuamini? Amini alifanya haya kwa ajili yako. Amini hayo moyoni mwako. Akili yako haiwezi kuelewa haya ninayokuambia, lakini amini kwa moyo wako. Sikiza moyo wako (roho yako). Warumi 10:9 inasema kwamba ikiwa utakiri kwa kinywa chako kwamba Yesu ni Bwana na uamini kwa moyo wako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka (zaliwa mara ya pili).
Kufi kia hapa, ikiwa umeamua kwamba unaamini yale ninayokuambia na unataka kumpokea Yesu, unahitaji kusema kwa sauti: Ninaamini Yesu ni Mwana wa Mungu.
Ninaamini Alikufa kwa ajili yangu. Ninaamini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Warumi 10:10 inasema kwamba ni kwa moyo mtu huamini hata kupata haki. Neno haki humaanisha anafanyika kana kwamba hajawahi kutenda dhambi; inamaanisha kutakaswa, na kuwa na haki mbele za Mungu. Ni kwa kumwamini Yesu pekee na yote aliyoyafanya kutakao kufanya uhesabiwe kama mwenye haki.
Hakuna kiasi chochote cha matendo mema kitakachokupa haki mbele za Mungu. Kuenda kanisani pekee hakutakupa haki. Kwanza, lazima upate haki kupitia kwa imani, ndiposa matendo mazuri yafuate kama ishara ya kubadilika rohoni. Roho yako lazima iwe sawa kwanza. Lazima uamini kwa moyo wako, yaani mtu wako wa ndani. Warumi 10:10 inaendelea kusema unahitaji kukiri kwa kinywa chako ili kuthibitisha Wokovu. Kuthibitisha yamaanisha “kustawisha.” Kusema kile unachoamini hukithibitisha kwa kinywa chako. Ni kana kwamba inasisitiza ni chako.
No comments:
Post a Comment