Sunday, 17 June 2018

UAMUZI MUHIMU ZAIDI UTAWAHI KUFANYA

Ningependa kuzungumza nawe kuhusu uamuzi muhimu zaidi. Kusema kweli, huu ndio uamuzi muhimu kabisa ambao utawahi kukabiliana nao. Uamuzi huu ni muhimu zaidi kuliko chaguo la shule utakayoenda, chaguo la kazi, ni nani utakayeoa, au ni wapi utakapoishi. 

Uamuzi huu unahusu mahali utakapokuwa milele.  Hebu lifi kirie jambo hili.  Milele ni muda mrefu, mrefu sana. Watu wengi wanajishughulisha tu na mambo ya leo, au ya miezi michache. 
Wengi wanashughulikia swala la watakapostaafu.Ningependa kuzungumza zaidi ya hayo.  Ningependa kuzungumza kuhusu “maisha baada ya kufa.” Je unashughulikia swala hilo? Je, wajua kwamba wewe sio nyama na mifupa tu, damu na misuli?  Wewe ni roho, una nafsi na unaishi katika mwili. Utakapokufa, ambalo ni jambo litamkumba kila mmoja wetu, mwili wako utalazwa kaburini.  Utaharibika na kuwa majivu na mavumbi.  Lakini je ni vipi kuhusu “yule wewe wa kweli” – wewe uliye ndani, utu wako, akili, hiari na hisia? Sehemu yako ya kiroho ni sehemu ile ya utu wako ambayo haionekani kwa macho ya miili yetu.  Sehemu yako hii ndiyo itakayoishi milele.

  • Na mahala roho yako itaishi kunategemea uamuzi utakaofanywa unaposoma somo Hili. Kuna nguvu za aina mbili ulmwenguni-wema na uovu, haki na makosa.Tuna “ufahamu” wa hayo ndani yetu hata bila kuambiwa.  Kuna nguvu za aina mbili katika ulimwengu wa kiroho  Mungu na Ibilisi; malaika wema ambao ni viumbe vilivyoumbwa na Mungu kutimiza kazi yake, na malaika wabaya, wanaoitwa mapepo. Wakati mmoja malaika hawa wabaya walikuwa wema lakini wakaamua kumuasi Mungu. 

Lusifa, malaika mkuu (ambaye pia anaitwa Belzebabu, Shetani au Ibilisi), aliwaongoza malaika hawa katika uasi huu naye Mungu akawatupa nje ya Mbingu na kuwatengenezea mahala pao na bwana wao paitwapo Jehanamu.  (Angalia Ufunuo 12:7-9)  Mungu na malaika wema wana makao yao huko mbinguni.  Shetani na  malaika hawa waovu wana makao yao huko Jehanamu. Kati ya  mbingu na jehanamu kuna dunia na anga. Malaika wema na wale waovu huizunguka dunia kila wakati.

Shetani pia huzungukazunguka hapa na pale kama simba angurumaye akitafuta mtu ammeze. Bibilia yatuambia haya katika  Waraka wa kwanza wa Petro 5:8.Roho Mtakatifu wa Mungu (Roho wa Mungu mwenyewe) pia  yupo duniani na hata mbinguni, na kazi aliyopewa na Mungu ni kuwatia muhuri, kuhifadhi, kuwatunza,  na kuwalinda watu wa Mungu (wale waliochagua kumtumikia Mungu). Roho Mtakatifu pia ana kazi ya kuwavuta na kuwaletea watu ambao bado hawajamchagua Mungu na njia yake ya kuishi.

Je umefanya chaguo lako? Chaguo ni lako.  Hakuna mtu atakayekuamulia. Mungu alikuumba na akakupa hiari, na hatakulazimisha kumchagua yeye. Hakuwalazimisha malaika. Baadhi yao waliasi, na akawaacha wafanye yale waliyotaka. Lakini kumbuka, chaguo lisilofaa lina adhabu yake.

No comments:

Post a Comment