Kutoa na kuishi katika hali ya kujitolea kwatoa mavuno katika maisha yetu. Hakuna makosa ya kutamani na kutarajia mavuno. Motisha yetu ya kuwasaidia watu wengine haipaswi kuwa ya kujipatia kitu fulani sisi wenyewe, lakini Mungu anatuambia tutavuna kile tulichopanda na tunaweza kutazamia manufaa hayo. Moja ya maandiko yanayoelezea ukweli huu kwa njia nzuri sana yanapatikana katika kitabu cha Luka 6:38; “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu, Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.”(KJV).
Mungu anaahidi kuwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii (angalia EBR 11:6). Neno thawabu katika maandiko asili ya Kigiriki ya Agano Jipya, linamaanisha “ujira unaopokewa katika maisha haya” au “fidia.”
Katika lugha ya kiibrania, ambayo Agano la Kale iliandikwa, neno thawabu linamaanisha, “tunda, mapato, bidhaa, malipo au matokeo.” Neno thawabu limetumiwa mara 68 katika Biblia ya ‘Amplified Bible’. Mungu anatutaka tutazamie thawabu za kumuogopa na chaguo zuri. Ikiwa tunawajali wale ambao ni maskini na walionyanyaswa, Mungu anaahidi kwamba “Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu, Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi.” (MIT 28:27). Mwandishi wa Mithali hata anasema “Amhurumiaye maskini humkopesha BWANA; Naye atamlipa kwa tendo lake jema” (angalia MIT 19:17). Sidhani kuwa Mungu halipi riba kuu kwa kile anachokopeshwa.
Ninakuhimiza ufanye kazi ulete haki kwa walioonewa. Hiyo inamaanisha kwamba wakati unapoona kitu unachojua kuwa hakiko sawa, unafanya kazi ili kukiweka sawa.
No comments:
Post a Comment